Ndugu msomaji,
Katika somo hili tutajifuinza kwa ufupi kuhusu Mitume 12 wa Yesu Kristo.
Mtume wa Yesu Kristo (kwa Kigiriki ἀπόστολος, apóstolos, aliyetumwa), kadiri ya Agano Jipya, ni mmojawapo kati ya wale wanaume 12 ambao Yesu aliwateua mapema akawatuma kuhubiri Ufalme wa Mungu kwanza kwa taifa la Israeli, halafu kwa mataifa yote duniani.
Neno “mtume” lamaanisha mwanafunzi au mfuasi. Neno “mtume” la maanisha “mtu aliyetumwa nche.”
Huku Yesu akiwa ulimwenguni, wafuasi wake kumi na wawili waliitwa mitume. Mitume kumi na wawili walimfuata Yesu Kristo, wakajifunza kutoka kwake, na wakaelimishwa naye. Baada ya kufufuka kwake na kupaa kwake angani, Yesu akawatuma mitume wake nche na kuwa mashahidi (Mathayo 28:18-20; Matendo Ya Mitume 1:8). Hapo basi wakaitwa mitume kumi na wawili. Ingawa, wakati Yesu alipokuwa ulimwenguni, neno “wanafunzi” na “Mitume” yalitumika kwa ubadilisho.
Mungu ndiye mwenye haki ya kutuma Mitume, na tunaona hapa kuwa Yesu na yeye alikuwa na Mitume. Kumbe basi Yesu hakuwa Mtu wa kawaida tu bali alikuwa Mungu na ndio maana alikuwa na MITUME.
Luka 6:12-16Neno: Bibilia Takatifu (SNT) 12 Siku moja Yesu alikwenda milimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. 13 Asubuhi akawaita wanafunzi wake, na kati yao akachagua kumi na wawili akawapa cheo cha “mitume.” Majina yao ni haya: 14 Simoni, aliyemwita Petro; Andrea, nduguye Simoni; Yakobo; Yohana; Filipo; Bartholomayo; 15 Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Simoni, aliyeitwa Mzalendo; 16 Yuda, mwana wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ambaye baadaye alimsaliti Yesu.
Vile vile, Mitume halisi kumi na wawili wameoredheshwa katika Mathayo 10:2-4, “Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo; Simoni mkananayo, na Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti.”
Bibilia pia yaorodhesha hao mitume kumi na wawili katika Marko 3:16-19 na Luka 6:13-16. Linganisho la fahamu hizi tatu laonyesha tofauti chache katika majina. Inaonekana Thadayo pia aliitwa “Yuda, mwana wa Yakobo” (Luka 6:16) na Lebayo (Mathayo 10:3). Simoni mfarisayo pia aliitwa Simoni Mkananayo (Mariko 3:18). Yuda Iskariote ambaye alimsaliti Yesu, nafasi yake ilichukuliwa na Mathiya (angalia Matendo Ya Mitume 1:20-26). Walimu wengine wa Bibilia wanamwona Mathiya kama mtume ambaye “hastahili” na wanaamini kuwa Paulo alikuwa chaguo la Mungu kumpadilisha na Yuda Iskariote kama mtume wa kumi na mibili.
Mitume kumi na wawili walikuwa watu wa kawaida waliotumika kwa njia ya kipeke. Kati ya hoa kumi na wawili, kulikuwa na wavuvi, watoza ushuru, na wapinduzi. Injili inanakili, makosa ya kila muda, magumu, na shuku ya hao wanaume kumi na wawili waliomfuata Yesu Kristo. Baada ya kushuhudia kufufuka kwa Yesu na kupaa kwake Yesu angani, Roho Mtakatifu aliwabadilisha mitume kumi na wawili kuwa wanaume wa Mungu wenye nguvu ambao waligeuza ulimwengu juu chini (Matendo Ya Mitume 17:6). Kulikuwa na badiloko gani? Mitume kumi na wawili “walikuwa na Yesu” (Matendo Ya Mitume 4:13). Ni maombi yangu kuwa tuambiwe ujumbe huo huo.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment