Katika Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu na1, Hadithi na 104 uk. 64 “ Hadithi ya Ibn Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Nilimuona Musa (a.s) katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua.Na nilimuona Isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……”
YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU.
Matendo 4:9-10,12 “ kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…………………….Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa a.s aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya kipofu Batromayo.
Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao? Yesu alimfufua Lazaro.
Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la Yesu Kristo wa Nazareth lenye wokovu?
Matendo 16:31 “ Wakamwambia , Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.”
Shalom,
Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu.
No comments:
Post a Comment