……………..
Tangu Mungu alipoanzisha Agano na Israeli pale Sinai (Agano la Kale), daima amekuwa anawasiliana na wanadamu kupitia MAKUHANI. Kunakuwa na KUHANI MKUU na makuhani walio chini yake.
……………
Kati ya kabila 12 za Israeli, aliiteua kabila ya Lawi wawe ndio makuhani.
Kumb 10:8 Na wakati huo Bwana aliitenga kabila ya Lawi … wasimame mbele ya Bwana kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.
……….
Hesabu 1:50 lakini uwaweke Walawi wawe juu ya maskani ya ushahidi, na juu ya vyombo vyake vyote, na juu ya vitu vyake vyote
……….
Kuhani Mkuu alikuwa Haruni.
…………
Yesu alipokuja, alianzisha Agano Jipya na sheria zake mpya. Imeandikwa:
Waebrania 7: 15-17 ametokea KUHANI MWINGINE MITHILI YA MELKIZEDEKI; asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo; maana ameshuhudiwa kwamba, WEWE U KUHANI MILELE KWA MFANO WA MELKIZEDEKI.
…………..
Yesu ni kuhani kwa mfano wa Melkizedeki na sio kwa mfano wa Lawi.
…………
Hivi sasa hakuna Kuhani Mkuu zaidi ya Yesu. ---- WEWE U KUHANI MILELE KWA MFANO WA MELKIZEDEKI.
…………….
Watumishi wote wa Mungu leo ni makuhani CHINI YA KUHANI MKUU YESU. --- 1 Pt 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu
……………..
MASWALI
1. Muhamamad alikuwa kuhani?
2. Kama ni ndio, alikuwa chini ya Lawi au chini ya Yesu?
3. Kama sio, uhalali wake ulitoka kwa Mungu gani?
4. Ndugu waisalmu, kuhani wenu ni nani?
…………….
Abiria chunga maisha!!!
Hakuna kama Yesu.
Imeletwa kwenu na Jimmy John
No comments:
Post a Comment