Friday, March 17, 2017

DALILI ZA UWEPO WA MAJINI KATIKA MAISHA YA WATU



Ndugu msomaji,
Hili somo sio la kukutisha bali kukufungua macho na kukufanya ujifahamu kama wewe unafuatiliwa na Majini ambayo ni ndugu za Waislam.
Dalili zifuatazo ni za mtu ambaye ama ana majini au anafuatiliwa na majini:-
Unakuwa unaota ndoto upo ndani ya maji; ama unatembea ndani ya maji, unaingia majini au unatembea juu ya maji. AU unaota unaogelea, basi elewa wewe upo kwenye msako wa Majini au teyari yamesha kuteka.
Kuota unalishwa nyama. Kula nyama ndotoni ni moja ya dalili kuwa unafuatiliwa na majini au teyari yamesha kuteka.
Ukiota unafanya tendo la ndoa na mtu ambaye labda unamfahamu au aumfahamu. Basi elewa kuwa teyari umesha shikwa na au olewa na Jini "Spiritual wife or husband". Unahitaji deliverance ya haraka sana.
Kila wakati unajikuta umeona au umeokota pete za dhahabu; mara nyingi majini wanaotaka kukutana kimwili na wanadamu hutegesha mikufu au pete ili kuunganishwa naye. Hii sio lazima iwe kwenye ndoto.
Mara nyingi unapotembea unakuwa unasikia harufu ya udi, ubani au marashi. Si lazima majini hayo yawe ndani yako lakini yanaweza kuwa yanakufuatilia ili kukudhuru.
Wakati wa usiku unasikia vitu vimepigwa kwenye bati au darini bila kujua chanzo na mwisho wake.
Kudondoka chooni ni dalili nyingine ya mtu anayefuatiliwa na majini.
Kumchukia mwenza wako pindi anapo kuwa karibu na wewe.
Basi elewa kuwa wewe una JINI SUBIANI.
Kuto kuona ladha yeyote na mwanamke kushindwa kutoa ute na kumpa maumivu, basi wewe elewa kuwa teyari unaishi na JINI JALWUSH.
Wewe ni Mkristo lakini ukisikia adhana unajisikia kuipenda; na ndio
maana watu wengi wakija kuombewa wanalipuka mapepo yanayopiga adhana.
Kukonda kupita kiasi.
Kupenda kuvaa nguo za nusu uchi.
2 Wathesalonike 2:8, alisema Mtume Paulo alikua amepakwa mafuta na Mungu kutenda mambo makubwa lakini pamoja na hayo shetani aliweza kumzuia kwenda Thesalonike kuifanya kazi ya Bwana. kumbe kupitia majini shetani aweza kutenda kazi ama ndani au nje ya watu ili kufanikisha azma yake ya kutesa maisha ya watu.

MAMLAKA YA KUTOA PEPO UMEPEWA NA YESU

Marko 16:17-18 inasema, "ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina Langu watatoa pepo...." Kila Mkristo anao uwezo wa kuwatoa pepo! Sio swala la kwamba "una nguvu" kiasi gani au jinsi gani upo "kiroho" ; cha muhimu ni kuwa Yesu Amekupa mamlaka Yake; unatembea katika jina Lake.
Shetani hana haki ya kuendesha mambo katika maisha yako, au nyumbani mwako au katika maisha ya wale uwapendao. Tumia mamlaka yako katika Kristo dhidi yake.
JE, NI WAKATI GANI UNAWEZA TOA PEPO
Unaweza kuwatoa pepo siku yoyote, muda wowote na mahala popote, kwa kutumia jina la Yesu tu. Usijadiliane naye; mtoe!
Unaweza ukajiuliza. "Nitajuaje kuwa pepo ametoka ninapomkemea?" Hilo ni rahisi. Yesu Alisema, unapowaambia pepo watoke, hutoka. Neno Lake Linakamilisha hilo. Kazi yako ni kumkemea pepo atoke, na jukumu lake pepo ni kutii.
Ingawa, wakati mwingine pepo hujionesha na kulia kwa sauti pindi wanapomtoka yule mtu unayewatoa kwake. Mfano ni kama tulivyosoma katika mstari wetu wa ufunguzi. Pia tunaona tukio kama hilo katika matendo 8:6-8 pale Filipo alipomuhubiri Kristo kwa watu: "...pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu..."
NINI KINAWEZA TOKEA WAKATI WA KUTO PEPO
Hivyo, katika kutoa pepo, roho waovu huweza kupiga yowe na kelele kwa kuteseka pindi wanapotoka; na kisha badiliko la wazi kwa wale ambao pepo wamewatoka hujionesha kuwa kuna tofauti.
Hata hivyo, haijalishi pepo wamepiga yowe au kelele wakati ulipowakemea; cha muhimu ni kile Yesu Alichokisema,"...kwa jina Langu mtatoa pepo..."( Marko 16:17). Huo ndiyo uhalisia, na unapaswa kuwa ndiyo msingi wa imani yako. Hivyo, unapowakemea pepo, wanakuwa hawana chaguo lolote- zaidi ya kukimbia.
Ndugu msomaji,
Nategemea umesha elewa kuwa, umepewa haki ya kuyatoa MaPepo, na anza kulitoa pepo ambalo linakusumbua, Ndio, unaweza kutoa pepo yako chafu. Biblia inasema kuwa (Marko 16:17-18) = [Ishara hizi zitawafuata Waaminio, watatoa pepo"], umepewa Mamlaka ya kutoa pepo, sio pepo wa mwenzako tu, la hasha, hata pepo ambayo imo ndani yako.
Mamlaka unayo na anza kufanya kazi ya Bwana.
Mungu akubariki sana,
Shalom
Dr. Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu.

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW