Saturday, February 18, 2017

NENO LAKO NI TAA YA MIGUU YANGU


Image may contain: text

UWEZA ULIO KATIKA NENO LA MUNGU

Neno ni nini?
Neno ni matamshi yenye maana yanayotoka kwenye kinywa cha mtu, au kitu !


Kibiblia Neno ni yale mambo yaliyojaza moyo wa mtu , Biblia inasema “Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake , hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoka yaliyo maovu; kwa kuwa mtu hunena yale yaujazayo moyo wake” Luka 6:45 Amplified Bible moyo umeandikwa kama (storehouse)

Neno la Mungu ni nini?
Neno la Mungu ni yale maneno yanayotoka kwa Mungu, na ni makusudio ya somo hili kujifunza uweza ulio katika neno la Mungu ili yamkini tupate kujua msaada tutakao upata kwenye neno hilo! Mungu anaongea sana kupita unavyofikilia lakkini unawezaje kulipokea neno na kulitumia hapo ndo wengi wanaposhindwa.

Uwezo wa NENO kukuongoza katika njia sahihi.

“Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu” Zaburi 119:105,

Neno linatuonyesha tunapoelekea, linatuongoza kutenda kwa usahihi kama vile nchi bila katiba inapotea, ndivyo mtu anayemwamini Yesu kutokuwa na neno la Mungu moyoni mwake! lazima atapotea! Mungu akamwambia Joshua “kitabu hiki cha torati kisitoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku…ndipo utakapoifanikisha njia yako…” Joshua 1:8. Ni kwa kufuata Neno la Mungu ndipo mtu anaweza ifanikisha njia yake!

Shalom,

Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW