Ndugu msomaji,
Je unafahamu kuwa Yesu anakupenda? Ndio nazungumza na wewe unaye soma hii mada, wewe mwenye dini, wewe unae sali kila siku mara tano, ndio, ni wewe unayesema la ilaha illallah muhammadur rasulullah.
…Wewe ni mnyanganyi, mwizi, mwongo, muuaji, usiye kuwa na ukweli? Yesu anakupenda na anataka kukuponya.
…Wewe ni mlozi mkubwa mwenye kutumikia Shetani, tena unawasomea watu albadiri na kutoa laana tulah na dua mbaya kwa jamaa yako, tangu ujana wako unazuru wanadamu wengine, unaua watoto, wanawake hata wanaume, unaharibu mavuno, unatawanya magonjwa toka jamaa kwa ingine, unaua hapa na pale. Unapopita ni woga mtupu na kukimbia mbali sababu ya mapepo mabaya yako. Mara na mara unajiuliza nini ulikuja kufanya hapa duniani, ukitafuta kujua sababu ya mabaya yote unayoyatenda. Unajiuliza namna gani uliweza kufikia hapo. Fahamu neno moja tu, hata unaishi mabaya haya yote : Yesu anakupenda na anataka kukuponya.
Yohana 3: 16-17 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”
Mungu anakupenda sana, anajua jinsi unavyoenenda na amemtuma Mwana wake wa pekee, Yesu afe msalabani kwa ajili ya ukombozi wako. Haupaswi tena kuendelea kuishi dhambini, neema ya wokovu imefunuliwa na yapatikana bure kwa kumkiri na kumwamini Yesu.
Warumi 10: 9-10 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”
Hata wewe Yesu anakupenda sana,
…Wewe ni mkoma, tangu miguu hadi kichwani. Ulipoteza vidole, sikio, pua, ukageuka kilema kwa namna fulani; fahamu jambo hili: Yesu anakupenda na anataka kukuponya.
… Wewe ni msichana unaye mswalia Muhammad, tena swala tano, waonekana kuwa ni mrembo sana na wakati wako wote unavunja jamaa za wengine. Unapotosha rafiki zako za darasa, za shule lako, za ofisi za mtaa wako. Mara nyingine ulitoa mimba, ulitafuta kupatia wengine sumu, ao uligonganisha wapenzi wako: wamoja wafariki ao wangali wagonjwa sana sababu yako, sababu ya unyofu wako, na sura yako nzuri sana. Sasa wajiuliza mengi kuhusu maisha yako: uliweza kutambua mabaya yote uliyotenda na unajiuliza nini Mungu atakayokutendea.
Unapatwa na woga wakati unawaza haya yote sababu unaambiwa yakuwa siku moja Mungu atahukumu matendo ya watu. Unaishi katika uasi, unajua ya kwamba JEHENAMU ndiyo inakungojea na unajifariji ukisema kwamba ni maneno yasiyokuwa na msingi hata unasema : Mungu hayuko!
…Wewe ni kijana unayejiita Ustaadh au Sheikh, wengine wanakuita Maalim, tena Muislam swafi kabisa, ndio wewe uliyetenda mambo sawasawa na yale na mwisho ukafikia kusema hivyo. Unajitia kwa mstari ya wale wasiosadiki kuwa Mungu yuko, ili ujitulize.
Kwa kumaliza, Roho Mtakatifu anakupa ujumbe huu:
“Basisisi,! Tutapona namna gani, tusipochunga wokovu mkubwa namna huu?” (Waebrania 2.3).
“Basisisi,! Tutapona namna gani, tusipochunga wokovu mkubwa namna huu?” (Waebrania 2.3).
Ndugu, rafiki, wajua sasa ya kwamba Mungu anakupenda, wajuwa kuwa Mwana wake Yesu ni tayari kukuponya. Haupatikane tena katika kutokujua. Mungu anataka kukufungua macho kwa maneno haya na anasema:
“Kwa maana Mungu alivyopenda ulimwengu, hata kutoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu akimwamini asipotee, bali apate uzima wa milele” (Yoane 3.16).
Chaguo ni lako: amini na uokolewe ao kutoamini na kuhukumiwa. Ndiyo, katika neema yake kubwa, Mungu anakuonyesha wazi njia ya kupitia. Anasema:
“Nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; kwa hivi chagua uzima ili uwe hai.” (Kumbukumbu la torati 30.19).
Amua leo kumpa Yesu maisha yako upate tumaini jipya la uzima wa milele. Ukimpokea Yesu utapata furaha, amani na uzima wa kweli. Huwezi kuzipata baraka za Mungu kama hauna ushirika naye, na pia huwezi kushinda dhambi bila msaada wa Mungu. Kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako, sali sala hii kwa kumaanisha kutoka moyoni.
“BWANA Yesu, nakuja mbele zako mimi ni mwenye dhambi. Nimetambua makosa yangu na kuwa siwezi peke yangu. Naomba uingie ndani ya moyo wangu, uondoe kiu ya dhambi, unisamehe makosa yangu yote, ufute jina langu kwenye kitabu cha mauti, na uliandike kwenye kitabu cha uzima. Nimeamua kukufuata wewe na kujitoa kwako siku zote za maisha yangu. Nisaidie niweze kutembea nawewe daima.”
Hongera! Sasa umeokoka. Tafuta kanisa linalohubiri kweli ya neno la Mungu uwe mshirika hapo. Jifunze biblia na omba kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Yesu anakupenda.
Katika huduma Yake,
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
No comments:
Post a Comment