Tuesday, January 10, 2017

WATOTO WA MUNGU NI NANI?

Image may contain: 12 people, people standing


Biblia ipo wazi kwamba watu wote ni viumbe wa Mungu (Wakolosai 1:16), na kwamba Mungu anaipenda dunia nzima (Yohana 3:16), lakini ni wale tu ambao wamezaliwa mara ya pili ndio watoto wa Mungu (Yohana 1:12; 11:52; Warumi 8:16, 1 Yohana 3:1-10).
Ninani mwana wa Mungu?
Kuzaliwa kwa kiroho hufanya mtu kuwa mwana wa Mungu. Imeandikwa Yohana 1:12-13 "bali waliompokea aliwapa uwezo wakufanyika watoto wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake walio zaliwa sikwa damu wala si kwa mapenzi ya mwili wala sikwa mapenzi ya mtu bali kwa Mungu."
Mungu amefungua njia yakuwa watoto wake. Imeandikwa 1Yahana 3:1 "Tazameni ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo kwa sababu hii ulimwengu haututambui kwa kuwa aukutambua yeye."
Wakristo wamefanywa kuwa jamaa ya Mungu imeandikwa Warumi 8:16 "Roho mwenywe hushuudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu."
Tazama watoto washanga. imeandikwa Luka 18:16-17 "Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema waasheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao amininawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe."
Katika maandiko, waliopotea kamwe hawajulikani kuwa watoto wa Mungu. Waefeso 2:3 inatuambia kwamba kabla ya sisi kuokolewa sisi tulikuwa "kiasili wana wa hasira" (Waefeso 2:1-3). Warumi 9:8 inasema kwamba "si watoto wa kawaida ambao ni watoto wa Mungu, lakini ni watoto wa ahadi ambao ni kuonekana kama uzao wa Ibrahimu." Badala ya kuzaliwa kama watoto wa Mungu, sisi tumezaliwa katika dhambi, ambayo hutenganisha sisi kutoka kwa Mungu na kutuweka sisi pamoja na Shetani kama adui wa Mungu (Yakobo 4:4, 1 Yohana 3:8). Yesu alisema, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, kwa maana nalitoka kwa Mungu na mimi nimekuja; wal sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma" (Yohana 8:42). Kisha mistari michache baadaye Yohana 8:44, Yesu aliwaambia Mafarisayo kwamba "nanyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda." Ukweli kwamba wale ambao hawajaokoka si watoto wa Mungu pia huonekana katika 1 Yohana 3:10: "Katika hili watot w Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake."
Sisi huwa wana wa Mungu wakati tumeokolewa kwa sababu tumetwaliwa katika familia ya Mungu kwa njia ya uhusiano wetu na Yesu Kristo (Wagalatia 4:5-6, Waefeso 1:5).
Shalom.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW