Thursday, January 12, 2017

TOFAUTI YA WATOTO WA MUNGU NA SHETANI (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: text
Waraka wa 1 Yohana 3:4-10 unasema “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhiirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwuona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa ibilisi; kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.”
DHAMBI NI UASI
1 Yohana 3:4 inasema “ Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi."
Mtu yeyote anayefanya dhambi anaasi zidi ya Mungu. Yaani anamkosea Mungu. Ni kama vile Adamu na mkewe walivyoasi katika bustani, Mungu aliyowaweka, aliwaambia kwamba wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hawakutii kama Neno la Mungu linavyosema kwenye Mwanzo 2:16-17 “Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” Na kwa sababu hiyo dunia nzima wakaingia kwenye uasi wao kama Neno la Mungu linavyotuambia katika Warumi 5:12 “ Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Na Warumi 5:19a inasema “ Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya mwenye dhambi,..” Kwa sababu hiyo mtu yeyote ambaye hajaokoka kwa kumuamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake anaendelea kuwa muasi kwa Mungu. Na yeyote anayeendelea na dhambi yeyote anafanya dhambi na ni muasi. Yeyote asiyefuata Neno la Mungu, ni muasi pia na Yeyote anayeshikilia mafundisho ya dini yake badala ya mafundisho ya Neno la Mungu, naye ni muasi pia, Wapo wale wanaobatiza watoto wachanga na watu ambao hawajatubu dhambi zao, wote hao wanajumuisha kwenye kundi la waasi kama Neno la Mungu linavyosema kwenye Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa la moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
Nitaendelea tena siku nyingine endelea kufuatilia somo hili mpendwa rafiki yangu. Mungu akubariki sana.
JAMBO LA MUHIMU SANA KUFANYA

Kama hujampokea Bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wako nakutia moyo kumpokea. Hizi hapa ni hatua zitakazo kusaidia.
KUBALI kwamba wewe ni mwenye dhambi kwa asili na kwa kukutenda na wewe mwenyewe huna tumaini. Mwambie Mungu binafsi umetenda dhambi katika mawazo yako, maneno na matendo yako. Tubu dhambi zako kwake, moja baada ya nyingine, katika maombi kwa uaminifu. Usiache dhambi yoyote unayoikumbuka. Kwa kweli geuka katika njia za dhambi na kuziacha. Kama uliba, usibe tena, kama ulifanya uzinzi au uasherati, acha. Mungu hatakusamehe kama hauna hamu ya kuacha dhambi, katika sehemu zote za maisha yako, lakini kama utakuwa mwaminifu, atakupa nguvu ya kuacha dhambi.
AMINI kwamba Yesu Kristo, ambaye ni Mungu Mwana , ni njia Pekee, ya Kweli na ya Uzima pekee. Yesu alisema “ Mimi ni njia, Kweli na Uzima. Hakuna ajae kwa Baba lakini kwa mimi”( Yohana 14:6) . Biblia inasema , “Kwa kuwa kuna Mungu mmoja, na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu, mwanadamu Yesu Kristo,ambaye alijotoa sadaka kwa wote “( 1Timotheo 2:5-6). “Na hakuna wokovu kwa mwingine awaye yoyote,(isipokuwa kutoka kwa Yesu Kristo) kwa kuwa hakuna jina jingine chini ya mbingu kati ya wanadamu ambalo linaweza kuokoa (Matendo 4:12).” “lakini kwa wote waliompokea, walioliamini jina lake, aliwapa uwezo wa kuwa Watoto wa Mungu..”( Yohana 1:12 ), LAKINI
FIKIRIA gharama ya kumfuata . Yesu alisema kwamba wote watakaomfuata ni lazima wajikane wenyewe, na hii inajumuisha pesa, jamii, na mipango mingine. Na pia alitaka wanaomfuata kuchukua misalaba yao kumfuata. Je umejiandaa kuacha mipango yako binafsi kilasiku kwa ajili ya ile ya Kristo? Je umejiandaa kuteseka naye na kufa kwa ajili yake kama itahitajika? Yesu hana chakufanya na watu wenye mioyo iliyo nusu. Anahitaji mtu kujitoa kikamilifu. Atawapokea tu na kuwasamehe wale wote walioandaliwa kumfuata, Kwa GHARAMA YOYOTE ile. Fikiria kuhusu hilo na hesabu gharama. Kama umejiandaa kumfuata yeye njoo kuna kitu cha KUFANYA
MKARIBISHE Yesu kuja kwenye moyo wako na maisha yako. Anasema “ Tazama nasimama katika mlango na kugonga. Kama yoyote atasikia sauti yangu na kufungua mlango (wa moyo wake na maisha yake ), nitaingia kwake na kula pamoja naye, na yeye pamoja na mimi.” (ufunuo 3:20 ). Kwa nini usisali kama ifuatavyo kama Roho Mtakatifu anavyokuongoza:
“Bwana Yesu, mimi ni mwenye dhambi niliyepotea ambaye nimetenda dhambi katika mawazo, maneno na matendo. Nisamehe dhambi zangu zote na unisafishe kwa damu yako. Nipokee mimi, Ee Mwokozi na unifanye mimi kuwa mtoto wa Mungu. Njoo katika moyo na maisha yangu sasa na unipe mimi uzima wa milele sasa. Na ahidi nitakufuata wewe kwa gharama yoyote ile, na muomba Roho Mtakatifu aniongoze katika maisha haya mapya. Amen”
Kama umesali hiyo sala hapo juu kwa uaminifu, Bwana Yesu amekujibu mara moja, na amekufanya wewe kuwa mtoto wa Mungu.
Tafadhali niandikie na nitakuombea na kukusaidia kuendelea mbele na Yesu Kristo.
***
REAGAN FRANCIS,
Simu: 0718730627 au 0783499064
P.O Box : 42376, DAR-ES-SALAAM,
E-mail : francisreagan88@gmail.com

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW