Monday, January 16, 2017

ROHO, NAFSI NA MWILI

Image may contain: cloud, sky, text and outdoor
Ndugu msomaji,
Je, mwanadamu ni nani?
Kwa kifupi ninaweza kusema kuwa Mwanadamu ni Roho, ina Nafsi na inakaa ndani ya Mwili.
Ukisoma 1 Wathesalonike 5:23 Inatusaidia Kuona maeneo yote matatu ya mwanadam/mtu;
"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU Mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo"
Hapa unaona Nafsi, Roho na Mwili vimetajwa kwenye hiyo aya.
ROHO NI NINI?
Roho ambayo inahusisha mambo ya Mungu.
Ni ile sehemu ya mtu yenye ufahamu wa Mungu, ambayo hufanywa hai na hutiwa nguvu na Roho wa Mungu wakati wa Wokovu. Kabla ya mtu Kuokoka, sehemu hii, haifanyi kazi kwa utimilifu kabisa kwa sababu ya dhambi. Dhambi huifanya kuondolewa nguvu ya kutenda kazi sawa sawa, kwa Amani na Roho ya Mungu. Lakini kupitia Ubatizo wa Roho Mtakatifu, mwanadamu hupokea nguvu ya kiroho, inayomwezesha kuishi maisha ya Kristo.
Roho inahusika na:-
i) Maombi na Ibada na Mungu,
ii) Ushirika na Mungu,
iii) Mapokezi ya karama za Roho,
iv) Vita vya kiroho,
v) Kuunda Mawazo na Ndoto,
vi) Dhamira, Kupambanua,
vii) Udadisi, Kuuliza,
viii) Ufahamu, Kutafsiri,
ix) Shuhuda kwa Wanadamu
NAFSI NI NINI?

Katika Biblia, neno “nafsi” limetafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania neʹphesh na neno la Kigiriki psy·kheʹ. Katika Kiebrania neno hilo kihalisi linamaanisha “kiumbe kinachopumua,” na katika Kigiriki linamaanisha “kiumbe kilicho hai.”
Nafsi inahusika na mambo ya mtu.
Ni ile sehemu ambayo ina ufahamu wamtu mwenyewe au kiini cha ubinafsi wa mtu. Kazi yake ni:-
i) Kufikiri – Kutafakari, kuona
ii) Hisia – Kujisikia kuwa na tamaa na Upendo
iii) Utashi – Nia, Kuamua
MWILI NI NINI?
Mwili unahusika na mambo ya Ulimwengu.
Ni ile sehemu ya mwanadamu ambayo inafahamu na kukubaliana na ulimwengu wa nje. Inafanya yafuatayo:-
i) Utambuzi wa Ulimwengu, - yaani ile hali ya mwili kupokea habari kutoka Ulimwenguni kwa njia ya Ufahamu.
ii) Urejeshi – yaani ile hali ya Mwitikio wa kutenda kutokana na kutendewa kitu, kupitia utaratibu wa Maneno na Matendo.
iii) Udhihirisho – yaani ile hali ya Mwili ya kutoa habari za Ulimwengu kwa Mawazo, Kujisikia na Maamuzi ya Nafsi.''
Hivyo basi, Mtu ni Roho.
1) Mungu alimuumba mwanadamu kwanza kama roho ( Mwanzo 1:26) hapo bila mwili ndiyo maana Biblia inasema Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake kwa sababu Mungu ni Roho.
Mtu ambaye Mwanzo 1:26 inamuongelea, Biblia yenyewe inathibisha kuwa ni roho lakini yenye mwili wa rohoni (1 Korintho 15:44) ikiwa kuna mwili wa asili basi kuna mwili wa rohoni pia.
2) Mungu aliumba roho ya Mwanadamu kwanza ndio akaumba mwili wa nyama na nafsi baadae.
(Mwnzo 2:7) Mungu akauumba mwili wa Adamu kwa udongo akaichukua ile roho (kumbuka ina mwili wa kiroho) akaiweka/ingiza katika mwili kwa kuipulizia ndani ya ule udongo alio uumba, na mtu akawa nafsi hai.
Hivyo basi;
Mwanadamu amegawnyika mara tatu
1) Roho yenye ufahamu wa mambo ya Mungu. Chakula cha Roho ni neno la Mungu.
2) Nafsi ni shemu yenye ufahamu ambapo vitu vya kujifunza au elimu au kumbukumbu vinakaa. Roho huitia nafsi nguvu au kuwa mahiri kwenye eneo fulani ambalo rohoni umebarikiwa ili hicho kitu kithiirike kwenye ulimwengu wa mwili.
3) Mwili ni sehemu ya mwanadamu inayo onekana na imebeba roho na nafsi.
Bonus question.
KUFA NI NINI?
Kufa ni kitendo cha roho kuachana na mwili, kama huyo mtu(roho) alipokuwa ndani ya mwili aliishi maisha matakatifu roho yake itakwenda kwa Mungu na kama aliishi maisha yasiyompendeza Mungu huyo mtu(roho) atakwenda kuzimu.
Hivyo basi itunze sana Roho yako maana wewe ni Roho una nafsi na unaishi kwenye mwili.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo

2 comments:

Moses Mgimwa said...

Ubarikiwe saana

Unknown said...

Barikiwa sana mtumishi wa Mungu max nimejifunza kitu kizuri.

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW