Tuesday, January 10, 2017

"MUISLAMU ZINDUKA KUTOKA USINGIZINI ILI UJUE KUWA MKRISTO SIYO KAFIRI"


Najua unaweza kustaajabu ni vipi muislamu wewe uzinduke ili hali unajiona kuwa u macho haupo kwenye Usingizi? ninaposema kuwa unajiona u macho ni katika imani uliyo nayo juu ya Mkristo kuwa ni kafiri, hivi ndivyo unavyoamini kwa sababu uliminishwa hivyo, ukaamini hivyo, kwa sababu tu Quran inasema! 👇
وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
التوبة (30) At-Tawba
Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!
Muislamu ukisoma aya hii moja kwa moja unaamini kuwa Wakristo ni Makafiri kwa kusema kuwa Masihi Yesu ni Mwana wa Mungu! unaamini kabisa kuwa hayo maneno ya kusema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, tunayosema sisi kwa vinywa vyetu yaani sisi ndo tumebuni, hivyo unatuona sisi ni Makafiri! tena unafurahia ujio wa Quran kuwa umekuja kwa ajili ya 👇
وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا
الكهف (4) Al-Kahf
Na kiwaonye wanao nena: Mwenyewe Mungu ana mwana.
مَّا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا
الكهف (5) Al-Kahf
Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu.
Nawe unaamini fika kuwa Quran imekuja kwa ajili ya kuwaonya Wakristo kwa sababu wanasema kwa vinywa vyao kuwa Mwenyezi Mungu ana mwana, nawe bila kuzinduka uangalie kama kuna usahihi wa jambo hilo unakurupuka na kuanza kusema kuwa, Wakristo ni Makafiri, LEO naomba nikuzindue ili kama unapenda kwenda kwenye UFALME WA MUNGU, basi uungane nami leo.
JE! NI KWELI KWAMBA WAKRISTO WANASEMA KWA VINYWA VYAO KUWA YESU NI MWANA WA MUNGU?
Hili 👆ni Swali la msingi sana mtu kujiuliza, kabla ya kuamini kuwa Wakristo wanasema kwa vinywa vyao na kuwaona ni makafiri (wenye kwenda kinyume na Mungu) kabla Wakristo hawajapatikana, na Yesu ambaye ndiye chimbuko la Wakristo hajazaliwa, Malaika alisema. 👇
Luka 1:30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Malaika ndiye aliyeanza kutangaza kuwa Yesu akizaliwa huyo ataitwa Mwana wa Mungu, na siyo Wakristo (wafuasi wa Kristo) kama ilivyosema Quran na hata Mungu mwenyewe alithibitisha kuwa Yesu kweli ni Mwana wake,
Mathayo 17:1 Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani;
2 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.
4 Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
5 Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
6 Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
Mungu anathibitisha mbele ya wanafunzi wa Yesu kuwa Yesu ni Mwanae, Muislamu Jiulize, Je! Malaika na Mungu hao ni Wakristo? Je! Mungu anaweza kuwa kafiri yeye na malaika wake? Pia Isitoshe Yesu mwenyewe alithibitisha kuwa yeye ni Mwana wa Mungu,
Yohana 9:35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?
37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.
38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.
Hivi kweli Yesu anaweza kuwa Kafiri? maana yeye ndiye anawadhihirishia Wakristo kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, na Mkristo aitwae Petro alipotambua kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na kusema, Yesu alisema kuwa hakusema kwa akili zake. 👇
Mathayo 16:13 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?
14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
Ikiwa tu kusema kuwa Yesu ni mwana wa Mungu ni ufunuo kutoka kwa Mungu ni vipi muislamu wewe uamini kuwa Wakristo ni Makafiri kwa kusema kuwa Yesu ni mwana wa Mungu? Muhammadi alitumia njia hiyo ili kuwafanya muwe wagumu kuipokea Injili, mkiamini kuwa Ukiwa Mkristo ukasema Yesu ni Mwana wa Mungu basi wewe unakuwa kafiri, kitu ambacho siyo kweli, bali unakuwa kafiri kwa kuendelea kubaki kwenye Uislamu kwa ushahidi wa maandiko haya 👇
Nehemia 5:8 Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lo lote.
9 Tena nalisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu?
Biblia imeweka wazi kabisa kuwa, Kabla hawajapatikana Wakristo, makafiri walikuwepo, na makafiri hao ni maadui wa Wayahudi, yeyote ambaye alijitangaza kuwa yeye ni adui wa Wayahudi huyo alihesabika kuwa ni Kafiri. Walipokuja kupatikana Wakristo walio nje na Wayahudi wao na Wayahudi waliompokea Yesu wakafanyika wamoja. 👇
Wagalatia 3:26 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Wakristo wasiokuwa Wayahudi hawakufanyika Makafiri kwa sababu wao hawakuwa na uadui na Wayahudi, lakini alivyokuja Muhammad akaweka wazi kuwa, Wayahudi ni maadui wa Waislamu 👇
( لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ )
المائدة (82) Al-Maaida
Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa Waislamu ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi.
Waislamu mnaambiwa kuwa walio maadui zaidi kwenu ni mayahudi (Wayahudi) na Nehemia 5:8-9 Imesema kuwa Maadui wa Wayahudi ni Makafiri, Swali la kujiuliza ninyi kufanya kwenu uadui na Wayahudi mtakuwa nani? Na Mungu anajua fika kuwa, Kuna Wayahudi na kuna Makafiri ambao ni maadui zao!
Ezekiel 34:28 Hawatakuwa mateka ya makafiri tena, wala mnyama wa nchi hatawala; bali watakaa salama salimini, wala hapana mtu atakayewatia hofu.
29 Nami nitawainulia miche iwe sifa njema, wala hawataangamizwa kwa njaa katika nchi yao tena, wala hawatachukua tena aibu ya makafiri.
30 Nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, Mungu wao, ni pamoja nao, na ya kuwa wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asema BWANA MUNGU.
na Mungu alivyosema hayo baada ya kusikia kilio cha watu wake Wayahudi dhidi ya Makafiri adui zao, Pale walipo mlilia MUNGU aweze kuwakomboa na kurejesha mali zao kutoka kwa Makafiri.
Maombolezo 5:1 Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.
2 Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri.
3 Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane.
ikiwa Mungu wa kweli, kabla hajakuwepo Quran, anajua fika kuwa Maadui wa Wayahudi ni makafiri, na ninyi waislamu mnazuiliwa kufanya urafiki na Wayahudi, 👇
( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ )
المائدة (51) Al-Maaida
Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
Hamjazinduka tu na kujua kuwa mmeingizwa kwenye Ukafiri kwa kuweka uadui na Wayahudi? Kama mlikuwa hamjazinduka basi Leo zindukeni, huwi kafiri kwa kusema Yesu ni Mwana wa Mungu, wala ukiamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, huwi kafiri kama Quran isemavyo. 👇
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَٰنُ وَلَدًا
مريم (88) Maryam
(Waliokufuru) husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana!
Bali utapata uzima wa milele kwa kuamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu. 👇
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Hivyo ukimwamini Mwana wa Mungu, jua kwamba uhukumiwi, usipoamini itahukumiwa kwa sababu hukuliamini jina pekee la mwana wa Mungu, na Yesu akazidi kusisitiza kuwa, 👇
Yohana 3:36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Muhammadi amewataka ninyi mtembee kwenye ghadhabu ya Mungu, kwa sababu anajua fika kuwa yeye mwenyewe hatima yake juu ya ufalme wa Mungu hajui itakuwaje!
( قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ )
الأحقاف (9) Al-Ahqaf
Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.
Kwa hivyo anataka muamini kwamba kusema Yesu ni Mwana wa Mungu ni kufuru, ili mwende katika moto wa milele, ZINDUKENI leo mtambue kuwa mtu hawi kafiri kwa kusema Yesu ni Mwana wa Mungu. Ingekuwa ni kweli ni Ukafiri kusema hivyo basi haya aliyosema Muhammadi 👇
( لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا )
مريم (89) Maryam
Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
( تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا )
مريم (90) Maryam
Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo (la kuwa Mwenyezi Mungu ana mwana), na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.
Jiulize ni zaidi ya miaka 1439 imepita ulishawahi kuona dalili za mbingu na aridhi kutatuka, na kupasuka na milima kuanguka vipandevipande kwa kusema Yesu ni mwana wa Mungu? Basi ndo ujue kuwa siyo Ukafiri kusema Yesu ni mwana wa Mungu.
SOMO HILI NIMELITOA KWA ABEL SULEIMAN SHILIWA

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW