Wakati Yesu akizungumza na Nikodemo, alisema, Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?” “Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu, “Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili…” (Yohana 3:3-7).
Msemo “kuzaliwa mara ya pili” unamaanisha “zaliwa toka juu” Nikodemo alikuwa na uhitaji wa kweli. Alihitaji mabadiliko ya moyo wake... Mabadiliko ya kirohoUzao mpya, kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo au hatua ya Kiungu ambapo uzima wa milele hupewa mtu yule aaminiye (2Wakorintho 5:17; Tito 3:5; 1Petro 1:3; 1Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1-4, 18). Yohana1:12, 13 inasema ya kuwa”kuzaliwa mara ya pili” pia ina maana “kufanyika mtoto wa Mungu”kwa imani katika jina la Yesu Kristo.
Kuzaliwa mara ya pili ina maana kufa kwa matendo ya mwili ya kale. Imeandikwa, Warumi 7:4 "Kadhalika ndungu zangu ninyi pia mmeifia torati kwa njia ya mwili wa Kristo mpate kuwa mali ya mwingine yeye aliyefufuka katika wafu kusudi tuzalie Mungu matunda."
Swali hasa ni kuwa, “kwa nini mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili?” Mtume Paulo katika Waefeso 2:1 asema, “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi …” Kwa Warumi katika Warumi3:23, Mtume aliandika, ”kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. “Kwahivyo mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili ili asamehewe dhambi zake na awe na uhusiano na Mungu.
Je, hii hutokea vipi? Waefeso2:8, 9 yasema, kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu.” Mtu anapo “okolewa”, basi yeye amezaliwa mara ya pili, akijazwa upya kiroho, na sasa amefanyika kuwa mwana wa Mungu kwa haki ya uzao mpya. Kwa kumwamini Kristo Yesu, yeye aliye adhibiwa kwa ajili ya dhambi alipokufa msalabani, ndiyo maana ya “kuzaliwa mara ya pili” kiroho. “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya…” (2Wakorintho 5:17 a).
Kama bado hujaweza kumwamini Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, je utakuwa na utayari wa kupokea Roho mtakatifu wakati akizungumza na moyo wako? Unahitaji kuzaliwa mara ya pili. Je, utaomba maombi ya kutubu na ufanyike kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo hivi leo? “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13).
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment