Tuesday, January 10, 2017

JE, TAIFA LA ISRAELI NI LA KIBIBLIA?

Image may contain: text
Je, Unabii wa Biblia Unasema Chochote Kuhusu Kuanzishwa kwa Taifa la Israeli la Kisasa?
LEO ulimwengu unatazama Mashariki ya Kati kwa wasiwasi. Mashambulizi ya roketi, mapigano kati ya makundi yenye silaha, na mashambulizi ya mabomu yanayotekelezwa na magaidi, ni mambo yanayotokea mara nyingi. Zaidi ya hayo, kuna uwezekano wa kutumiwa kwa silaha za nyuklia. Si ajabu kwamba watu kila mahali wana wasiwasi!
Ulimwengu pia ulitazama Mashariki ya Kati kwa wasiwasi mnamo Mei 1948. Wakati huo, miaka 62 iliyopita, mamlaka ya Uingereza ya kusimamia maeneo ambayo wakati huo yaliitwa Palestina ilikuwa inakaribia kuisha, na vita vilikuwa karibu kuanza. Mwaka uliotangulia, Umoja wa Mataifa ulikuwa umetoa kibali cha kuanzishwa kwa Taifa huru la Wayahudi katika sehemu fulani ya maeneo hayo yaliyosimamiwa na Uingereza. Mataifa jirani ya Waarabu yalikuwa yameapa kufanya chochote kile ili kuzuia kuanzishwa kwa taifa hilo. “Mpaka wetu na taifa hilo utakuwa moto na damu,” ukaonya Ushirika wa Nchi za Kiarabu.
Ilikuwa Ijumaa saa 10:00 alasiri, Mei 14, 1948, na baada ya saa chache tu, mamlaka ya Uingereza ya kusimamia Palestina ingefikia mwisho. Kwenye Jumba la Makumbusho la Tel Aviv, kikundi cha watazamaji 350 waliokuwa wamefika baada ya kualikwa kisiri, walingoja kwa hamu kutangazwa rasmi kwa taifa la kisasa la Israeli. Kulikuwa na ulinzi mkali ili kuhakikisha kwamba maadui wa Taifa hilo jipya hawavurugi tukio hilo.
David Ben-Gurion, kiongozi wa Baraza la Taifa la Israeli, alisoma tangazo la kuundwa kwa Taifa la Israeli (The Declaration of the Establishment of the State of Israel). Tangazo hilo lilisema hivi kwa sehemu: “Sisi, washiriki wa Baraza la Watu, wawakilishi wa Jumuiya ya Nchi ya Israeli . . . kwa msingi wa haki yetu ya kiasili na ya kihistoria na kwa msingi wa Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tunatangaza kuanzishwa kwa Taifa la Wayahudi katika nchi ya Israeli, ambalo litaitwa Taifa la Israeli.”
Je, Tukio Hilo Ni Utimizo wa Unabii wa Biblia?
Waprotestanti fulani wa makanisa ya Kiinjilisti wanaamini kwamba kuanzishwa kwa Taifa la Israeli la kisasa kulitimiza unabii wa Biblia. Kwa mfano, katika kitabu fulani (Jerusalem Countdown), kasisi John Hagee anasema hivi: “Tukio hilo muhimu liliandikwa na nabii Isaya, akisema, ‘Nchi itazaliwa katika siku moja.’ (Ona Isaya 66:8.) . . . Huo ulikuwa utimizo mkubwa zaidi wa unabii katika karne ya ishirini. Ulikuwa uthibitisho ulio wazi kwa wanadamu wote kwamba Mungu wa Israeli yuko hai.”
Je, maneno hayo ni ya kweli? Je, andiko la Isaya 66:8 linatabiri kuanzishwa kwa Taifa la Israeli la kisasa? Je, Mei 14, 1948, ‘ilikuwa tarehe ambayo utimizo mkubwa zaidi wa unabii ulitokea katika karne ya ishirini’?
Unabii wa Isaya unasema: “Ni nani amesikia jambo kama hili? Ni nani ameona mambo kama haya? Je, nchi itazaliwa kwa uchungu katika siku moja? Au, je, taifa litazaliwa wakati uleule mmoja? Kwa maana Sayuni ameshikwa na uchungu wa kuzaa naye vilevile amezaa wanawe.” (Isaya 66:8) Mstari huo unatabiri waziwazi kuzaliwa ghafula kwa taifa zima, kana kwamba katika siku moja. Lakini ni nani angesababisha kuzaliwa huko? Mstari unaofuata unatoa dokezo hili: “‘Nami, je, nitasababisha kupasuka wala nisisababishe kuzaliwa?’ asema Yehova. ‘Au, je, mimi ninasababisha kuzaliwa na kwa kweli ninasababisha kufunga uzazi?’ Mungu wako amesema.” Yehova Mungu anaonyesha waziwazi kwamba yeye ndiye angefanya taifa hilo lizaliwe kwa njia hiyo ya ajabu.
Shalom.
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW