Mungu aweza kufanya mambo yasiyowekana. Imeandikwa katika Luka 18:27 "Akasema yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu." Tume ahidiwa moyo mpya na maisha mapya Imeandikwa Ezekieli 36:26 "Mimi nitawapa moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama." Ametuahidi kutusamehe dhambi zetu. Imeandikwa katika 1Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment