Friday, December 2, 2016

Nilipokuwa Nje ya Mwili Wangu Nilimwona Mungu, na Wafu Walio Hai!




Huu ni ushuhuda wa mtumishi wa Mungu, Dr. Roger Mills, ambaye anaishi North Carolina kule Marekani. Hii ni sehemu tu ya ushuhuda huo ambao ameuandika kwenye kitabu. Lakini nimeona niulete viyo hivyo katika ufupi wake, maana naamini kuwa kuna mambo ya muhimu mengi ya kujifunza katika sehemu hii kwa ajili ya uzima wetu wa milele katika Kristo Yesu.
Tafadhali karibu uendelee kupokea kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kile ambacho alimfunulia mtumishi wake kwa ajili yangu na yako.
……………………………..
Jinsi Kitabu Hiki Kilivyo:
Mungu aliniambia niwaonye wacha Mungu na wasio wacha Mungu juu ya hatari ya giza la nje la kuzimu.
kwa wale wote watakaosoma kitabu hiki, ni shauku yangu kuelezea mambo ya kweli yaliyo kwenye kitabu hili kinachoitwa “Nilipokuwa Nje Ya Mwili Wangu, Nilimwona Mungu Na Wafu Walio Hai.”
[Maelezo ya blogger: wafu walio hai hapa anamaanisha watu waliokufa duniani lakini wako mbinguni, yaani watakatifu; au wako kuzimu]
Oktoba 5, 1998, Mungu Mwenyezi alinitokea katika umbo la mwanadamu na kuniambia, “Nimekuja kuzungumza na wewe kuhusiana na Giza la Nje la Kuzimu (Outer Darkness of Hell), na ninataka wewe nawe ukaongee na wengine juu ya Giza la Nje la Kuzimu.” Aliniambia kuwa angejidhihirisha kwangu. Mungu Mwenyezi aliniambia kuwa angeniruhusu kumwona kama ilivyokuwa kwa Petro, Yakobo na Yohana walivyomwona saa chache kabla ya kusulubiwa, na siku kadhaa baada ya kufufuka kwake. Nilipomwona, sikuanguka chini kama ambavyo baadhi ya wahubiri wanasema ningetakiwa kufanya. Na hata mitume walipomwona saa chache kabla ya kusulubiwa , au siku kadhaa baada ya kufufuka nao hawakufanya hivyo. Yesu aliwatokea mitume: (Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:31; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8).
Nilimwambia Mungu Mwenyezi, “Watu hawataniamini nitakapowaambia kuwa nimekuona.” Bwana akaniambia, “Watakuwapo watu, baadhi yao wakiwa wahubiri, ambao watapinga ujumbe huu. Baadhi wataamini na wengine hawataamini, lakini kwa wale ambao hawataamini, waambie kuwa nimesema kwamba imeandikwa kwenye Neno langu Takatifu ‘Nitajidhihirisha kwa wale wanaonipenda.’”
“Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake” (Yoh 14:21).

Ushuhuda huu usichukuliwe kuwa unachukua nafasi ya Biblia Takatifu, na wala si kusudi langu kupunguza kutoka kwenye tafsiri zilizozoeleka za maandiko matakatifu, japokuwa kitabu hiki kina baadhi ya maandiko. Kutokana na ukweli huu, namtahadharisha msomaji asiruhusu rejea za kwenye Biblia kuwa kama sheria (legalistic), bali kuzipokea kama kweli kuu za Mungu Mwenyezi, ambazo Kanisa lote linatakiwa kuzifuata. Kilichomo ndani ya kitabu hiki si matokeo ya ndoto au maono. Badala yake ni rekodi kabisa ya Uzoefu wangu halisi wa kuwa nje ya mwili pamoja na Mungu Mwenyezi na wafu walio hai, kwenye Giza la Nje. Kitabu hiki kina kweli za kiroho kama ambavyo Mwenyezi Mungu alinifunulia wakati nilipokuwa nimekufa, nikiwa nje ya mwili wangu (Oktoba 5, 1998). Dr. R. Mills
Tafadhali kumbuka:
Hii si habari yote kuhusiana na uzoefu wangu wa kuwa nje ya mwili na kuwa kwenye Giza la Nje. Baadhi ya mambo nimeyaacha kwa sababu yanatisha sana. Ulikuwa ni uamuzi wa busara kuyaacha, maana, kama ningeyaweka yangeleta uchungu mkubwa sana na fedheha nyingi kwa ndugu za watu niliowaona kule ambao bado wako hai; ambao ninawataja kwenye kitabu hiki na ambao nilizungumza nao kule kwenye Giza la Nje la Kuzimu.
Nimegawa vitabu hivi kwa watu wengi walio magerezani. Haijawahi kuwa nia yangu kuandika vitabu kwa ajili ya kuuza na kupata faida. Nia yangu ya kuuza kitabu hiki ni ili niweze kuokoa baadhi ya roho, na fedha zozote zinazopatikana kutokana na mauzo zinarudishwa kwenye gharama za uzalishaji, kama vile uhariri, uchapaji, na usambazaji wa kitabu hiki. Kitabu hiki kimechapishwa kwa lugha zingine na gharama zimetumika katika kutafsiri. Pia, mapato yoyote yanayopatikana, yanatumika kugharamia safari zinazoweza kutokea kwa ajili ya mihadhara inayohusiana na kitabu hiki. Kwa kifupi ni kuwa, makusudi kabisa ya kitabu hiki si kujipatia mapato binafsi bali kuzifikia roho zilizopotea kwa gharama yoyote ile.
“Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA wa majeshi.” (Isaya 45:13).
Ujumbe wa Kinabii kwa Roger Kutoka kwa Bwana Mungu
Mungu Mwenyezi alizungumza nami siku ya Jumanne, Agosti 12, 1992, saa 4:20 asubuhi na akanipatia ujumbe. Hivi ndivyo alivyosema:
“NIMEKUJA KUZUNGUMZA NAWE KUHUSIANA NA KURUDI KWANGU. NITAKUPATIA ISHARA KUHUSIANA NA KURUDI KWANGU. SIKU YA SABATO, UWE MTAKATIFU SIKU YA SABATO, MAANA KILA SIKU INATAKIWA IWE SABATO KWAKO. UTAANDIKA KITABU; UTAKUWA NA KITABU KUHUSIANA NA WAKATI WA UNYAKUO NA WAKATI KITABU KITAKAPOKUWA KINASAMBAA, UNYAKUO UTAKUWA KARIBU. UNYAKUO UTAKUJA NAMI NITALIPELEKA KANISA NYUMBANI … INJILI ITAHUBIRIWA KWA MATAIFA YOTE. KISHA ULE MWISHO UTAKUJA.”
Tafsiri ya Ujumbe:
Kuhusiana na kurudi kwa Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo, acha niharakishe kusema kwamba mimi si mpangaji wa tarehe yenyewe. Ninaamini kabisa kwamba hakuna ajuaye siku wala saa ya Bwana Mungu – Yesu kurudi kuchukua Kanisa lake, japokuwa Yesu alisema katika kitabu cha Mathayo kwamba tutajua wakati utakapokaribia.
“…nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.” (Mt 24:33).
Ni kwa nia njema tu ninataja maneno hayo ambayo Bwana Mungu – Yesu aliyasema wazi kwangu kuhusiana na kitabu hiki, na kwamba kitabu kilichoandikwa kitakuwa ni ishara yangu binafsi kutoka kwake, ambayo itaonyesha kwamba kurudi kwake ku karibu. Ni karibu kiasi gani? Mimi sijui. Labda alimaanisha ni miaka mingi baadaye, lakini aliniambia kuwa itakuwa ni wakati kitabu changu kikisambaa; na binafsi nina mpango wa kukichapisha kitabu hiki wakati wote nitakapokuwa hai. Ni Mungu pekee ndiye ajuaye muda halisi wa kurudi kwake. Nikutahadharishe tu kwamba unatakiwa kuwa tayari wakati wote kwa ajili ya kurudi kwa Yesu.
“Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yu aja.” (Mt 24:44).
“Basi kesheni, kwa kuwa hamwijui siku wala saa.” (Mt 25:13).
Utangulizi
Uwezekano wa Mtakatifu Paulo Kuwa Alipitia Uzoefu wa Kuwa Nje ya Mwili
“Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono ya mafunuo ya Bwana. Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na mine, (kwamba alikuwa katika mwili, sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo; (kwamba alikuwa katika mwili, sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayatamke.” – MTUME PAULO (2 Kor 12:1-4).
Salamu takatifu kwenu nyote mnaosoma kitabu hiki. Mimi ni mtu wa kwenye televisheni. Wengi wenu mnanifahamu kupitia kwenye vipindi vya televisheni. Ninaendesha kipindi cha televisheni kutoka kwenye kituo changu cha TV kilichoko kwenye jiji la Detroit, Michigan. Kwa baadhi, ninajulikana kama Nabii wa Mungu, na kwa wengine, mimi ni Mchungaji. Napenda mfahamu jambo hili kuhusiana nami – kwamba nilikuwa mwenye dhambi, nikaokolewa na sasa namtumikia Mungu kadiri ya uwezo wangu, kwa moyo safi na kwa moyo wote.
Siku ya Jumanne, Agosti 12, 1992, saa 4:30 asubuhi, Bwana Mungu alinitokea na akaongea nami kwa sauti ya wazi kabisa na akaniambia kwamba ningeandika kitabu hiki. Sikujua kuwa ingechukua miaka kadhaa ya maandalizi na kukusanya taarifa zote za kibiblia ili kuandika muswada wake. Ilinichukua mwaka mzima kuyaweka mambo mbalimbali kwenye karatasi. Uandishi wa muswada ulikamilika mwaka 2000. Sikuwa na shauku hata kidogo ya kuandika kitabu. Kusema kweli, Mungu alimtumia mtu mwingine kuniambia kwamba niandike, ili kunitia moyo kufanya hivyo. Mtu mmojawapo ni dada yangu wa thamani na mpendwa katika Kristo, Mary K. Baxter, ambaye ni mwandishi kitabu maarufu sana kiitwacho, “A Divine Revelation of Hell” [Ufunuo wa Kimungu Juu ya Kuzimu].
Bwana Mungu aliniandaa kuandika kitabu hiki tangu wakati nilipokuwa tu tineja. Mwaka 1980, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuiona Kuzimu. Wakati huo, Mungu Mwenyezi alichukua roho yangu nje ya mwili na kuniweka kwenye shimo la Kuzimu kwa dakika mbili.
Siku moja wakati nikifanya mahojiano kwenye kipindi changu cha televisheni na mgeni wangu, rafiki yangu, mshindi wa tuzo ya Grammy, Usher Raymond, nilimuuliza swali hili: “Kama ungekuwa na kipindi chako mwenyewe cha televisheni na ukawa na uwezo wa kufanya mahojiano na Mungu, je, ungemuuliza nini? Jibu la Usher lilikuwa, “Je, nitakwenda Mbinguni?”
Katika siku za hivi karibuni nilipata fursa ya kuwa na watu wawili wa thamani na wacha Mungu wakubwa duniani. Naongelea juu ya wazazi wangu wa kiroho, wanaojulikana kimataifa, Dr. Jack na Dr. Rexella Van Impe. Wakati tukiwa tumezama kwenye mazungumzo kuhusiana na uzoefu wangu juu ya Kifo changu na kuwa nje ya mwili, Dr. Rexella alinifahamisha kuwa na yeye naye aliwahi kupitia uzoefu wa kufa - kuwa nje ya mwili. Dr. Jack na Dr. Rexella Van Impe wanaongelea uzoefu huo kupitia kitabu chao kiitwacho: “Heaven: An Out-Of-Body Adventure.”
Mengi yalishaongelewa kuhusiana na watu kuwa nje ya mwili, na watu wengi walishasema kuwa wamewahi kupitia uzoefu huo. Kura ilishawahi kupigwa kwenye mapema miaka ya 1980. Ilionekana kwamba Wamarekani wengi wanaamini juu ya kuwapo kwa maisha baada ya haya. Cha kushangaza ni kuwa, 71% ya wale walioulizwa walikiri kuwa wanaamini juu ya kuwapo kwa Mbingu, huku 21% walikuwa wamaamini juu ya kuwapo kwa Kuzimu. Cha kushangaza pia, 67% ya Wamarekani walionyesha kuwa na imani kubwa juu ya kuwapo kwa maisha mengine baada ya kufa. Januari 31, 2000 katika toleo la gazeti la Newsweek, kura zilionyesha kwamba 64% ya wale walioulizwa walikuwa wanaamini juu ya Kuzimu, huku 25% walikuwa hawaamini juu ya kuwapo kwa Kuzimu. 9% walisema kuwa hawajui kama kuna Kuzimu.
Baada ya kusoma kitabu cha Dr. Moody kiitwacho, “Life After Life,” niligundua kuwa katika kitabu chake hiki, anatoa shuhuda nyingi za watu waliowahi kupitia uzoefu wa kufa. Niliishia kuwa na picha kwamba kila mmoja ya watu aliofanya nao mahojiano, aliyewahi kupitia uzoefu wa kuwa nje ya mwili, ama aliona Mbingu au alienda Mbinguni. Dr. Moody anaelekea kuonyesha kwamba hakuna aliyeona Kuzimu – ambao si utafiti wenye mizania nzuri sana. Kuzimu ni halisi kama ilivyo Mbingu. Inasikitisha kufikiria jinsi ambavyo watu wengi wanapuuza wazo la kuwapo kwa mahali kunakoitwa Kuzimu.
Tafiti Zaidi – Gazeti la NEWSWEEK 1/31/00
Waliosema kuwa Kuzimu ni mahali halisi ambako watu wanapata mateso ya moto ya milele: 1997-48%; 2000-34%
Waliosema kiwa Kuzimu ni hali ya maumivu makali ya mtu kuishi akiwa ametengwa na Mungu milele: 1997-46% 2000-53%;
Waliosema kuwa hawajui: 1997-4%; 2000-11%
Wakati nilipokuwa nje ya mwili nilimwona Mungu, Kuzimu na Wafu Walio Hai wakiwa Mbinguni (yaani watu waliokufa zamani lakini sasa wako hai Mbinguni). Kimsingi, hakuna mtu anayetaka kwenda Kuzimu, bali kila mmoja anataka kwenda Mbinguni bila kuwa na maandalizi yoyote ya kumwezesha kufika huko. Yesu, aliye Mungu wa Maandiko ya Agano Jipya aliongea mara nyingi kuhusiana na Kuzimu na wale wote watakaoenda kule.
“Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa Jehanum ya moto.” (Mt 5:22).
“Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya Jehanum?” (Mt 23:33).
“Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.” (Mt 11:23).
Napenda sasa nizungumzie juu ya uzoefu wangu wa kuwa nje ya mwili. Ilikuwa ni wakati huo ndipo nilipomwona Mungu. Nimekuwa nikisimulia ushuhuda huu kwa miaka mingi sasa, tangu siku ulipotokea. Mwaka 1998, Mungu Mwenyezi alinitokea na akaniambia kuwa alikuja kuzungumza na mimi kuhusiana na Kuzimu, na kwamba alitaka na mimi pia nizungumze na wengine kuhusiana na Kuzimu. Alisema kuwa alitaka kunipeleka Kuzimu, safari hii kwa kutoa roho na nafsi yangu nje ya mwili kwa muda wa saa 3 na dakika 45. Pia alisema kuwa angenifunulia upande mwingine wa Kuzimu unaoitwa Giza la Nje.
Kabla sijakusimulia juu ya kuwa kwangu nje ya mwili kulikonifikisha hadi Kuzimu, napenda hata hivyo ufahamu kwamba kumwona kwangu Mungu Mwenyezi mwaka 1998 haikuwa mara ya kwanza kwangu. Kwa hiyo, haikuwa jambo la kushangaza. Nilishamwona Mungu mara zingine mbili kabla ya kutembelewa naye mwaka 1998. Mara ya kwanza ilikuwa ni Oktoba 1988. Mara ya pili ilikuwa ni Desemba 1992, na ni wazi kuwa mara ya tatu ilikuwa ni hii Oktoba 1998.
Oktoba 5, 1998, saa 3:45 asubuhi, ulikuwa ni muda ambao ndipo Mungu Mwenyezi alinitokea na kuniambia kwamba alikuja kuzungumza na mimi kuhusiana na Kuzimu, na kwamba alitaka na mimi pia nizungumze na wengine na kuwaonya kuhusiana na mahali hapo panapoitwa Kuzimu. Aliniambia kuwa angeniruhusu nione kwa undani … kwa kina sana kama nilivyoona mwaka 1998. Vilevile, aliniambia kuwa alitaka kunionyesha undani wa sehemu hii iitwayo “Kuzimu”, ambako ni tofauti kabisa na vile nilivyoona mwaka 1980.

Wazazi, kama mnasoma kitabu hiki kwa watoto wenu, natumaini kuwa mtakisoma kwa hadhari na welewa. Mambo niliyoandika ni mambo yanayohusiana na kile ambacho Mungu Mwenyezi alinionyesha kwa Roho Mtakatifu wake. Ingawaje mambo haya yanaweza kuwa ya kutisha, nasikitika kusema kuwa, yote ni ya kweli kabisa. Mungu Mwenyezi alichukua roho yangu na nafsi yangu nje ya mwili wangu na kuniruhusu nimwone uso kwa uso. Mungu aliniruhusu kwa Roho Mtakatifu wake, nione vyumba 175 Kuzimu. Alinionyesha mashimo ya Kuzimu. Alinionyesha ndimi za moto na mioto ya Kuzimu. Alinionyesha Ziwa la Moto, na alinionyesha baadhi ya watu wanaoteswa Kuzimu kwa ndimi za moto.
Alinionyesha mapepo na ‘familiar spirits’. Pia aliniwezesha kumwona Lusifa, ambaye pia anajulikana kama Shetani na Ibilisi, na anaitwa na baadhi ya wasomi Beelzebub. Katika ulimwengu wa Biblia ambao tunaishi ndani yake, unaojulikana zaidi kama jamii ya Kikristo, labda anajulikana zaidi kama Lusifa, kerubi aliyeanguka. Mwenyezi Mungu alinionyesha kweli zingine za kiroho ambazo zinaweza kuhitaji kitabu kingine kuzielezea zote.
Mwenyezi Mungu aliniambia kuwa kitabu hiki kitachapishwa na kwamba kitawafikia watu wengi wa mataifa mbalimbali. Mungu aliniambia kwamba kitawasaidia baadhi ya watu. Alinionyesha chumba kinachoitwa Chumba cha Wafu wa Baadaye. Aliniruhusu niongeee na nione watu ambao hawajafa bado, lakini bado wanaishi duniani. Alinichukua na kunionyesha yajayo ili nione wengi wa watakaokufa; na kwamba hakutaka wafe na kuishia Kuzimu. Aliwataja kama Wafu wa Baadaye. Mungu Mwenyezi aliniambia kuwa ameniita mimi kwenye huduma yake na amenipaka mafuta kuwa mmoja wa manabii wake. Alisema kuwa ningeona maono mengi, na kwamba angenifunulia mambo mengi kwa nguvu yake ya kiungu. Alisema kuwa ningekuwa na ufahamu usiokuwa wa kawaida kuhusiana na binadamu, kwani Roho Mtakatifu wake angeniwezesha. Pia alisema kuwa angenionyesha matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa kabla ya kutokea duniani. Na cha muhimu zaidi, aliniambia kwamba ameniita kuwa shahidi kwa niaba ya Ufalme wake Mtakatifu na kwa ajili ya kugeuza mioyo ya watu imwelekee Yeye.
Tangu nilipopitia uzoefu wa kuwa nje ya mwili mwaka 1998, Mungu ameruhusu yote haya kutokea katika maisha yangu. Nimeshaona maono mengi na nimewafunulia watu wengi mambo binafsi kuhusiana na maisha yao. Vilevile, nimeshatoa unabii juu ya matukio mengi ya kitaifa na ya kimataifa, ambayo yote yametokea, na yote haya ikiwa ni kwa Roho wa Mungu.
Utangulizi wa Kuzimu:
Kwenda kwangu mara ya kwanza
Septemba mwaka 1980, nilikuwa nimefika nyumbani kutokea shuleni, nikiwa nimechoka sana. Nakumbuka nilipanda ngazi kuelekea chumbani kwangu kwenye nyumba yetu ya vyumba vinne iliyoko East Spencer, North Carolina. Nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba niliweka vitabu vyangu sakafuni pembeni mwa kitanda na kurukia kitandani ili nipate japo usingizi kidogo, kitu ambacho kilikuwa ni kawaida yangu kila nitokapo shuleni, lakini safari hii huu haukuwa usingizi wa kawaida.
Nilipolaza tu kichwa changu kwenye mto, nilipatwa na hisia kuwa nilikuwa nanyofolewa kutoka kwenye mwili wangu. Nakumbuka niling’ang’ania shuka langu kwa mikono yote miwili, nikijaribu kujitia nguvu, lakini hali hiyo haikuondoka. Nilijihisi nikiondoka kwenye mwili wangu na kupenya moja kwa moja kwenye kitanda changu, huku nikielekea chini. Labda naweza kusema kuwa hisia hizo ni kama zile hisia za mtu awapo kwenye lifti inayoshuka chini na wewe unapata hisia fulani tumboni mwako. Hivyo hasa ndivyo nilivyojisikia. Na jinsi nilivyokuwa nashuka chini, kila kitu kilianza kuwa cheusi.
Hakukuwa na nuru … hakukuwa na sauti. Kisha ghafla nilijiona nateleza kwa kutumia tumbo. Hisia zilikuwa ni kama nateleza kwenye mawe, huku mikono yangu ikiwa imenyooshwa kwa mbele kama vile naogelea. Nilipitiliza kwenye shimo, kama shimo la mgodi wa makaa ya mawe chini ya ardhi, ambamo kuna giza totoro na ni baridi.
Nilianza kuona ulimi mdogo wa moto ambao ulionekana unatokea kwenye shimo nilimokuwa nimelala. Niliyachunguza mazingira yangu nikiwa nimelala pale shimoni. Ilinikumbusha juu ya pango. Sehemu hii ilifunika mwili wote wa kiroho. Nilijihisi kana kwamba niko ndani ya jeneza la jiwe. Nikiwa nimelala kwa tumbo, na uso wangu umeelekea chini ardhini, niligundua kwa mshangao kwamba mikono yangu ilionekana kama imetengenezwa kwa moshi mchafumchafu mweupe! Kisha nikaanza kuuchunguza mwili wangu wote. Ilikuwa ni hapo ndipo nilipogundua kwamba nilikuwa naangalia roho na nafsi yangu! Hii haikuwa ndoto! Wakati huo, nilitamani kwamba ingekuwa ni ndoto. Nilianza kupiga kelele na kuanza kuwaita ndugu zangu kuomba msaada. Kadiri nilivyopaza sauti zaidi kuomba msaada, ndivyo mwangwi ulivyonirudia kutokea mle shimoni.
Nikiwa nawaza, nilijisemea, “Roger, umeshakufa!” Hakukuwa na alama zozote kwenye lango la Kuzimu zinazosema Karibu Kuzimu; lakini bado nijua moyoni mwangu kwamba huko ndiko nilikokuwa. Nilijua kuwa nilikuwa katikati ya viumbe vya kutisha, vya kipepo, vyenye sura mbaya. Nilihisi uwepo wa uovu kote kunizunguka wakati nikiwa nimelala pale.
Shimo lile lilikuwa kama futi tatu kwa upana kwa futi sita urefu, likiwa limejengwa kwa mawe. Nilitambua kuwa nilikuwa nimekufa na nilikuwa Kuzimu, na sikuwa na jinsi ya kutoka humo kamwe! Nilianza kumwita Mungu; nilipaza sauti, “Mungu, tafadhali nisaidie!” Tena na tena nilimwita Mungu, lakini sikujibiwa.
Nikiwa nimelala gizani, nilijiuliza, “Nimefanya nini ambacho kilikuwa kibaya sana hadi kikamfanya Mungu anilete Kuzimu?” Ndipo nilisikia maneno ambayo hayakuwa yangu. Ilikuwa ni kama sauti ya mwanamume. Sauti ile iliniambia kwamba nilikuwa mbahili na mchoyo. Sauti iliendelea kusema kuwa nilikuwa mkatili kwa watu wengine. Kisha ghafla, nilianza kuona kupitia ule ukuta wa mwamba kama vile kuangalia kwenye skrini ya televisheni. Nilionyeshwa kila kitu ambacho nilifanya kwenye maisha yangu ya duniani. Niliona wakati niliposema uongo kwa wazazi wangu au kwa kaka zangu, niliona pale nilipotenda mambo ili kuwaumiza rafiki zangu, na kusema maneno ya kuumiza. Niliweza hata kuhisi kuumia kwao.

Niliona wakati mmoja ambapo mimi na kaka yangu Tony tulipokuwa tukimwangalia kaka yangu Bernard na binamu yetu Mark walipokuwa wakimkatakata mbwa tulipokuwa bado wadogo. Ingawaje yule mbwa hakufa, niliona wakimkata mkia, na sisi tulikuwa tukicheka.
Baada ya kuziangalia dhambi zangu za zamani, nilitambua kuwa ilikuwa ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nilikufa na kutupwa kuzimu. Nilifanya jaribio moja tena la kumwomba Mungu, nikasema, “Mungu, tafadhali nisaidie! Ninasikitika kwa mabaya yote niliyowahi kufanya!” Nilimwambia kuwa natubu kwa kusema uongo kwa wazazi wangu, kaka zangu, kwa kuwaumiza rafiki zangu, na kwa kumtesa yule mbwa mdogo. Nilianza kulia sana, huku nikimwomba Mungu anisamehe, na kunitoa kwenye lile shimo.
Ghafla, nuru pamoja na nguvu fulani vilikuja pale shimoni na kunivuta mara moja. Nilijiona nikielea juu na nikaanza kuona mwanga. Kadiri nilivyoendelea kutazama, niligundua ulikuwa ni mwanga wa jua ukipenya kupitia dirisha la chumba changu. Niliuona mwili wangu ukiwa umelala uso chini kitandani kwangu; na nguvu isiyoonekana ilinisukuma kuelekea kwenye mwili wangu. Kwa mara ya kwanza nilijiona jinsi nilivyo kutokea nyuma bila kutumia kioo. Niliweza kuona fanicha zote chumbani kwangu.
Wiki moja kabla ya kufa kwangu na kutoka nje ya mwili, rafiki yangu mmoja wa shuleni aliniazima kalamu ya wino mweupe, na nilikuwa nameitafuta kwa wiki nzima. Sikuweza kuipata. Nilipokuwa narudi kwenye mwili wangu, huku nikiona mwanga wa jua uliokuwa unapitia dirishani kwangu, nilianza kuona eneo lote la chumbani kwangu kwa uwezo usio wa kawaida. Nakumbuka niliangalia sakafuni ambapo niliona vitabu vyangu vya shule. Na kwa kutumia uwezo huu, niliweza kuona moja kwa moja hadi chini ya kitanda changu. Nilishangazwa sana na huo ugunduzi wangu. Nikiwa naona kwa macho yangu ya kiroho, niliiona ile kalamu ya wino mweupe ya rafiki yangu ambayo nilikuwa naitafuta. Ghafla, ile nguvu isiyoonekana ilianza kuivuta roho yangu na mara nikawa kwenye mwili wangu.
Niliruka kutoka kitandani na, ili kuthibitisha kwamba sikuwa naota, niliinama na kuchungulia chini ya kitanda. Na hakika kabisa, ile kalamu ilikuwa iko pale. Nikiwa niko pale sakafuni, nilianza kumsifu na kumshukuru Mungu kwa kutoiacha roho yangu Kuzimu.
Sikumweleza mtu yeyote juu ya kile kilichonitokea. Wiki kadhaa zilipita, na nikaanza kutafakari juu ya kule Kuzimu, kitu ambacho kilinifanya nimuulize Mungu kuhusiana na safari yangu ya Kuzimu. Ndio nilikuwa tu nimetoka kuokoka mwaka 1979! Sasa, kwa kuwa nilikuwa Mkristo, sikutarajia kuwa Mungu angenipeleka Kuzimu. Nilimwomba Mungu na kumwuliza, “Kwa nini mimi? Kwa nini umengoja muda mrefu hivyo kunipeleka Kuzimu?”
Sikutarajia kuwa Mungu angenijibu maombi yangu haraka hivyo. Kwa mshangao wangu, alinijibu mara moja, kwa sauti ya kusikika kabisa, akisema, “Roger! Sikukupeleka Kuzimu kwa kuwa u mwenye dhambi. Sababu ya kukupeleka ni kwa niaba ya wenye dhambi. Nilitaka uwe shahidi kwa niaba yangu. Kwa hiyo, niliruhusu roho na nafsi yako ya kibinadamu itoke nje ya mwili kwa dakika mbili na kuiweka kwenye shimo Kuzimu, ili uweze kujua mwenyewe kwamba Kuzimu ipo. Nataka uwaambie watu wa kila rangi kwamba umeiona Kuzimu, na kuwaonya watubu dhambi zao. Waambie kwamba Kuzimu ni mahali pabaya sana pa mateso. Waambie wayatoe maisha yao kwangu kabla hawajachelewa. Nimekuchagua wewe uwe shahidi uwaonye watu wengi juu ya ubaya mkubwa wa Kuzimu.”
Baada ya kuisikia sauti ya Mungu, niliogopa. Nikahitaji mtu wa kuzungumza naye, kwa hiyo niligeukia kwa kaka yangu Tony, na nikamweleza jinsi nilivyoisikia sauti ya Mungu na kwamba alikuwa akizungumza na mimi. Nilimwambia kaka yangu kwamba Mungu aliniambia kuwa amenichagua kuwa shahidi kwa niaba yake. Nilipokuwa nasema haya kwa kaka yangu, aliniamini moja kwa moja, kisha naye akaanza kuogopa.
Shahidi maana yake nini? Shahidi ni mtu ambaye amekusanya taarifa sahihi na kuona yeye mwenyewe mambo yanayohusiana na jambo fulani. Na hicho hasa ndicho nilichopitia. Nimeona kwa macho yangu mwenyewe mahali hapa panapoitwa Kuzimu, na nikajua kwa nini baadhi ya watu wanakwenda Kuzimu – ni kutokana na sababu mbalimbali ambazo zingine huwezi kuzitarajia au unaweza kuwa hujawahi hata kuzisikia. Japokuwa utanisikia nikieleza haya na zaidi ya haya katika safari yangu ya pili Kuzimu ambayo ilikuwa mwaka 1998.
Sura ya Kwanza: Malango ya Kuzimu
Oktoba 5, 1998, nakumbuka niliangalia kwenye saa yangu kwenye chumba changu kimoja cha kulala katika mji wa Roseville, ambao ni sehemu ya Detroit, Michigan. Ilikuwa ni saa 3:45 asubuhi. Wakati nikiwa nimelala kitandani nikitafakari juu ya uwepo wa Mungu, na nikiwa katika uongozi wa Roho Mtakatifu, nilihisi udhihirisho wa uwepo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo kabla, mimi si mgeni na uwepo wa Mungu maana roho na nafsi yangu ya kibinadamu vimeshatoka nje ya mwili mara tatu tofauti, na kila mara, niliweza kutambua uwepo wa Mungu.
Mungu alisema kwa kinywa chake –
“Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.” (Yoh 10:3).
“Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.” (Yoh 10:4).
“Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.” (Yoh 10:5).
Hiki ndicho ambacho Mungu alisema nami, akimaanisha kuwa kila mtu anayemwamini atakuwa na uwezo wa kuutambua uwepo wake wa kiungu na mtakatifu, na ataweza kusikia sauti yake kwa namna yoyote ambayo Mungu ataamua kusema naye. Kama nilivyosema kabla, kuna nyakati ambazo nimesikia sauti ya Mwenyezi Mungu pale aliposema nami siku za nyuma. Ilikuwa ni sauti ileile ambayo niliisikia pale nilipotoka nje ya mwili wangu kwa mara ya kwanza mwaka 1980. Siku hiyo iliyokuwa na baridi ya Oktoba 1998, pale Mungu aliponitokea chumbani kwangu, alisema nami kwa Kiingereza. Niliweza kumsikia lakini sikumuona alipokuwa akizungumza nami. Mungu alizungumza nami, na alisema, “Nimekuja kuzungumza nawe kuhusiana na Kuzimu.”
Kuingia Kuzimu
Kisha aliniambia, “Nataka uanze kuongea na wengine kuhusiana na Kuzimu.” Nikasema, “Mungu, nimekuwa naongea, nahubiri na kufundisha kuhusiana na somo la Kuzimu kwa miaka karibu 20!” Halafu Mungu akaniambia, “Najua, lakini safari hii nitakupatia kitu cha kuzungumzia!”
Mungu aliendelea kusema, “Nitajidhihirisha kwako. Nitakuruhusu uone kwa undani zaidi, kama ulivyoniona mimi mwaka 1988. Nitakuruhusu uone kama ambavyo Petro, Yakobo na Yohana walivyoona saa chache kabla ya kusulubiwa kwangu na muda mfupi baada ya kufufuka kwangu.” Kisha Mungu akaniambia, “Nataka nikuonyeshe sehemu tofauti ya Kuzimu ambayo ni Giza la Nje. Nimekuja kuzungumza na wewe kuhusiana na Giza la Nje la Kuzimu. Giza la Nje la Kuzimu liko kwenye Mbingu ya Pili, ambako ni pa kutokea pa mahali pale nilipopaandaa kwa ajili yako na wale wote wanaoniamini Mimi. Sehemu hiyo ni Mbingu ya Tatu. Nitakuruhusu uone sehemu ndogo ya Mbingu ya Tatu utakapokuwa umemaliza kutembelea Giza la Nje la Kuzimu. Nitasema nawe kwa mara nyingine, Mbingu ya Pili ni mahali liliko Giza la Nje la Kuzimu liliko sasa hivi. Ni watu wachache walio hai duniani wameshaona sehemu hii ya Kuzimu. Makasisi wengi, wachungaji na wahubiri kwa ujumla, ambao wako hai duniani … nataka kuwaonyesha nao pia sehemu hii ya Kuzimu ambayo nataka nikuonyeshe. Nitakupeleka ndani ya Giza la Nje la Kuzimu, na kukuonyesha mateso makubwa sana na adhabu zinazowangoja wale ambao kwa kuamua wenyewe wamenikataa niwe Mungu Mwenyezi wao na Mwokozi wao. Watakuwapo baadhi ya watu watakaojaribu kupinga habari hii. Baadhi wataamini na baadhi hawataamini; lakini kwa wale ambao hawataamini, waambie kuwa nimesema katika Neno langu Takatifu kwamba, wale wanaonipenda, nitajidhihirisha kwao.”
“Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake” (Yoh 14:21).
Kisha Bwana Mungu akaniambia, “Nataka uwe shahidi wa kweli kuhusiana na uhalisia wa kuwapo kwangu na kuwapo kwa mahali hapa panapoitwa Giza la Nje la Kuzimu pamoja na mateso yake. Waambie watu kuwa umeniona Mimi na uwaambie kuwa umeona sehemu ya Kuzimu.”
Nilimwuliza Mungu, “Kwa nini umenichagua mimi ili kunipeleka Kuzimu na si wahubiri wengine?” Mungu akajibu, “Ni kwa sababu wewe unapatikana na wao hawapatikani. Si wote, lakini wengi wa wahubiri wangu wanaonitumikia duniani wanatenda dhambi maishani mwao. Wanadhani kuwa hakuna mtu anayejua, lakini Mimi najua kila kitu. sababu mojawapo ya Mimi kuruhusu uingie kwenye Giza la Nje la Kuzimu ni ili uweze kuona adhabu na mateso ya kutisha yanayowangoja wahubiri wanafiki na wasiotaka kutubu pale watakapokufa. Utaweza kuwaonya wale wanaohubiri na kufunza Injili yangu Takatifu.”
Nilitamani kumwambia Bwana Mungu kuwa sikutaka kwenda Kuzimu. Mwaka 1980, nilipoenda kwa mara ya kwanza Kuzimu na kurudi tena duniani, nilijiwekea nadhiri kwamba nisingeenda tena Kuzimu kwa sababu yoyote ile. Uzoefu wangu wa kwanza kuhusiana na Kuzimu ulikuwa wa kutisha mno!
Kabla sijatamka neno kumwambia Mungu kwamba sikutaka kwenda Kuzimu, nilihisi roho na nafsi yangu ya kibinadamu ikivutwa nje ya mwili wangu. Kwa haraka sana, tayari nilikuwa nimesimama pembeni mwa kitanda changu nikiwa katika roho. Nilijikagua mara moja, kisha nikautazama mwili wangu. Niliona mwili wangu ukiwa umekaa kitandani, kisha nikauona ukiangukia tena kitandani! Niliona jinsi kichwa changu kilivyogonga ubao wa kichwani mwa kitanda.
Kisha kwa ghafla, kwa mshangao, nikaona mwanga mkali mweupe ambao uligeuka na kuwa na umbo la mtu, ambaye alitembea kunijia huku akipenya kwenye ukuta wa chumba changu! Ile nuru ilipungua, na yule mtu akawa anaonekana wazi.
Ilikuwa ni wakati uleule ndipo nilipomwona Mungu Mwenyezi chumbani kwangu. Nilikosa cha kusema! Niliingiwa na hofu na pia shauku kwa wakati uleule, wakati nilipomwangalia Mungu kwa haraka na kwa kumheshimu sana. Niseme kuwa, siwezi kukupatia maelezo makamilifu ya jinsi alivyo kwa sababu maneno hayawezi kuelezea uzuri alio nao, lakini nitajitahidi kadiri niwezavyo. Machozi hunijaa machoni kila mara ninapowaeleza watu kwamba nilimwona Mungu. Kisha Mungu akasema, “Nitazame. Mimi ni Mungu Mwenyezi, Mwokozi wa ulimwengu na Yeye aliyeumba Mbingu na Nchi, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Vitu vyote viliumbwa na Mimi.”
Mungu aliendelea kusema, “Nimekuja kukuruhusu unione kama ambavyo wale mitume kumi na mbili walivyoniona, saa chache kabla ya kusulubiwa kwangu na siku kadhaa baada ya kufufuka kwangu. Nataka uwaambie watu kuwa umeniona. Ni kwa kusudi hili ulizaliwa: kuwa shahidi aliyeona ukweli wa kuwapo kwangu. Nakutuma kama nabii na mjumbe wangu. Nitakupatia ishara kwamba nimekuchagua wewe. Na ishara hiyo ni kwamba utawafikia watu wengi nje ya jamii (race) yako na taifa lako; na karama za Roho Mtakatifu wangu zitatenda kazi kupitia wewe. Utakuwa na maarifa yasiyo ya kibinadamu juu ya watu mbalimbali. Nitafunua kwako kweli fulani na mambo ya siri ambayo yamo mioyoni mwa watu wengi. Hii ndiyo itakayokuwa ishara yangu kwako na nyingine nyingi na kwamba nimekuruhusu kuniona na nimekupatia ufahamu huu mkubwa juu ya Giza la Nje la Kuzimu. Nataka uwaambie watu kuwa nimekuruhusu kuniona Mimi na kwamba nitakuja hivi karibuni kuhukumu ulimwengu; na uwaambie kuwa nawapenda sana. Pia uwaambie kuwa nataka wajue kile kinachotokea kwa mtu baada ya kufa.” Niliangalia wakati Mungu Mwenyezi akigeuza mgongo wake kwangu, kisha akanitazama tena. Halafu alinyosha mkono wake na kusema, “Niguse.”

Kwa hiyo, nilinyosha mkono wangu wa kushoto na kugusa mkono wake wa kulia, na kwa mshangao wangu, alikuwa mgumu tu na ana mwili kabisa! Wakati Mungu aliposimama mbele yangu, alikuwa na tabasamu usoni mwake. Alizungumza na kuniambia, “Roger, wewe umeshakufa, lakini usiogope. Ubongo wako, moyo wako na damu yako vitahifadhiwa kwenye mwili wako wa nyama.” Baada ya kumsikia Mungu akisema hivi, niliutazama tena mwili wangu ambao ulikuwa hauna uhai ukiwa umelala pale kitandani. Ukweli kabisa ni kwamba, wala sikuwa najisikia kwamba nimekufa! Nilijisikia niko tu hai na nina amani kabisa. Vilevile, wakati ule, nilijiona niko salama kuliko nilivyowahi kujisikia maishani mwangu mwote. Furaha isiyoelezeka ilinifunika. Nilijisikia nikiwa katika umoja na Mungu.
Bwana Mungu aliniambia, “Nimekuja kukuchukua ili ukatembelee Giza la Nje la Kuzimu. Tutatembelea huko kwa saa tatu na dakika arobaini na tano. Nitakufundisha na kukuonyesha uwepo wa kweli wa mateso ndani ya Giza la Nje la Kuzimu.” Niliposikia Mungu akisema hayo kwangu, … wakati uleule, nakumbuka nilipata hisia za kwamba ninapaa katikati ya giza kwenye anga; kwanza kuelekea juu angani, kisha polepole, nikaanza kushuka kwenye giza totoro hadi nikawa siwezi kuona chochote. Kisha Mungu akaniambia, “Tumeshafika kwenye Lango la Kuzimu.” Sikuweza kuona chochote kila upande, lakini niliweza kumwona Bwana kwa sababu mwili wake ulikuwa unatoa nuru. Nilipomwangalia, mwili wake na uso wake ulifanya nisiweze kutazama sawasawa kutokana na mng’ao. Nilipomtazama mwili wake ukiwa unatoa nuru nyeupe, mara moja ulinijia mstari wa Biblia ambapo Yesu anasema kuwa Yeye ni Nuru ya ulimwengu.
“… Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na niru ya uzima.” (Yoh 8:12).
Nuru iliyokuwa inatoka kwenye mwili wa Mungu ilikuwa inatosha tu kwa mimi kuona eneo tulikokuwa tumesimama. Nilikuwa nimesimama Kuzimu. Eneo hilo lilinikumbusha juu ya mgodi wa makaa ya mawe wa chini ya ardhi. Ardhi ilikuwa imeundwa kwa mawe meusi; kuta zilikuwa hivyo hivyo; na angahewa la hapo nalo lilikuwa jeusi tii. Nakumbuka ilikuwa ni kama nimesimama kwenye barabara chafu iliyokuwa kama vile ya mawe, lakini mawe hayo yalikuwa ya baridi. Namkumbuka Mungu vizuri sana. Nakumbuka jinsi alivyoniangalia na kusema, “Nimekuleta hapa ili nikuonyeshe upande mwingine wa Kuzimu tofauti na ulivyozoea kusikia baadhi ya wahubiri wakifundisha. Nitakuonyesha eneo tofauti … tofauti kabisa na vile nilivyokuonyesha mwaka 1980.”
Nakumbuka jinsi Kuzimu kulivyokuwa nilipopaona mwaka 1980. Rafiki zangu, kama umewahi kupitia uzoefu wa kuwa nje ya mwili na ukaona sehemu yoyote ya Kuzimu, unajua vema kwamba hautakaa usahau kamwe sehemu hiyo ya kutisha!

Kisha Mungu akaniambia, “Kutakuwa na nyakati ambazo nitaongea na wewe kwa Kiaramu, Kiebrania na Kigiriki.” Mungu alianza kuzungumza na mimi kwa Kiebrania na Kigiriki. Alisema, “Kuna maneno manne ambayo nitayatumia ambayo yako kote kwenye Biblia ili kuelezea juu ya Kuzimu. Neno la kwanza ni la Kiebrania nalo ni Sheol [sheh-ole’], ambalo linamaanisha ulimwengu wa wafu au kaburi. Hapa ni mahali ambapo roho za wasio wacha Mungu pamoja na za wacha Mungu zilikokuja pale walipokufa karne nyingi zilizopita. Neno la pili ni la Kigiriki Hades [hah’-dace], ambako ni mahali zinakoenda roho za watenda dhambi baada ya kufa. Hata hivyo, kabla ya kusulubiwa na kufufuka kwangu, Hades ilikuwa imegawanyika sehemu mbili ambazo zilikuwa zimetengwa na bonde kubwa lisilopitika, nililolitengeneza Mimi. Sehemu ya juu ya Hades ilijulikana kwa jina la ‘Kifuani mwa Ibrahimu’ au Paradiso. Chumba cha Waliolaaniwa ni sehemu ya palipokuwa Kifuani mwa Ibrahimu kwenye Hades. Nitakuruhusu uone Chumba cha Waliolaaniwa kabla ya kumaliza ziara hii yako kwenye Giza la Nje la Kuzimu. Kwenye Paradiso iliyolaaniwa ya Giza la Nje la Kuzimu, kulikuwa kuzuri sana zamani. Kulikuwa na vijito vya maji vikipita humo pamoja na miti ya kijani. Ilikuwa ni kama bustani inayotunzwa vizuri. Humo kulikuwa na zile roho zote za watu ambao walikufa na kuweka matumaini yao kwangu Mimi kama Mungu wa kipindi cha Agano la Kale, hadi wakati wa kufa na kufufuka kwa Bwana na Mwokozi wako, Yesu Kristo. Roho hizo zote zilizokuwa kwenye Paradiso ya Hades [Hell] walikuwa na ufahamu wote kabisa. Hazikuwa ni roho zilizolala. Walikuwa wako hai kabisa. Baada ya kusulubiwa, nilitumia siku tatu Hades, nikihubiria roho zilizokuwa humo.”
“…ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;” - 1 Petro 3:19).
Mungu aliendelea kusema, “Waamini wote waliokufa wakati wa Agano la Kale waliponiona Mimi pale Paradiso ya Hades kwa siku tatu, kwa mfano Adamu, Eva, Mfalme Daudi, Musa, Ibrahimu na maelfu wengine, walifurahi sana. Mwisho wa zile siku tatu, waamini hao wote wa Agano la Kale, na wale wote ambao waliamini hadi kufikia wakati wa kifo cha Bwana na Mwokozi wako Yesu Kristo, niliwatoa kutoka hapo Kifuani mwa Ibrahimu … Paradiso ya Zamani iliyokuwa kwenye Hades. Niliwapeleka kwenye Paradiso Mpya, ambayo iko kwenye Mbingu ya Tatu, ambako ndiko wanakoishi hadi hivi sasa. Hadi sasa, Paradiso Mpya bado inaitwa ‘Kifuani mwa Ibrahimu’. Watu wote walioishi katika Agano la Kale, ambao hawakuweka imani yao kwangu kama Mungu wao, walipokufa, roho zao zilikuja hapa Hades. Wao walifungwa kwenye upande wa chini, kushoto kwenye Hades, ambako kuna mateso mengi na mioto inayolela maumivu makali. Sehemu hii ya Hades au Hell pia inajulikana kama Mashimo ya Moto ya Hades (Fiery Pits of Hades). Ziko roho nyingi sana zinazoungua kwa moto kwenye mashimo hayo hivi sasa.
Neno la tatu linaloelezea Kuzimu nalo ni la Kigiriki, yaani Tartaros [Tar-tar-os’]. Tartaros ni hii sehemu ya Kuzimu ambayo ndiyo hasa nataka uione. Hii ndiyo sababu ya kukuleta hapa Kuzimu – ili uweze kuwa shahidi kwa watu wote kule duniani, ukishuhudia kwamba kuna sehemu ya adhabu na hukumu kali sana kwa wale wasiotii Neno Takatifu, ambalo linaitwa Biblia. Sehemu hii inajulikana kama Giza la Nje la Kuzimu. Tartaros ina vyumba vingi vya jela. Nimeongelea juu ya Tartaros katika Neno langu Takatifu. Sehemu hii ya Kuzimu ina malaika ambao walifanya dhambi za uzinzi na wanawake wa duniani kabla ya gharika ya Nuhu. Nilitaja Tartaros mara moja tu kwenye Biblia yote: kwenye kitabu cha pili cha Petro, sura ya pili, mstari wa nne.”
“Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;” (2 Peter 2:4).
“Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.” (2 Peter 2:17).
Mungu aliendelea kuniambia, “Pia nilimwambia Mtume wangu, Yuda, aandike juu ya Giza la Nje la Tartaros kwenye Kitabu changu Kitakatifu.”
“Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.” (Yuda 1:6).
Kumbuka:
Ili kujua zaidi juu ya malaika ambao hawakuilinda enzi yao wenyewe, tazama Mwanzo 6:1 hadi 6:5.
Mungu akasema, “Malaika walioanguka ambao nilimwambia Petro aandike juu yao bado wanaendelea kuadhibiwa hadi sasa kwa kitendo chao cha kuzini na wanawake wa kibinadamu kama wafanyavyo wanadamu. Malaika walioanguka walifanya mapenzi na binti za wanadamu, jambo ambalo Mimi naliona ni baya kabisa. Baada ya muda mfupi nitakupeleka Tartaros kwenye Giza la Nje la Kuzimu na kukuruhusu uwaone malaika walioanguka ambao waliacha enzi yao wenyewe, ambao wamefungwa kwa minyororo, wakisubiri Hukumu Kuu ya Kwenye Kiti Cheupe cha Enzi, ambayo dunia yote itashuhudia.”
Kisha Mungu alinitazama moja kwa moja machoni, na kusema, “Nimekuja kukuonyesha Zophos [Dzof’-os] na Choshek [Kho-shek’] ambazo ni sehemu za Kuzimu.” Alifafanua akisema, “Zophos ni neno la Kigiriki lenye maana giza, weusi na utusitusi wenye unyevu. Choshek ni neno la Kiebrania. Nalo lina maana ya giza. Pia, linamaanisha mateso, uharibifu, mauti, huzuni na uovu. Nilijaribu kuonyesha sehemu hii kwa wengi wa watumishi wangu, mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na walimu, lakini ninakuonyesha wewe kwa sababu wewe unapatikana.”
Kisha maneno yake yakawa makali. Alisema, “Mwanangu, kile ambacho naenda kukuonyesha na kukufundisha kuhusiana na Kuzimu ni cha kweli, kwa hiyo, angalia, sikiliza na ujifunze. Kwenye upande huu wa Kuzimu, kuna giza sana. Nimepataja kwenye Injili yangu … kwenye Kitabu changu Kitakatifu, ambacho mnakiita Biblia Takatifu. Ziko roho nyingi sana mahali hapa. Mwanangu, tazama, sikiliza na ujifunze. Kile ambacho naenda kukuambia, kisha kukuonyesha baada ya muda mfupi, ni kweli. Roho nyingi ziko hapa Kuzimu sasa hivi. Baada ya muda mfupi utasikia maelfu kwa maelfu ya watu wakilia. Kumbuka kile nilichosema kwenye Injili yangu, kwenye kitabu cha Mathayo Mtakatifu, sura ya nane, mstari wa kumi na mbili.”
Mungu alinukuu:
“…bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” (Mathayo 8:12).
Mungu aliendelea kusema, “Neno la nne linaloelezea Kuzimu ni Geenna [Gehenna - Gheh’-en-nah] kwa lugha ya Kigiriki. Nataka ufahamu kuwa, kama mtu yeyote anayeishi duniani leo, akimkataa kabisa Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, pale atakapokufa ataletwa hapa Hades na kuungua kwenye Gehenna, mahali ambako moto wake hauzimiki.”
“Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.” (Mathayo 5:22).
“Jicho lako la kuume likikukosea, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.” (Mathayo 5:29).
“Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.” (Mathayo 5:30). Tazama pia Marko 9:43-47).
Mungu aliendelea kusema, “Gehenna (Jehanamu) ilikuwa ni sehemu ambapo wakazi wa Yerusalemu walikuja kutupa takataka zao; na sehemu hii ilikuwa ikiwaka moto saa ishirini kwa siku. Hapa pia zilitupwa maiti za wahalifu na kuchomwa moto. Harufu ya mahali pale ilikuwa ni mbaya sana, ikichafua hewa. Sehemu hii ilikuwa iko nje ya ukuta wa jiji la Yerusalemu, kwenye bonde la Hinomu. Nimeongelea kuhusu Gehenna mara nyingi kwenye Injili yangu. Nimelipa Ziwa la Moto jina la Gehenna ili kuonyesha kwamba linawaka saa ishirini na nne kwa siku. Litawaka na kuzitesa roho na nafsi za wanadamu wenye dhambi ambao wameamua wenyewe kunikataa Mimi. Gehenna imeandaliwa kwa ajili ya Shetani na malaika zake na pia kwa ajili ya mwanadamu yeyote ambaye hana shauku ya kunipenda na kunitii Mimi kama Mungu wake.”
“Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;” (Mathayo 25:41).
Mungu alinitahadharisha kwa kusema, “Unaenda kuona watu kutoka kila rangi na historia. Unaenda kuona roho nyingi sana za wanadamu na mapepo wabaya. Kuna nyakati ambapo mapepo na roho za wanadamu watakuona wewe na Mimi. Kuna nyakati ambapo mapepo na roho za wanadamu hawatatuona. Kuna nyakati ambapo mapepo na roho za wanadamu watakuona wewe tu, lakini hawataniona Mimi, na kuna nyakati ambapo mapepo na roho za wanadamu wataniona Mimi tu lakini hawatakuona wewe.”
Niligundua kuwa mwenendo wake ulibadilika ghafla. Uso wake ulionyesha huzuni. Alinitazama na kusema, “Mwanangu, kuna nyakati ambazo hautaweza kuniona Mimi.” Akaendelea kusema, “Kutoniona Mimi, haina maana kwamba siko pamoja na wewe. Sitaki uanze kuwaza kwamba katika nyakati hizo nimekuacha. Nataka ujue kuwa haitakuwa hivyo.” Alitulia kidogo kisha akaniambia, “Unakumbuka nilichosema kwenye Injili yangu, kwenye kitabu cha Yohana, sura ya kumi na nne, mstari wa 27?”
Mungu alinukuu: “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.” (Yoh 14:27).
Mungu aliendelea kusema, “Tazama, sikiliza, jifunze, maana … ‘tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”’ (Mathayo 28:20).
Kisha Mungu akasema, “Nifuate.” Kadiri tulivyotembea kwenye ile barabara nyeusi yenye mawe, mbele yangu niliona mwanga mdogo, na ndani ya mwanga ule, niliona maelfu ya watu wamesimama mbele ya kile kilichoonekana kama lango la kuingilia kwenye chumba kikubwa. Japokuwa hakukuwa na mwanga wa kutosha, niliweza kuliona lango hili na watu hao. Unajua, sitaweza kamwe kuwasahau watu wale kwa sababu nilisimama na kuwaangalia. Ni kawaida yangu. Mimi ni mtu ninayependa watu. Sijali ni watu wa aina gani. Ninapenda tu watu! Nilianza kuwaona watu hawa maelfu kwa maelfu wamerundikana pamoja; wamesimama kwenye mstari mrefu kwenye barabara ya mawe. Ilikuwa ni kama watu wanaongojea kuingia kwenye hoteli.
Malango ya Kuzimu
Nikiwa nimesimama pale, nikiwa nimewakazia macho watu wale, niligundua kitu kingine niipoangalia kushoto kwangu, kisha kulia. Niliona malango ya chuma makubwa mno kuliko niliyowahi kuona. Yalikuwa ni malango marefu sana, yaliyojaa kutu na meusi. Malango haya lazima yalikuwa karibia sawa na urefu wa maghorofa kumi na nne au kumi na tano. Yalikuwa na michoro ya ajabu ajabu ambayo ilinikumbusha kuhusu nyoka. Nikajisemea mwenyewe, “Haya lazima yatakuwa ni Malango ya Kuzimu.” Wakati nikiwa nimesimama pale, huku nikitazama juu kwenye malango yale, aya chache ziliniijia akilini kutoka kwenye kitabu cha Mathayo.
“Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.” (Mthayo 7:13).
“Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.” (Mathayo 7:14).
“ …na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.” (Mathayo 16:18).
Macho yangu yalianza kushangaa umati ule tena. Nilitembea kulelekea kwao hadi nikawa niko kati yao. Ilikuwa ni hapo ndipo nilipogundua kuwa ni watu wa kila rangi, wenye kila historia unayoweza kuifikiria. Ghafla, nikasikia mtu akiniita jina langu. Sauti ile ilisema, “Roger, unafanya nini hapa? Wewe hautakiwi kuwa hapa!” Nilitazama kushoto kwangu, maana huko ndiko sauti ilikotokea. Ndipo nikamwona kijana wa Kikokasia. Alonekana kuwa na urefu wa futi kama sita hivi. Nywele zake zilikuwa za rangi kahawia nyeusi, na alikuwa na masharubu kiasi. Alikuwa mrefu na aliyekonda, akiwa na shingo ndefu. Alikuwa ananikodolea macho, na akasema tena, “Roger, unafanya nini hapa? Wewe hautakiwi kuwa hapa!”
Huku nikiwa namuangalia, nilimwuliza, “Umejuaje jina langu? Akasema, “Nimekuona ukija hapa kutokea duniani.” Akasema tena, “Wewe hautakiwi kuwa hapa!”

Kwa mara nyingine nikamwuliza, “Umejuaje jina langu?” Naye kwa mara nyingine tena akasema, “Roger, tafadhali rudi ulikotoka. Hautakiwi kuwa hapa.” Nilipandwa na hasira na kudai aniambie amejuaje jina langu. Akajibu, “Mimi ni Bobby! Je, haunikumbuki? Mimi ni Bobby!” Nikamwambia, “Simfahamu mtu yeyote anayeitwa Bobby!” Akasema tena, “Haunikumbuki mimi? Tulikuwa tunasoma wote, na nilikuwa nikikaa kulia kwako kwenye darasa tulikokuwa tunafundishwa na mwalimu aliyeitwa Mrs. Ritchie.” Alianza kunikumbusha, lakini haikuwezekana. Kwa mshangao wangu, nilimgeukia Mungu ili anipe jibu. Nilimtafuta lakini nikagundua naye haonekani popote. Nikaanza kutembea kupita yale malango ya Kuzimu, huku nikiwapita watu mbalimbali. Nilikuwa nimeingiwa na hofu kwa sababu nilikuwa simuoni Mungu.
Nikiwa natembea kwenye barabara hii, angahewa lilionekana kugeuka kuwa jeusi zaidi na zaidi. Nilianza kulia. Niliancha kutembea na nikafunika macho kwa mikono yangu. Nilikuwa nimezidiwa na hali ile kihisia. Kisha Mwenyezi Mungu aliongea na mimi na kusema, “Amani yangu iwe na wewe.” Mara moja nilitoa mikono yangu machoni, na Mungu alikuwa hapo amesimama mbele yangu. Nikasema, “Mungu, ulienda wapi? Kwa nini uliniacha?”
Akajibu, “Usiogope! Nilikuahidi kuwa sitakuacha kamwe. Pia nilikuambia kuwa kuna nyakati ambazo utakuwa haunioni. Unaweza usinione lakini siwezi kamwe kuwa nje ya mahali ulipo.” Siwezi kuelezea, lakini baada ya kumsikia Mungu akiniambia maneno hayo, nilifarijika sana. Nilijisikia kama vile ninafunikwa na kwa blanketi lenye joto. Niligundua nilipomwangalia, kwamba alikuwa mzuri sana. Nitaeleza jinsi Mungu alivyo kadiri ya uwezo wangu baadaye kwenye kitabu hiki. Anapokuangalia, unaona na kuhisi upendo ukitiririka kutoka kwenye macho yake. Aliniambia, “Haya, tuondoke. Kuna mambo mengi ninayotaka kukuonyesha. Nitakuonyesha upande wa giza wa Kuzimu.”
Mimi na Mungu tulipoanza kutembea, niliweza kusikia sauti za ajabuajabu kwenye eneo lote. Zilikuwa kama za minyororo ikigongana, ikiburuzwa ukutani; kama vile wanyama wanalia, kama watu wakilia … na ilikuwa kama vile mtu au watu walikuwa wanakimbia mbele yetu, ingawaje sikuweza kuona lolote. Wakati nikiwa natembea pamoja na Mungu, nilishikilia mkono wake wa kushoto. Wakati huu nilikaa karibu sana naye.
Kuingia Hades
Niligundua kuwa tulikuwa tunatembea kwenye sehemu iliyoonekana kama barabara nyeusi yam awe. Japokuwa nilikuwa naona kidogo tu – kidogo tu kilichodhihirishwa na nuru iliyokuwainatoka kwenye mwili wa Mungu – niliweza kutambua baadhi ya vitu. Barabara ambayo mimi na Mungu tulitembea ilikuwa imepindapinda. Niligundua pia kuwa, baada ya kutembea kwa muda, harufu ya mahali pale ilikuwa ni mbaya sana. Kulinuka kama mnyama aliyekufa na kuoza. Wakati wote huo tulipokuwa tunatembea kwenye barabara ile, Mungu hakusema hata neno moja … hadi nilipopata wazo hili: “Hii haionekani kuwa kama Kuzimu ambayo huwa nasikia wahubiri wakiisema kule duniani. Kuzimu ambayo huwa naisikia ni ya moto na kiberiti.”
Nilishangaa kuona kwamba Mungu alikuwa anajua nilichokuwa ninawaza. Tuliacha kutembea, akanitazama na kusema, “Unataka kuona moto?” Kabla sijajibu, alinishika mkono wa kulia akapunga hewani, kisha akanyosha kidole chake cha shahada kwenye welekeo ambao ulikuwa giza kabisa. Aliponyoosha mkono wake, niligundua kuwa amevaa vazi jeupe lenye mikono mirefu hadi kwenye vifundo vya mikono. Mkunjo kwenye mikono ya vazi hili ilikuwa ni dhahabu safi. Alipoinua mkono wake wa kulia, mikono ya vazi ilianguka hadi kwenye kiwiko. Nilishangaa kuona tundu kwenye kifundo cha mkono wake! Nikawaza, “Ni kwa nini Mungu awe na tundu kwenye mkono wake?” Tundu lile lilikuwa la ukubwa wa sarafu ya nikeli! Tundu lile lilinikumbusha juu ya kusulubiwa kwa Yesu, isipokuwa tu nilijua kuwa Yesu alikuwa na matundu kwenye viganja kutokana na kupigiliwa misumari msalabani.
Nikiwa natafakari hayo, alipopunga mkono wake, eneo lote tulikokuwa tumesimama liliangazwa kwa nuru kali; na ilionekana kwamba, kadiri nilivyotazama maili nyingi mbele yetu, nilianza kuona mianga mingi midogomidogo ikiang

1 comment:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW