Sunday, December 4, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA TISA)


Daniel Mlango wa 5:
Belshaza ambaye alirithi ufalme toka kwa mfalme Nebukadneza Baba yake hakujifunza juu ya Mungu wa Mbinguni licha ya kujua yote ambayo Mungu aliyafanya wakati wa utawala wa Baba yake. Siku Moja Mfalme Belshaza , aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa. Akiwa katika kilele cha ulevi na anasa, akaamuru wavilete vile vyombo vya dhahabu na fedha, ambavyo baba yake, Nebukadreza, alivitoa katika hekalu ililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.
Na kibaya Zaidi ya haya Mfalme Belshaza akiwa katika anasa zake hakumsifu Mungu wa Mbinguni wala kumtukuza, Bali wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe. Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara maneno ambayo hakuna awezaye kuyasoma. Mfalme na wote waliokuweko katika ile sikukuu wakakiona kile kitanga cha Mkono kilichoandika.
Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana. Mfalme akaagiza waletwe wachawi, na wanajimu na wakaldayo na wenye hekima wa Babeli ili kwamba wapate kumsomea Maneno yaliyoandikwa Ukutani na kile kitanga cha mkono. Walakini wenye hekima wote wa Babeli hawakuweza kuyasoma naneno yake yote yaliyoandikwa. Walakini Malkia alimwendea Mfalme katika ile karamu kisha akamwambia kuwa asifadhaike kwani yupo Mtu aitwaye Danieli ambaye Roho ya Miungu watakatifu inakaa ndani yake na ambaye wakati wa Baba yake alimtafsiria Mfalme Nebukadneza ndoto zake zote alizoziota.
Mfalme akaagiza Kwamba Danieli aletwe ilia some naneno yale na kumjulisha mfalme tafsiri ya maneno yale kwa ahadi kwamba atapewa zawadi kubwa na kufanywa awe mtu wa tatu katika Ufalme. Danieli alivyoletwa mbele za Mfalme na kuyasoma yake maandishi aligundua maana yake. Nabii danieli akamkumbushia Mfalme kisa cha Baba yake jinsi alivvyojitukuza dhidi ya Mungu wa Mbinguni, na jinsi Mungu alivyokinyenyekeza kiburi chake.
Alimwambia Mfalme kwambaIngawa aliyafahamu hayo yote yaliyompata Baba yake, hakumtukuza Mungu wa Mbinguni bali aliagiza vyombo vya Mungu wa Mbinguni viletwe ili vitumiwe katika Ulevi na Anasa, na Zaidi ya hayo yote akaitukuza miungu ya miti na ya shaba na ya Mawe na kumsahau Mungu wa Mbinguni.
Ndipo Danieli akamsomea yale maneno yaliyoandikwa katika ule ukuta. Biblia yasema hivi;”- Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi. Ndipo Mfalme kwa Hofu alamvika danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake na kumtangaza Daniel kama Mtu wa tatu katika Ufalme. Lakini Hukumu ya Mungu ilitekelezwa siku ileile. Wamedi na waajemi waliuvamia Ufalme wa Babeli usiku ule na mfalme akauawa na Wamedi wakaumiliki Ufalme.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:1 na 30, Belshaza alikuwa ni nani? 

J: Herodotus, mwana historia wa Kigiriki akiandika karibu miaka 90 baada ya kuanguka kwa Babeli, hakumtaja Belshaza kabisa na alisema bayana kuwa mfalme wa mwisho alikuwa Nabonidus. Hadi karne ya 20, hayo ndio yalikuwa maneno ya mwisho kuhusu swala hili mbali yale yaliyomo kwenye Biblia. Hili ni moja ya mambo ambayo Wakristo wanaafiki kuwa yatakuja kuelezwa siku moja, bila kujua maelezo yenyewe.
Hata hivyo, kwenye karne ya 20, wataalamu wa elimukale wamegundua jedwali la kikabari liitwalo "Aya ya Kiajemi inayomzungumzia Nabonidus." Belshaza alikwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Nabonidus, na baada ya miaka mitatu ya kwanza ya utawala wake (mwaka 553 KK), Nabonidus alikwenda uhamishoni Tema Arabuni kwa hairi yake mwenyewe kwa miaka kumi, na Nabonidus alimteua Belshaza kuwa mtawala. Jambo la muhimu ni kuwa Wababeli walipoishinda Babeli, Nabonidus hata hakuwepo; alikuwa Tema sehemu ya kaskazini ya Saudi Arabia ya leo. When Critics Ask, uk.209 unahitimisha jambo hili, "Kwa kuwa Belshaza chini ya Nabonidus, jina lake lilisahauliwa, kwa sababu wana historia wa Babeli na Ugiriki za zamani walipenda kuongelea tawala za wafalme rasmi. Rekodi za Danieli zimehibitisha kuwa zina usahihi wenye kustaajabisha."
Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.286 inataja "maandishi ya Nabunaid" yaliyovumbuliwa huko Uru. Haya yanaweza kuwa ni ile ile "Aya ya Kiajemi inayomzungumzia Nabonidus." Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.286 pia unaongezea kuwa nyaraka za vikabari zinasema jinsi Belshaza alivyotoa sadaka za kondoo na ng’ombe kwenye mahekalu ya Sippar kama "matoleo ya mfalme."
Sasa Herodotus anachukuliwa kuwa sahihi kwa ujmla. Kama mtawala mwenza wa Belshaza (chini ya Nabonidus) hakuwa wa maana sana hata Herodotus, alipokuwa anaandika miaka 90 baadaye, alimsahau, ni kwa namna gani Kitabu cha Danieli kinaweza kutarajiwa kuandika jambo hili kiusahihi, isipokuwa kilikuwa tayari kimeishaandikwa kufikia muda huu? Kwa kuwa Danieli alijua jambo hili kuliko Herodotus, kama inavyoshangaza kuwa baadhi ya wanazuoni wenye kutilia shaka msimamo wa asili mwishoni mwa karne ya ishirini bado waliichukulia Danieli kuwa kitabu cha karne ya pili. Tazama 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.193 kwa maelezo zaidi kuhusu jambo hili.
Kitabu cha mwenye kushuku Asimov’s Guide to the Bible, uk.606 hakitoi maelezo haya, isipokuwa kinasema kuwa Belshaza (Bel-shar-utsur neno linalomaanisha "Bel, mlinde mfalme") alikuwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Nabonidus.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:1, je ni hali gani ya hewa ya kisiasa ambamo Danieli aliishi wakati huu?
J: Baada ya Nebukadneza wa sura zilizotangulia kufa mwaka 562 KK, kulikuwa na nyakati za shida. Wana historia wanaiita himaya hii ‘Himaya ya Babeli Mpya’, ili kutofautisha na himaya iliyopita iliyokuwa chini ya Hammurapi. Wafuatao ni wafalme wake:
Mwaka 627-605 KK Nabopolassar (Nabu-apal- usur)
Mwaka 605-Aug/Sep 562 KK Nebuchadnezzar II Nabu-kudurri-usur) Mwaka 562-Aug 560 KK Merodach mwovu (Amel-Marduk) mtoto wa kiume wa Nebukadneza (aliuawa)
Mwaka 560-556 KK Neriglissar (Nergal- Sharezer) mkwe wa Nebukadneza May-June 556 KK (miezi 2) Labashi-Marduk (aliuawa)
Mwaka 556-539 KK Nabonidus (Nabu-na’ia) Mwaka 553-Okt 11 au Des 539 KK Belshaza (Bel-shar-usur) (msaidizi wa mtawala aliye badala ya mfalme [vice-regents] kwenye himaya za kale za Umedi na Uajemi)
Okt 11 au Des 539 KK Gavano wa Uajemi Ugbar wa Gutium aiteka Babeli
Kwa mujibu wa mwanahistoria wa Kigiriki, Herodotus (1:191) njia waliyotumia kumtaka ilikuwa ya ubunifu mkubwa. Walijenga ziwa "kubwa" ili kuyahamisha maji kwa muda maji ya Mto Frati. Kisha usiku, walitembea chini ya ukuta ambapo Mto Frati ulikuwepo na kuwatokea Wababeli waliokuwa wanafanya sikukuu kwa kushtukiza.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:1, ni kwa jinsi gani Wababeli walikula sikukuu, wakati jeshi kubwa la Waajemi wa Umedi likiwa nje ya kuta?
J: Huenda yalikuwa ni majivuno yao ya jumla ya ulinzi wao, au ilikuwa ni onyesho la kushtukiza la ujasiri wenye lengo la kutisha. Kuta za mji zilikuwa kubwa, na sehemu ya ukuta ilikuwa (inavyoonekana) haiwezekani kushambulia kwa sababu Mto Frati ulipita chini yake. Mji ulijengwa kwa lengo la kuhifadhi chakula kwa muda wa miaka 20.
Pia mama wa Nabonidus alikuwa kuhani mkuu mwanamke wa Harani, mungu wa jua. Aliyafufua mahekalu mengi sana likiwemo hekalu la Sini la mungu jua Harani. Kwa hiyo sababu mojawapo ya kuchukua vyombo toka kwenye hekalu la Yerusalemu yawezekana ilikuwa ni kuonyesha ukubwa wa miungu yao. Sababu nyingine inayofanana nah ii huenda ikawa kuondoa athari ya Nebukadneza ya kumwinua Mungu wa Danieli.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:1-5, kwa nini unafikiri Mungu alichagua kuandika kimiujiza kwenye ukuta, na kutangaza hatima yao muda huu?
J: Kuna sababu mbili. Kwanza, walikuwa wanatumia vitu vya thamani vilivyotolewa kwa ajili ya hekalu la Mungu kutukuza miungu ya kipagani. Pili na huenda ikawa inafanana nay a kwanza, usiku ule wangeweza kuchinjwa na Waajemi. Kwa taarifa yako, Waajemi waliitwaa Babeli lakini hawakuiangamiza mpaka miaka ya baadaye.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:1-5, je Mungu alitimiza ahadi au unabii gani kwa kuandika kwenye ukuta?
J: Kwenye Yer 27:21-22, Mungu alisema vyombo vitakatifu vitahifadhiwa Babeli, mpaka siku atakayovitembelea, kisha vitarudishwa Yerusalem. Hata hivyo, Wababeli hawakupata fursa kubwa sana ya kuvitumia, kabla ya maandishi ya ukutani kutokea.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:2, je vyombo vya kunywea vya dhahabu vilitoka wapi awali?
J: Sulemani alifanya dhahabu na fedha nyingi sana kwa ajili ya Hekalu la Bwana karibu mwaka 950 KK. Kitu cha kufurahisha kuhusu dhahabu ni kuwa hata kama ikufunikwa kwenye udongo haichuji. Hatujui endapo walichukua vyombo vya kunywea vya fedha kutoka hekluni, na fedha ilizuiliwa kuchuja, au endapo vyombo vya kunywea vya fedha havikutoka hekaluni. Kwa uapnde mwingine, ingawa Septuajinti, Vulgate, na Theodotion wanasema vyombo vya kunywea vya dhahabu na fedha, toleo le Kiarami linasema vyombo vya kunywea vya dhahabu tu.
SWALI: Kwenye Daniel 5:29b, je halikuwa jambo la kawaida kuwa na mtu wa tatu katika ufalme?
J: Hapana, maandishi ya Kiashuri na Kibabeli yanasema kuhusu kuwepo kwa mtu wa tatu katika ufalme. "Mtu wa tatu" anaweza kuwa kama waziri, au "meneja" chini ya mfalme na warithi wake. Kuwepo kwa watu wengi wenye uwezo wa kurithi kunaweza kuwa kwa salama zaidi inapotokea wafalme wawili wa juu wanakufa ghafla.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:10, kwa nini "malkia" anamtambulisha Danieli?
J: Belshaza hakufikira kufanya hivi, jambo ambalo linamaanisha kuwa hakuwa na ushirikiano na Danieli, na hakuuthamini ushauri wake. Wakati huu ni miaka 23 baada ya kifo cha Nebukadneza, kwa hiyo Danieli alikuwa na umri mkubwa sana sasa. Neno "maikia" hapa linaweza kuwa linamaanisha mama wa malkia, au pengine mke wa Nebukasneza, aliyemkumbuka Danieli na kumleta.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:25-28, je wageni waliweza kusoma maandishi ukutani?
J: Maneno manne yaliandikwa Kiarami, na Kiarami kilitumika sana Babelli na Uajemi, hivyo huenda watu wote waliokuwa wanajua kusoma waliweza kuyasoma maneno hayo. Hata hivyo, kulitambua fumbo hili kulikuwa hadithi nyingine.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:25-28, je Mene, Mene, Tekel, Upharsin inamaanisha nini?
J: Wanazuoni hawana uhakika wa maana ya maneno haya ya Kiarami. Kuna vitu vitatu vinavo wezekana, na kucheza na maneno kunaweza kuhusisha neno zaidi ya moja.
a) Ni maneno yanayoongelea fedha. Mina, shekeli, na nusu-mina zilikuwa sarafu zilizokuwa zinafahamika sana. Wycliffe Dictionary of Biblical Archaeology, uk.170 ina picha ya ‘mina’ moja ya wakati wa Nebukadneza.
b) Maneno haya yalimaanisha umehesabiwa, umepimwa, na umegawanyika.
c) "u" kwenye upharsin inaweza kumaanisha "na." Pharsin ni uwingi wa peres, ambayo inatamkwa karibu sawa na neno lao lenye kumaanisha Waajemi (Persian).
SWALI:
Kwenye Daniel 5:25-28, je maandishi ya ukutani yalimsaidiaje Danieli?
J: Watu wengi wangeweza kuelewa kwa uhakika kabisa kuwa Daniele alitabiri kuwa Waajemi wangewashinda Wababeli. Kitu cha kukisia ni kuwa endapo Waajemi wangesikia jambo hili wangefurahishwa sana na Danieli, na huenda wangependa kumwacha aendelee kuwa kiongozi wao wa ngazi ya juu.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:29, kwa nini Danieli alifanywa kuwa mtu wa tatu katika ufalme na si wa pili?
J: Belshaza hangeweza kumpa Danieli kitu chochote kikubwa zaidi, kama Nabonidus alikuwa kiongozi mkubwa zaidi, na Belshaza mwenyewe alikuwa wa pili.
SWALI :
Kwenye Daniel 5:30, orodha ya wafalme wa Babeli ni ipi?
J: Wana historia wanaiita himaya hii ‘Himaya Mpya ya Babeli’, ili kuitofautisha na himaya ya zamani iliyokuwa chini ya Hammurapi. Wafuatao ni waflme wake:
Mwaka 627-605 KK Nabopolasa (Nabu-apal- usur)
Mwaka 605-Aug/Sep 562 KK Nebukadneza II (Nabu-kudurri-usur)
Mwaka 562-560 KK Merodaki mwovu (Amel -Marduk) mtoto wa kiume wa Nebukadneza
Mwaka 560-556 KK Neriglissar (Nergal- Sharezer) mkwe wa Nebukadneza
Mwaka 556 KK (miezi 2) Labashi-Marduk
Mwaka 556-539 KK Nabonidus (Nabu-na’ia)
Mwaka 553-10/12/539 KK Belshaza (Bel-shar- usur) (msaidizi wa mtawala aliye badala ya mfalme [vice-regents] kwenye himaya
za kale za Umedi na Uajemi)
SWALI:
Kwenye Daniel 5:30-51 na 9:1, kuna tofauti gani kati ya Umedi na Uajemi?
J: Swali hili ni gumu kuliko linavyoonekana kwa mara ya kwanza. Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kulijibu.
1. Wamedi na Waajemi walikuwa jamii mbili tofauti lakini zilikuwa na uhusiano. Wamedi walihusiana kwa karibu zaidi na Wasinthia (walioishi ukanda wa zamani wa kusini mashariki mwa Ulaya na Asia) na waliishi Irani ya Kati, wakati Waajemi waliishi Elamu ya zamani kusini magharibi mwa Irani. Jamii hizi zilikuwa zinashirikiana kwa pamoja, huku Wamedi wakiwa washiriki wenye nguvu zaidi. Hali hii ilibadilika wakati wa utawala ya utawala wa Koreshi (Muajemi aliyekuwa na robo), wakati alipomshinda Astyges, babu yake Mmedi, mwaka 625 KK. Kuanzia wakati huo, Waajemi walikuwa na nguvu zaidi, na Herodotus 3.91-96 inasema Wamedi walitakiwa kuilipa Himaya ya Uajemi kodi ya mwaka.
2. Hata hivyo, Herodotus 1.135 pia inasema Waajemi waliyafanya mavazi ya Kiajemi kuwa yao. "Kama Widengren anavyosema, ‘Mara nyingi Wagiriki waliwaita Wamedi na Waajemi ‘Wamedi’, na ushahidi wa kuitwa hivi umeonekana wakati wa kukutana kwao na Wagiriki kwa mara ya kwanza huko Ionia na Wairani wa magharibi." Waajemi walijulikana kuwa Wamedi hadi kwenye enzi za Demosthenes, karne ya nne KK" (Persia and the Bible, uk.56-57).
3. Kwenye Biblia, walichukuliwa kuwa jamii moja, "Wamedi na Waajemi", kwenye Dan 6:8, 12, 15, na "Waajemi na Wamedi" kwenye Est 1:3, 14. Persia and the Bible, uk.57 pia inasema kuwa majina haya yaliitwa "Wamedi" tu kwenye Isa 13:17 na kuendelea na Yer 51:11, 28).
SWALI:
Kwenye Daniel 5:30-6:1 na 9:1 kwa ufupi sana, Dario Mmedi alikuwa ni nani?
J: Watu wengi wanafikiri alikuwa gavana wa kwanza wa Babeli, aliyeitwa Gubaru, ingawa wengine wanafikiri alikuwa ni Koreshi mwenyewe. Sababu ya kusema ni Dario ni ama:
a) kosa la kunakili wa hati yenye maandiko,
b) jina la kifalme la Koreshi, au
c) Wayahudi hawakuwa na tafsiri nzuri ya jina "Gubaru."
Angalia swali lifuatalo kwa jibu refu zaidi.
SWALI:
Kwenye Daniel 5:30-6:1 na 9:1 huyu Dario Mmedi alikuwa ni nani?
J: Kwanza kuna mambo kadhaa ya kihistoria, kisha ya kibiblia, na mwishoni maoni matatu.
1. Mambo ya Kihistoria
1.1 Historia ya Wamedi imetazamwa upya kutoka vyanzo vya Kiashuri, Kibabeli, Kiajemi na Kigiriki, kwani hakuna maandiko ya Kimedi ambayo yamegundulika. Mwana historia mwangalifu wa Kigiriki, Herodotus, alisema kuwa alisikia masimulizi manne tofauti ya maisha ya utotoni ya Koreshi. Ctesias alikuwa mwana historia mwingine wa Kigirik, lakini hakuwa anaaminika sana.
1.2 Mwaka 625 KK, Wamdei waliwashinda Waajemi na kuwatawala hadi mwaka 553 KK.
1.3 Kutoka mwaka 553 hadi 550 KK, Muajemo Koreshi Mkuu aliasi na kufanikiwa kwa msaada wa Harpagus, chifu wa Kimedi (mwaka 550 KK). Wamedi bado walikuwa na nafasi ya juu zaidi baada ya Waajemi, na kama matoleo ya mwaka 1956 na 1972 ya Encyclopedia Britannica yanavyosema, "Wamedi wengi maarufu waliajiriwa kama viongozi, maliwali, na majemedari."
1.4 Astyages (Kwa Kimedi, Ištumegu) alikuwa mfalme wa Kimedi aliyepinduliwa na Koreshi mwaka 550 KK. Mwana historia Ctesias anasema kuwa Koreshi alikuwa mwema kwa Astyages, na alimfanya kuwa liwali wa Barcania au Hyrcania, lakini Oebares (kwa Kibabeli Ugbaru) alimuua Astyages.
1.5 Kwenye Himaya ya Kiajemi, Medi lilikuwa moja ya majimbo 20 ya Himaya ya Uajemi yaliyokuwa yanaongozwa na maliwali, lakini liligawanyika sehemu mbili kwa sababu za kodi. Kama wazo la ziada, majimbo haya 20 yaligawanywa kwenye wilaya 120, ambazo wakati mwingine nazo ziliitwa majimbo (satrapies), bali kwa kweli zilikuwa hyparchs.
1.6 Ugbaru, gavana wa Kibabeli wa Gutium (kwa mujibu wa orodha ya matukio ya Nabonidus), alihamia upande wa Waajemi na kuwa jenerali wa jeshi la Uajemi liliiangusha Babeli tarehe 11 au 12 Okt mwaka 539 KK. Alikufa 6/11/539 KK, karibu mwezi mmoja baadaye. Ingawa hatujui ukoo wake, kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 2, uk.39 kinasema kuwa Wababeli walitumia neno Gutium kumaanisha Kaskazini mashariki, na Wamedi waliishi sehemu ya kaskazini mashariki ya Himaya ya Babeli. Pia kinasema kuwa mwana historia Berossus alimworodhesha Gutium pamoja na watawal makatili wa Wamedi.
1.7 Koreshi mwenyewe alikuwa na vikosi vingine huko Opis wakati Babeli ilipotekwa, na Koreshi hakuingia Babeli hadi 29/10/539 KK. Koreshi alisemekana kuwa mjukuu wa Astyages, kupitia binti wa Astyages aliyeitwa Mandane. Hata hivyo, the Wycliffe Bible Dictionary, uk.424 inaonyesha kuwa huyu hakuwa Mfalme wa Uajemi, kwa sababu Dario hapa inamaanisha "alifanywa mfalme." Danieli naye aliitwa "mfalme" kwenye Dan 5:29, na hakuwa mfalme.
1.8 Gubaru/Gaubaruwa (ambaye Mgiriki Xenophon alimchanganya na Ugbaru), alichaguliwa na Koreshi kuwa gavana wa Babeli kwa mwaka mmoja au miwili.
1.9 Dario I, mtoto wa kiume wa Hystaspes/Vishtaspa, alikuwa Muajemi (siyo Mmedi) aliyekuwa mfalme mwaka 522 KK, baada ya Koreshi na Bardiya wa uongo kutawala. Dario I alihusika na kuzimisha uasi huko Babeli mwaka 520 KK, miaka 19 baada ya Uajemi kuishinda Babeli. Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.287 inaonyesha kuwa alikuwa na miaka ishirini na alipoanza kutawala, si miaka 62. Kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 2, uk.39 inasema kuwa maandishi yake yanasema "Mimi ni Muajemi, mtoto wa kiume wa Muajemi."
1.10 Kwenye ulimwengu wa kale, wafalme wa Misri na sehemu nyingine walikuwa na majina waliyopewa wakati wa kuzaliwa, na jina la pili lilitolewa wakati wa kuanza kutawala.
1.11 Neno la Kiajemi Dario "Darayawush/Dareyawaes" linahusiana na neno la Kiajemi dara linalomaanisha mfalme. Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.288 inasema hikli linaweza kuwa ni cheo na jina la mtu. Kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, uk.39 pia inasema kuwa darayarahu inamaanisha "Yeye ashikiliaye mema." Hii ndiyo sababu ya nadharia kuwa Dario lilikuwa ni jina la cheo.
1.12 Mwaka huo huo au miwili wa kuteka, Koreshi almfanya mtoto wake wa kiume Cambyses kuwa gavana wa Babeli, akichukua nafasi ya Gubaru.
1.13 Kwenye Agano la Kale kuna makosa kadhaa ya kunakili, hasa kwenye namba na majina. Kwa mfano, toleo la Kigiriki la Proto-Theodotion linasema "Artashasta (Artaxerxes)", na si "Dario" kwenye Dan 6:1. Kuna nyongeza kadhaa kwenye tafsiri ya Kigiriki (Septuajinti) kwenye Kitabu cha Danieli. Jerome anasema kuwa ingawa kanisa la awali lilitumia Septuajinti, hawakutumia Septuajinti ya Kitabu cha Danieli, lakini toleo la Kigiriki la Theodotion. Inaelekea waliona makosa mengi sana kwenye Septuajinti ya Danieli.
1.14 Nakala zetu zote za "Kiebrania" za Danieli zina zina sehemu ya kati ya Danieli, 2:4b-7:28, iliyoandikwa kwa Kiarami, si Kiebrania. Huenda iliandikwa Kiarami toka mwanzoni, au ilitafsiriwa kutoka kwenye hati yenye maandiko ya kale ya Kiebrania.
2. Mambo ya Kibiblia
Dario wa kwenye Kitabu cha Danieli alikuwa Mmedi, mwenye miaka 62, aliyekuwa na wilaya/majimbo 120 ya utawala chini yake. Alikuwa mtoto wa Ahasuero. Alikuwa na uwezo wa kutoa amri, na aliabudiwa. Kwenye Dan 6:6, aliitwa mfalme. Kutoka Dan 9:1, huyu Dario, alisistiziwa kuwa Mmedi, siyo Dario Muajemi. Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.287 inasema kuwa kitenzi cha kawaida malak kinamaanisha fanyika kuwa mfalme, lakini kitenzi homlak hapa, ambacho ni kitendewa na kinamaanisha kufanywa mfalme. Kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 2, uk.39 pia inaonyesha jambo hili. Hivyo, mtawala mwenye mwenye mamlaka makubwa zaidi amemfanya kiongozi. Pia, maneno "dunia yote" yanaweza kutafsiriwa kuwa "nchi yate."
3. Dario Mmedi ni nani hasa
Kwa kuwa Dario ndiye aliyeiteka Babeli, kuna mambo matatu yanayowezekana:
3.1 Koreshi: Huyu alikuwa Koreshi hasa, na jina lisilokuwa sahihi liliandikwa, sawa na jinsi jina Yehoakimu lilivyoandikwa kimakosa kwenye Yer 27:1 kwenye nyingi ya hati zenye maandiko za Kiebrania wakati mandhari na hati zenye maandiko ya kazi za kale vinaonyesha kuwa ilikuwa Zedekiya. Ingawa Koreshi alikuwa Muajemi, mama yake, Mandane, alikuwa Mmedi na binti ya Astyages, na chifu wa Kiajemi Cambyses. Huenda ni kweli kuwa alikuwa robo Mmedi na mjukuu wa mfalme wa zamani, au alidai kuwa hivyo ili aungwe mkono na Wamedi.
3.1.1 Kwa kuwa wafalme wengi walikuwa na majina ya vyeo, Koreshi anaweza kuwa alikuwa na jina la cheo la Dario Mmedi. Dan 6:28 inaweza kutafsiriwa kuwa "utawala wa Dario, ‘hata’ utawala wa Koreshi Mmedi." Maoni haya yanaungwa mkono na D.J. Wiseman, na John F. Walvoord anasifia maoni haya kwenye Daniel: The Key to Prophetic Interpretation, uk.134. The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1347 pia inasema kuhusu maon haya lakini inapendelea maoni yanayofuata kuhusu Gubaru. Mifano mingine ya majina yanayofanana au majina ya vyeo yaliyotumiwa kwenye Biblia ni:
Yoramu kwa Yehoramu (2 Fal 8:23)
Yehoashi kwa Yoashi (2 Fal 12:1)
Koniya kwa Yekoniya (Yer 22:28)
Shalumu kwa Yehoahazi (Yer 22:11, 2 Fal 23:30-34)
3.1.2 Koreshi hakuwa na jina la cheo Dario. Jina Dario limekuja hapa kama kosa la kunakili, likichanganya Koreshi kuishinda Babeli mwaka 539 KK na Koreshi kuishinda Babeli mwaka 522 KK.
3.2 Gubaru ametajwa hapa, kwa kuwa Koreshi alimteua kuwa gavana wa Babeli, kama When Critics Ask, uk.295 inavyoafiki. Hata hivyo, hatuna rekodi ya kihistoria inayosema ama Gubaru alikuwa Mmedi au la. Ama Dario ni namna Waebrania walivyomwita Gubaru, au mwandishi wa Kiebrania aliyekuwa amechanganyikiwa aliandika jina Dario. Ingawa jina Gubaru lilichukuliwa nafasi yake na jina Cambyses baadaa ya mwaka mmoja au miwili, Kitabu cha Danieli hakisemi kitu chochote baada ya mwaka wa kwanza. Magavana walikuwa wakiitwa "wafalme", kwa sababu Maandishi ya Behistuni yanasema kuwa Hystaspes "alifanywa mfalme" na Koreshi, kama Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.287-288 inavyosema.
3.3 (si jibu) Dario hapa watu wengine wanaweza kufikiri kuwa ni Dario I (Muajemi) wa kweli, na patakuwa na pengo la mika 19 kati wa kupinduliwa kwa Wababeli kwenye Dan 5:30, na Dario aliyeelezwa mwishoni. Hata hivyo, jambo halielekei kuwa hivyo kwa sababu kitabu hiki kinasema bayana kuwa Dario huyu alikuwa Mmedi. Isitoshe, hakuna aya ya Biblia inayosema kuwa Dario huyu alikuwa juu wa Wamedi na Waajemi wote, bali alifanywa mfalme kwa Wababeli tu.
Muhtasari: Kwa kuwa maoni ya tatu hayana uwezekano wa kuwa kweli, mtu aliyekusudiwa hapa ni ama:
SWALI LA 1. Gubaru, gavana wa kwanza wa Babeli chini ya utawala wa Koreshi, au
SWALI LA 2. Koreshi. Ama Dario lilikuwa ni jina la cheo la Koreshi, ama waandishi walifanya makosa katika hati zao za maandiko, wakati ilitakiwa iandikwe Koreshi.
Makosa ya kunakili na mabadiliko si vitu vigeni kwenye Agano la Kale, na Septuajinti ya Kitabu cha Danieli ina mabadiliko kadhaa yanayofahamika.
SWALI: Kwenye Dan 5:31, je Babeli ilitekwa lini?
J: Wataalamu wa mambo ya kale wanaamini kuwa ilikuwa usiku wa Oktoba 11 au 12, 539 KK. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa Babeli haikubomolewa mpaka baada ya miaka kupita.
SWALI:
Kwenye Daniels 5:31; 6:1 na 9:1, jina "Dario" linatamkwaje?
J: Cruden’s Concordance na The New International Dictionary of the Bible, uk.254 zina da-RI-us, yenye ‘a’ na ‘u’ fupi, ‘i’ ndefu, na kiinitoni kwenye silabi ya pili. Waebrania walilitamka daryawesh, na Wagiriki walilitamka Darious. Wamedi na Waajemi walilitamka jina la Dario sawa na "Darayawush / Dareyawaes."
USIKOSE SEHEMU YA KUMI ...Kwenye Daniel 6:1, nani walikuwa maliwali 120?
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW