Daniel 6
Kisa cha Daniel ni fundisho kwa hao watakaoitwa kumtetea Mungu siku za Mwisho.Danieli alichaguliwa kuwa Mmoja wa Viongozi wakubwa aliye Juu ya maliwali wa Mfalme,na Mfalme alimpenda sababu alikuwa Mwaminifu.Biblia yasema,’’Basi Danieli Huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali,kwa kuwa Roho Bora ilikuwa ndani yake;naye Mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote[DAN6:3].
Kisa cha Daniel ni fundisho kwa hao watakaoitwa kumtetea Mungu siku za Mwisho.Danieli alichaguliwa kuwa Mmoja wa Viongozi wakubwa aliye Juu ya maliwali wa Mfalme,na Mfalme alimpenda sababu alikuwa Mwaminifu.Biblia yasema,’’Basi Danieli Huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali,kwa kuwa Roho Bora ilikuwa ndani yake;naye Mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote[DAN6:3].
Lakini mawaziri na Maamiri walimuonea wivu.Maadui hawa wa Daniel walitafuta kosa lilote ili wapate kumshitaki Daniel lakini walikosa.Biblia yasema,’’Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Daniel kwa habari za Mambo ya ufalme,lakini hawakuweza kuona sababu,wala kosa;kwa maana alikuwa mwaminifu,wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake[Danile6:4].
Ndipo Hao maadui wa Daniel wakashauriana kutafuta Sababu kuhusiana na Mambo yake ya kumwabudu Mungu,ili wapate kumshitaki.Biblia yasema,’’Ndipo wale watu wakasema,Hatutapata sababu ya kumshitaki Daniel Huyo,tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake[Daniel 6:5].Ndipo wale viongozi wanaomchukia danieli wakakusanyana pamoja na kumwendea Mfalme na kumshawishi Mfalme ili Atie sahihi na kuidhinisha agizo kwamba Mtu yeyote asimwabidu Mungu yeyoye ama mtu yeyote isipokuwa Mfalme kwa mda wa siku thelathini.
Iliazimiwa kuwa Atakayekiuka Agizo hilo alitupwa katika tundu la Simba.Licha ya Agizo hilo ambalo lilitungwa makusudi ili Kutia hatiani Daniel,Danieli alibaki kuwa Mwaminifu katika Kumwomba Mungu wake kama ilivyo desturi yake,wala Hakuogopa Agizo hilo lenye sahihi ya Mfalme.Wale Maadui walipoona kuwa Danieli amekwenda kinyume na Agizo lao wakaenda kumshitaki Daniel kwa Mfalme kuwa amekiuka maagizo ya mfalme.Mfalme aligundua Hila yao na kuchukia sana ila Sababu sheria ya wamedi na waajemi ilikuwa haibadiliki,Aliazimu kuagiza kuwa Daniel Atupwe katika Tundu la Simba.
Siku inayofuata Mfalme alikwenda kuchungulia mle tunduni ili kuona kama Mungu wa Daniel Atamuokoa Daniel kwani Mfalme alimpenda Daniel.Kweli Mungu alimuokoa Daniel,wala Simba hawakumla.Biblia yasema,’’Mungu wangu amemtuma Malaika wake naye ameyafumba Makanwa ya Simba nao hawakunidhuru kwa kuwa Mbele zake Mimi nalionekana kuwa sina Hatia,wala Mbele zako ee mfalme Sikukosa neno[Daniel 6:22].
Pambano litakalowajia Watu wa Mungu katika siku za Mwisho litakuwa pia ni juu ya Ibada ya kweli dhidi ya ile ya Uongo na baina ya Amri za Mungu na Sheria za kibinadamu. Katika Siku za Mwisho zijazo Watu wa Mungu watajazwa roho Mtakatifu,na Mungu ataonyesha wazi kuwa Amewatia Mafuta na Kuwabariki kuliko watu wowote wale Duniani. Mamilioni ya watu wataisikia injili na kuwafuata watu wa Mungu.Hili litachochea wivu kwa viongozi na wachungaji wa mshahara,nao watafanya Shauri pamoja la kuwazimisha hao watu wa Mungu.
Viongozi hao watatafuta Msaada wa Serikali na Sheria za kibinadamu ambazo zinakinzana kabisa na Sheria za Mungu zitatungwa kwamba watu wote wakubwa kwa wadogo walazimishwe kuzishika. Hasa hasa Mtihani Mkubwa utakaowajia watu wa Mungu ni juu ya siku ya Kuabudu. Sabato ya Uongo yaani Jumapili itatukuzwa na serikali za kidunia, na Sabato ya Ukweli, itapingwa na kukataliwa. Wale watu wa Mungu wote watakaoishi katika siku za Mwisho sharti wawe waaminifu kwa Kuitetea Sabato ya Kweli hata ikibidi kufa kwa ajili ya ukweli.
Lakini Mungu aliyemwokoa Daniel Atakuwa na watu wake mnamo siku za Mwisho,naye atawaokoa. Watu wa Mungu watafukuzwa mijini na kukimbilia vijijini. Wengine watanyang'anywa makazi yao na kukimbilia kwenye mapango na kwenye majabali. Wengine watafungwa katika vifungo vya giza na vya mateso. Lakini Mungu anatoa ahadi hii kwa watu wa Mungu;'-Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma. [Isaya33:16].Ole wao watakaomwabudu Mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake. Lakini heri wale wenye subira ya watakatifu yaani hao wazishikao Amri za Mungu na Imani ya Yesu [Ufunuo14:12]
SWALI:
Kwenye Daniel 6:1-5, kwa nini maliwali walikusudia kumtia Danieli matatizoni?
Kwenye Daniel 6:1-5, kwa nini maliwali walikusudia kumtia Danieli matatizoni?
J: Huenda ni kwa sababu mbili:
Wivu: Danieli alikuwa mgeni, Myahudi, aliyepandishwa cheo mara moja na kuwa juu yao.
Wivu: Danieli alikuwa mgeni, Myahudi, aliyepandishwa cheo mara moja na kuwa juu yao.
Kutokuwa na upendo: Hata kama hawakuwa na chuki au hisia mbaya dhidi ya Danieli, baadhi ya watu wasiokuwa waadilifu huwa hawaogopi kuwaondoa wandani wao ili kuweza kuendelea na mambo wanayoyafanya.
Kwa hiyo kitu cha kwanza walichokifanya ni kufanya uchunguzi wenye matumaini ya kupata habari. Kwa kuwa wengi wa viongozi hawakuwa waadilifu, walichunguza ili kufahamu uozo wa Danieli ili wautangaze. Huenda walifikiri kuwa kuutangaza uozo au uzemba wa Danieli watakavyochagua kutangaza ndilo jambo pekee walilotakiwa kulifanya. Hata hivyo, mawazo haya hayakuwa ya viongozi wote. Walipokuja kufahamu bila kutarajia kuwa hawakuona kitu chochote kibaya, kwenye mstari wa tano walitafuta ‘mpango mbadala’, na kuangalia kitu kinachohusiana na sheria ya Mungu. Si kila mtu anayesoma neno la Mungu anakuwa amesukumwa na nia njema.
SWALI:
Kwenye Dan 6:6-9, je waliwezaje kuwafanya viongozi kwenye himaya yote kukubaliana na mpango huu?
Kwenye Dan 6:6-9, je waliwezaje kuwafanya viongozi kwenye himaya yote kukubaliana na mpango huu?
J: Hawakuweza. Huenda walitegemea kuwa viongozi wengine watakubaliana na mpango huu bila kupinga. Kumbuka kuwa endapo kiongozi mpagani wa kawaida alikubali kupendekeza amri hii, asingeweza kujua kuwa lengo la mpango huu lilikuwa kumtega Danieli na huenda na Wayahudi wengine. Vinginevyo, wanaweza kuwa hawakuwahi kubaliana kabisa na walijua kuwa hawakuwasilisha ukweli kuwa walikuwa na uwezo wa kufikia makubaliano. Pia kumbuka kuwa walimdanganya Dario waliposema kuwa viongozi "wote" wamekubaliana. Danieli hakuwa amekubaliana na jambo hilo.
SWALI:
Kwenye Dan 6:6-9, kwa nini Dario alitoa amri hii kuwa mtu yeyote asiombe kwa mungu au mtu yeyote yule kwa muda wa siku thelathini?
Kwenye Dan 6:6-9, kwa nini Dario alitoa amri hii kuwa mtu yeyote asiombe kwa mungu au mtu yeyote yule kwa muda wa siku thelathini?
J: Ingawa Maandiko hayasemi, tunaweza kukisia sababu kadhaa:
Kupitisha uamuzi bila kuuzingatia: Dario aliambiwa (huenda kwa uongo) kuwa maliwali wengine wote walikubaliana na wazo hili. (Kwa hakika hawakukubali wote, kwani Danieli hakuwa amefanya hivyo). Kwa kuwa Dario aliwaamini watu wake, alisaini tu kitu walichosema.
Kupitisha uamuzi bila kuuzingatia: Dario aliambiwa (huenda kwa uongo) kuwa maliwali wengine wote walikubaliana na wazo hili. (Kwa hakika hawakukubali wote, kwani Danieli hakuwa amefanya hivyo). Kwa kuwa Dario aliwaamini watu wake, alisaini tu kitu walichosema.
Mshikamano wa himaya: Kundi kubwa na lenye nguvu la watu waliokuwa wanatawaliwa na serikali ya kigeni, Wababeli, mpaka wakati karibu na huo walikuwa huru na wanapigana kwa ajili ya Himaya ya Uajemi. Jambo hili lingetia mkazo kwa Wababeli na watawaliwa wa zamani wa Himaya ya Babeli kuwa hawako chini ya Wababeli tena bali sasa wako chini ya Waajemi. Kwa hiyo walitakiwa kuacha kumwabudu Marduku, au miungu mingine ya Babeli kwa siku thelathini, kwa sababu Waajemi walichukuliwa kuwa wakuu kwani waliweza kutoa amri ya kusitisha ibada kwa miungu mingine. Watu ambao wangekataa wangetambuliwa kuwa waasi na kushughulikiwa ipasavyo.
Majivuno yasiyo na maana: Dario angeheshimiwa, si tu kwamba watu walikuwa wanamwabudu na kumwomba, lakini hawangekuwa wanamwomba mungu au mtu mwingine yeyote yule kwa siku thelathini.
SWALI:
Kwenye Dan 6:6-9, kuna ushahidi wowote wa elimukale wa amri hii ya siku thelathini?
Kwenye Dan 6:6-9, kuna ushahidi wowote wa elimukale wa amri hii ya siku thelathini?
J: Hapana, lakini hili ni jambo ambalo Mfalme Dario hangependa likumbukwe.
SWALI: In Dan 6:10, should we always kneel or do another posture when praying?
J: Ndiyo na Hapana. Hapana, Biblia haituamuru kutumia mkao wowote maalumu tunaposali. Wakati mwingine watu waliomba:
Huku wakipiga magoti (Ezra 9:5-6; Daniel 6:10; Luka 22:41; Matendo 7:59-60; Efeso 3:14)
Huku wakipiga magoti (Ezra 9:5-6; Daniel 6:10; Luka 22:41; Matendo 7:59-60; Efeso 3:14)
Kuanguka kifudifudi (Mwanzo 17:17, 18; Yos 6:7-9; Matayo 26:39)
Kupiga magoti au kuanguka kifudifudi (Marko 14:35)
Kusimama wima (Mwanzo 18:22-23; 24:11-13; Nehemia 9:4-5)
Kukaa (2 Sam 7:18; 1 Fal 19:4)
Kulala kitandani (2 Fal 20:2)
Bila kuweza kubadilisha mkao (Amos 16:28; Nehemia 2:3-4; Yon 2:1; Matayo 27:46; Marko 15:34; Luke 23:46).
Kupiga magoti au kuanguka kifudifudi (Marko 14:35)
Kusimama wima (Mwanzo 18:22-23; 24:11-13; Nehemia 9:4-5)
Kukaa (2 Sam 7:18; 1 Fal 19:4)
Kulala kitandani (2 Fal 20:2)
Bila kuweza kubadilisha mkao (Amos 16:28; Nehemia 2:3-4; Yon 2:1; Matayo 27:46; Marko 15:34; Luke 23:46).
Hata hivyo, tuna uhuru wa kutumia mkao wowote utakaoyafaa maombi tuombayo.
SWALI:
Kwenye Daniel 6:10, je ni vizuri kuwa na muda maalumu wa kuomba?
Kwenye Daniel 6:10, je ni vizuri kuwa na muda maalumu wa kuomba?
J: Ndiyo. Ingawa Biblia haisemi tusali wakati fulani, waamini wengi wameona kuwa inasaidia zaidi kuwa na wakati maalumu wa kusali. Maombi ya mara kwa mara yanahitaji nidhamu, na kuwa na wakati maalumu wa kusali kunasaidia kufikia lengo hili.
SWALI: Kwenye Daniel 6:10, je tunapaswa kuelekea Yerusalemu wakati tunasali? Je Mungu anayasikia vizuri maombi tuyafanyayo tukiwa tumeelekea upande fulani?
J: Kwenye nyakati za Agano Jipya upande tunaoelekea wakati wa kusali hauna umuhimu wowote. Kwenye nyakati za Agano la Kale hakuna amri ya kuelekea Yerusalemu, au kuelekea kwenye hekalu wakati wa kusali, lakini Danieli alikuwa anafikiria maombi ya Sulemani ambapo alimwomba Mungu kuwasikiliza watu watakaomwomba kuelekea hekalu na kuelekea Yerusalemu kwenye 1 Fal 8:29, 42, 44, 48. Mungu alizungumza na kujibu ombi la Sulemani kwenye 1 Fal 9:3-9 kwa njia chanya na inayotia moyo, lakini Mungu hakusema kitu chochote kuhusu kusikia maombi vizuri zaidi ikiwa mwombaji ataelekea upande wowote ule. Mungu alisema kuwa ingawa hekalu lilikuwa zuri na lenye kuvutia, siku inakuja ambapo watatishwa na uwanja wa hekalu.
SWALI: Kwenye Daniel 6:10-11, je unaweza kufanya nini ikiwa unapenda kumcha Mungu kwa kufanya kitu fulani, ikiwa kuendelea kufanya hivyo kutaleta hasara kifedha, aibu, au hata kitu kingine kibaya zaidi?
J: Ningejaribu kuona endapo kuna njia ya kuendelea kufanya kitu hicho na kutokupata hasara. Hata hivyo, si tu kwamba Wakristo wasiwe waovu, bali pia waepushe kitu chochote chenye mwonekano wa uovu. Katika nyakati za kanisa la awali, Wakristo waliamriwa kutoa kafara kwa mfalme kama kwa Mungu. Wakristo wengi walichagua mateso na kifo kuliko kuabudu sanamu. Lakini wengine walikuwa wanyonge na walifanya dhambi kwa kutoa kafara. Ikiwa mtu alitoa rushwa ili kwamba asitoe kafara lakini alimhonga kiongozi wa umma aliyesema kuwa ametoa kafara, bado hangekuwa anamcha Mungu kwa sababu ya kuwa na mwonekano wa kufanya dhambi ya kutoa kafara.
SWALI:
Kwenye Daniel 6:10-11, je Danieli alinunua mapazia? Kwa kutumia sitiari, ni wakati gani tunatakiwa kununua mapazia leo hii? Na vipi kuhusu kusali sirini?
Kwenye Daniel 6:10-11, je Danieli alinunua mapazia? Kwa kutumia sitiari, ni wakati gani tunatakiwa kununua mapazia leo hii? Na vipi kuhusu kusali sirini?
J: Kusali sirini, mbali na watu wasio amini ni kitu kizuri, lakini Yesu alituagiza kusali sirini kwenye Agano Jipya (Mat 6:5-8) si Agano la Kale, na Agano Jipya lilikuwa bado halijatolewa wakati ule. Mapazia yasingeweza kusaidia kitu, kwa sababu watu wale waliishajua kuwa aliomba, na wangekuja kumwona, kama walivyofanya kwenye Dan 6:11.
SWALI:
Kwenye Daniel 6:12, je simba hawa walifanana na kitu gani?
Kwenye Daniel 6:12, je simba hawa walifanana na kitu gani?
J: Simba walikuwa wanazunguka Mashariki ya kati hadi watu walipowawinda na kuwamaliza. Watu wengi, hasa Waashuri na Waajemi, walipenda kuwawinda. Samsoni alimuua simba Israeli kwenye Amu 14:5. Makala yenye kufurahisha sana yenye kichea ‘Simba wa Mwisho wa Asia’ kwenye The National Geographic Magazine (Juni 2001), uk.46-61. Simba wa Asia walikuwa wadogo kiasi kuliko simba wa Afrika, walikuwa na manyoya mafupi, na walikuwa na fundo la ngozi kwenye pande zao za chini ambazo simba wa Afrika hawana. Eneo lao lilikuwa kuanzia kaskazini mwa India kupitia Iraki, hadi Ugiriki, Bulgaria na Albania.
SWALI:
Kwenye Daniel 6:14, kwa nini Biblia inasema Dario alijaribu kumuokoa Danieli kwani kwenye Dan 6:16 mfalme aliamuru Danieli atupwe kwenye simbo la simba?
Kwenye Daniel 6:14, kwa nini Biblia inasema Dario alijaribu kumuokoa Danieli kwani kwenye Dan 6:16 mfalme aliamuru Danieli atupwe kwenye simbo la simba?
J: Kwa sababu aya zote zilikuwa sahihi. Huyu alikuwa mtu mwenye nguvu asiyeamini, ambaye anaweza kuwa alifikiri kuwa ni kiongozi mzuri na mwenye haki, ambaye kwa ujumla alipenda kumsaidia Danieli, lakini utiifu wake kwa mila ulikuwa mkubwa kuliko utiifu wake kwa mambo ya haki. Leo hii kuna watu wengi ambao mara nyingi hupenda kufanya mambo ya haki, lakini mila zao au mambo yaliyotangulia ndio kipimo chao kikuu, na cha muhimu zaidi kuliko dhamiri zao za kumfuata Mungu.
SWALI:
Kwenye Daniel 6:24, je hakikuwa kitendo cha ukatili kuwatupa kwenye shimo la simba wake na watoto wa watu waliokuwa wamemshtaki Danieli?
Kwenye Daniel 6:24, je hakikuwa kitendo cha ukatili kuwatupa kwenye shimo la simba wake na watoto wa watu waliokuwa wamemshtaki Danieli?
J: Biblia haisemi kuwa Wababeli hawakuwahi kuwa wakatili, au kuwa walifanya vitu sahihi kila wakati. Lakini ikilinganishwa na Waashuri waliokuwa wanajisifu kwa kutesa watu, Waajemi walikuwa wapole.
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MOJA...Kwenye DanIEL 7:2, je pepo za mbinguni zinawakilisha kitu gani? Kwa nini kuna pepo nne?
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo
No comments:
Post a Comment