Sunday, December 4, 2016

FAHAMU KUHUSU UCHAWI, BUNDUKI, NA MISHALE YA KICHAWI (SEHEMU YA KWANZA)




Ndugu msomaji wangu,
Kumekuwa na matukio mengi sana ya kichawi hapa duniani, na ni bora tuwafahamu hawa wachawi na jinsi ya kujikinga nao. Kwa kifupi njia pekee ya kujikinga na uchawi ni NJIA YA YESU.
NINI MAANA YA UCHAWI?
Kwanza tujifunze maana ya neno “UCHAWI” na tafsiri zake tofauti tofauti kutoka wanachuo mbali mbali:
Al Azhari ambaye ni mtungaji wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo “Lisanul Arab” amesema:
“Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shetani na kwa msaada wake (shetani)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”

Ama Sahaba Ibni Abbas (Radhiya Llaahu ‘anhu) amesema:
"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."
Hayo ni katika kamusi za lugha.
Amma katika kamusi ya dini ya Kiislam, maana ya neno Uchawi (As Sihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhruddin Al Razi kuwa;
"Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa (khidaa)."
Amma Sheikh Wahiyd Abdulsalaam Bali, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho 'Al Saarim Al Batar fiy muhaarabat Al Saharatul ashraar', na kitabu kiitwacho "Al wiqaya mina l jinni wa shaytan", ambaye pia ni mtaalamu maarufu katika elimu ya majini na mashetani na uchawi na ambaye pia ni katika maulamaa maarufu wanaotoa majini kwa njia ya kusoma Qur-aan, yeye anasema:
"Uchawi ni makubaliano baina ya mchawi na Jinni akishurutishwa mchawi kufanya mambo ya haramu au ya shirki, na baada ya kufanya hayo, Jinni anashurutishwa kumsaidia na kumtii mchawi huyo kwa kila anachotaka."
Maana ya uchawi kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili:
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, toleo la 3, neno ‘uchawi’ limefafanuliwa katika sehemu kuu mbili zifuatazo, Kwanza ni ‘ufundi wa kutumia dawa au vitabu maalum vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe; au juju. Pili ni ‘vifaa vinavyotumika katika shughuli za kurogea’
Neno “mchawi’ limetafsiriwa kuwa ni mtu anayesadikiwa kuwa anaweza kuwadhuhuru watu kwa kuwaroga; mlozi, kahini. Wachawi mara nyingi hufanya kazi katika ulimwengu wa roho yaani ulimwengu ambao huwezi kuuona kwa macho ya kimwili.

Kwa mujibu wa Merriam-Webster dictionary neno “witchcraft” ambalo katika Kiswahili hutafsiriwa kama “uchawi” limetafsiriwa kama “magical things that are done by witches, or the use of magical powers obtained especially from evil spirits” kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili “uchawi” maana yake mambo ya kimiujiza yanayofanywa na wachawi”, maana ya pili, “matumizi ya nguvu za kiroho zilizochukuliwa toka kwa roho waovu”. Wengine wanatafsiri uchawi kama matumizi ya silaha za mashetani au nguvu za mashetani ili kusababisha madhara kwa watu.
Iyke Nathan Uzorma, Katika Kitabu chake kinachoitwa “Mkuu Wa Wachawi Sasa Ampokea Kristo” anaandika hivi; mchawi ni mwanadamu ambaye hupitia vitengo mbali mbali katika ufalme wa giza, ili atumiwe kuzidhihirisha nguvu zisizoonekana za Shetani katika Ulimwengu wa mwili. Kwa lugha nyingine mwanadamu yeyote ambaye hutumia nguvu au maarifa yasiyoonekana kudhuru, kuharibu, kudhibiti, kumiliki, au kupumbaza akili za mwanadamu mwenzake huyo ni mchawi.
UCHAWI UNAFANYWAJE?
Baadhi ya yale ambayo mchawi anatakiwa na shetani ayatende ili ajikurubishe naye ni:
• Mchawi anatakiwa auvae MSAHAFU miguuni na aingie nao chooni
• Aandike baadhi ya aya za Qur-aan kwa damu ya hedhi.
• Miongoni mwao wanashurutishwa kuandika aya za Qur-aan penye nyayo za miguu.
• Au aiandike suratul Fatiha kinyume nyume.
• Asali bila ya Udhuu.
• Wengine hutakiwa kuchinja mnyama huku wakilitaja jina la Allah kisha amtupe mnyama huyo mahali maalum anapoamrishwa na shetani.
• Wamo miongoni mwao wanaozungumza na nyota au kuzisujudia, kama Marehemu Shehe Yahaya.
• Au hutakiwa kuandika herizi “HIRIZI” kwa maneno yenye aya za Qur-aan ndani yake. Maneno haya lazima yaandikwe Kiarabu.
VIPI UTAWEZA KUMJUA MCHAWI?
Zifuatazo ni dalili zitazokuwezesha kumfahamu mchawi. Utakapoona mojawapo ya dalili zufuatazo utambuwe kuwa huyo ni mchawi bila shaka yeyote na ni labda shekhe au mganga:-
• Mchawi huuliza jina la mgonjwa na jina la mama yake
• Huchukua baadhi ya vitu vya mgonjwa kama vile nguo za nje au za ndani au kitambaa cha kufutia jasho n.k.
• Hutaka mnyama mwenye sifa maalum au rangi maalum ili achinjwe na hupigiwa Bismillahi anapochinjwa
• Huandika hirizi kwa aya za Quran.
• Husema maneno ya Kiarabu yasiyojulikana
• Humtaka mgonjwa aepukane na watu muda maalum na akae katika chumba kisichofikiwa na juwa
• Mara nyengine humtaka mgonjwa asiguse maji muda wa siku arubaini hivi (anasema Sheikh Wahiyd Abdulsalaam Bali kwamba akikutaka ufanye hivyo ujue kwamba Jinni anayemtumikia mchawi huyo ni Muislam)
• Humpa mgonjwa vitu ili avifukie ardhini
• Humpa mgonjwa karatasi aziunguze kisha ajifukize na moshi wake
• Mara nyengine humwambia mgonjwa jina lake na mji anaoishi
• Huandika maneno ya Kiarabu “Quruani” katika karatasi na kumwambia mgonjwa azichemshe na kunywa maji yake
JINSI WACHAWI WANAVYO FANYA KAZI:
Wachawi wanapo taka kumuadhibu adui yao wana njia nyingi sana za kufanya hivyo. Wao wana kauli mbiu yao moja wanasema “KUNA NJIA NYINGI ZA KUMUUA PANYA”.
HUTUMIA JINA LAKO:
Jina la mtu anaye takiwa kupewa adhabu ya kichawi linapo fika katika meza ya madhabahu husika, mambo kadhaa hufanyika kama vile, kujua jina kamili la mtu huyo pamoja na jina la mama yake mzazi, kama jina la mama yake mzazi halitapatikana , basi watatumia hata jina la baba yake, na kama jina la baba yake, halitapatikana pia, watatumia jina la ADAM kama jina la ubini. Majina haya hutumika katika kutafuta address kamili ya mtu wa ndani wa mtu huyo.
HUTAFUTA ANUWANI YAKO “UNAPO ISHI” KWA KUTUMIA JINA LAKO:
Wakipata anwani ya mtu huyo, ndipo humpigia, sasa, napo sema kumpigia, namaanisha, kumtupia uchawi wao.
WACHAWI HUCHAGUA ADHABU YA KUKUPA:
Kabla hawaja mtupia uchawi mtu huyo wachawi huchagua adhabu za kumpa MTUHUMIWA wao. Adhabu zinatofautiana,
Zinaweza kuanzia kupigwa upofu, kuchukuliwa msukule, kusababishiwa ajali mbaya, kupigwa ugumba, ukichaa, utasa, kutumiwa kama banda la kufugia pepo wachafu, laana ya vifo vya familia, au kifo kabisa kutegemea na namna ambavyo wataamua kufanya.
USIKOSE SEHEMU YA PILI, WACHAWI HUCHAGUAJE ADHABU YAKO…..
Karibu kwa Yesu aliye hai na Mungu Mkuu ili ujilinde na uchawi na nguvu za giza.
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
www.maxshimbaministries.com

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW