Sunday, November 20, 2016

ZANZIBAR INAONGOZA KWA KUWA NA IDADI KUBWA YA MASHOGA WENYE UKIMWI


Na Nora Damian
KISIWA cha Unguja, kinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mashoga wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na Dk Subilaga Kasesela-Kaganda wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), alipokuwa akizungumza katika kongamano kuhusu maambukizi ya ukimwi kwa wafanyabiashara ya ngono, mashoga na watumia dawa za kulevya.
Alisema Zanzibar ndio eneo lenye mambo ya ushoga hapa nchini na kwamba asilimia 12 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika Kisiwa cga Unguja ni wale wanaojishughulisha na mambo hayo.
Alisema baadhi ya sababu zinazochangia kukua kwa tatizo hilo ni vishawishi, wazazi kuwa mbali na watoto wao, yatima wanaokosa malezi mazuri, watoto wa kiume kulelewa na mama kwa kipindi kirefu na mtoto wa kiume kupenda kuvaa mavazi ya kike.
Alisema sababu nyingine zinazochangia tatizo hilo ni mazingira ya shule za bweni, ambazo baadhi yake zina wanafunzi wa kiume pekee, mwanaume kuwa na homoni nyingi za kike na wanaume wengi kukaa sehemu moja kama jeshini na magerezani.
�Na wanawake wanaopenda kufanya ngono ya haja kubwa wanapaswa nao kujua kuwa ina hatari zaidi, kwa maana ya kupata maambukizo kuliko njia ya uke,�alisema Dk Kaganda.
Alisema utafiti uliofanywa umeonyesha kuwa asilimia sita ya Watanzania wanaishi na virusi vya ukimwi, wanawake wakiwa ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo.
Dk Kaganda alisema tatizo hilo liko zaidi katika maeneo ya mijini na ligawagusa mno watu wazima na wanawake wenye uwezo wa kufanya ngono na watoto wadogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la TAWIF lililoandaa kongamano hilo, Fransisca Matao alisema jamii inachangia kwa kiasi kikubwa watoto wengi kuwa mashoga kufuatia kuwanyanyapaa na kuwatenga.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW