Thursday, November 17, 2016

YESU NI MWEMA


YESU NI MUNGU
Leo nitajibu HOJA ya Waislam ya Mungu Ndiye Mwema.
Waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidni wamekuwa na tabia ya kutumia aya 18-19 iliyopo katika Luka Sura ya 18, inayo sema Mungu Ndiye Mwema. Waislam wanadai kuwa, katika aya hii, Yesu amekana kuwa yeye si "MWEMA" na kuwa Mungu Pekee ni Mwema, hivyobasi, kukana kwa Yesu kuwa yeye si Mwema kunapinga Madai ya Wakristo kuwa Yesu ni Mungu.
Kwa hivyo utaona kuwa wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia na kusema kuwa eti Yesu amekana kuwa yeye si MWEMA. Fundisho hili la "MUNGU PEKEE NDIYE MWEMA" wanalieneza kwa kupitia Mitandao mbalimbali kama ya Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingawa hawajabadili dini wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila Mkristo, je, ni kweli Yesu alikana kuwa yeye si MWEMA? Nakusihi fuatilia somo hili kwa makini ili kujua Ukweli wa aya hii:
Luka 18.18-19 "Tena mtu mkubwa mmoja alimuuliza Yesu, akisema, Mwalimu Mwema, nifanye nini ili kuuruthi uzima wa milele? Yesu akamwambia mbona unaniita Mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, Naye ndiye Mungu".
Ukitazama kwa haraka haraka namna wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu wanavyoifunda hii aya ya Biblia unaweza ukashawishika kuamini hicho wanachokifundisha, lakini ni vyema tukajifundisha kwa undani kadiri majibu ya Yesu kuwa "Mungu Pekee Ndiye Mwema" kisha tuone kama kuna ukweli juu ya hayo mafundisho yao, ya kusema kuwa Yesu kakataa kuwa yeye si Mwema na hivyo kunamfanya kuwa yeye si Mungu.
Haya tuanze utafiti wetu.
Katika hii aya hapo juu, je, Yesu katoa jibu au kauliza swali? Hapa tunaona aya zinatufundisha waziwazi kuwa Yesu aliuliza swali na si kukana kuwa yeye si Mwema.
NUKUU: Yesu akamwambia Mbona waniita Mwema? Hapa Yesu kamuuliza swali, Yule mtu aliye muita “MWALIMU MWEMA” na si kukana kuwa yeye si “MWEMA" kama wanavyo fundisha Wahadhiri wa dini ya Kiislam katika Mihadhara yao ya kidini.
Baada ya Yule mtu kushindwa kujibu kwanini alimwita Yesu "Mwalimu Mwema". Yesu akasema yafuatayo:
Hakuna aliye Mwema ila mmoja, Naye ni Mungu. Je, Yesu alipo sema haya maneno alikana kuwa yeye si Mungu?
WAISLAM WANAKUBALI KUWA ALIYE MWEMA NI MUNGU TU.
Je, kuna sehemu yeyote ile katika Biblia ambayo Yesu anajiita yeye Mwema. Sasa tumsome Yesu katika Injili ya Yohana 10:14
Yesu anasema yafuatayo:
"14 Mimi ni Mchungaji MWEMA: ninawafahamu Kondoo wangu nao wananifahamu"
KATIKA YOHANA YESU ANAJIITA MWEMA.
Sasa basi, kufuatana na Waislam kukubali kwao kuwa "MUNGU PEKEE NDIE MWEMA" na Yesu kujiita Mwema katika Injili ya Yohana 10:14. Leo hii Yesu amewajibu Wahadhiri wa dini ya Kiislamu kuwa yeye ni Mwema na hivyo hii adhama ya Mwema inamfaya kuwa yeye ni Mungu, kutokana na Luka 18: 18-19. "Mungu Pekee ni Mwema".
Ni matumaini yangu kuwa leo hii umeweza kujua kwa undani maana ya "Mungu Pekee Ndiye Mwema" na Yesu alipo sema hayo alikuwa anamfahamisha yule kijana kuwa yeye ni Mungu na yule kijana hakukosea alipo muita MWALIMU MWEMA.
Sasa wapi aya Allah anasema yeye ni Mwema?
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW