Wednesday, November 16, 2016

SABABU TANO KWANINI WAKRISTO WANAABUDU JUMAPILI


Ndugu msomaji,
Katika kijarida hiki kifupi, nitakuwekea sababu tano (5) kwanini Wakristo wanaabudu siku ya Jumapili.
Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-
1) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].
2) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].
3) Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO 2:1]
4) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].
5) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.
Hakuna andiko lolote linalosema mtu yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi. Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].
KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA
Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13].
Wokovu wetu siku hizi uko ndani ya Kristo, siyo kwa kushika Torati ya Musa. Kuna watu wasiijua Biblia tena hawaelewi hata Agano Jipya. Hawaelewi KWA NINI Yesu alikufa. Kwa mfano wanaposema, ‘Imeandikwa katika Kutoka 20:8-11 lazima tushiike sabato!’ Je! ina maana mtume Paulo alifundisha uongo? Au alitaka kutudanganya? Au Unafikiri Biblia inajipinga yenyewe? Je! Unaamini Biblia siyo neno la Mungu? Au kwa nini watu wanapenda kujizika katika Agano la Kale?
Najua kuwa narejea kwenye mambo yale yale ambayo tayari nimekwisha yaandika hapo juu. Lakini mambo hayo ni ya kimsingi. Ni lazima tuyaelewe mambo hayo pale tunapoyaangalia maisha ya watu wa Agano la Kale! Kwa kupitia Biblia nzima tunajifunza sasa juu ya Yesu Kristo na wokovu wake. Lakini kama Biblia ni neno la Mungu (na ndivyo lilivyo) kwa nini basi waopo watu wanaopinga mpango wa Mungu kupitia mwanae Yesu Kristo ili waweze kubakia katika mpango wa kale ambaop Mungu mwenyewe ameuondoa?
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo… Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.”
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 16, 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW