Monday, November 21, 2016

MAANA YA NAMBA 666? (SEHEMU YA KWANZA)


Kifungu kuu katika Biblia ambacho kinataja "alama ya mnyama" ni Ufunuo 13:15-18. Marejeo mengine yanaweza kupatikana katika Ufunuo 14: 9, 11, 15:2, 16:2, 19:20, na 20:4. Alama hii hutumika kama muhuri kwa wafuasi wa Mpinga Kristo na nabii wa uongo (msemaji wa Mpinga Kristo). Nabii wa uongo (mnyama wa pili) ndiye ambaye husababisha watu kuchukua alama hii. Alama hasa huwekwa katika mkono au paji la uso na sio kadi mtu atabeba.
Ufunuo 13:16-18 na imeandikwa:
"Naye awafanya wote wadogo kwa wakubwa, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu aawaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu . Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita(666)".
Katika siku za hivi karibunu, namba hii imeanza kujitokeza kwa nguvu sana katika bidhaa mbalimbali. Namba hii inakuwa imeandikwa katika vifungashio na hata kwenye bidhaa yenyewe. Watu wengine wanaihusisha namba hii na matandao wa siri wa Freemasons ambao athari zake zinaonekana duniani na inasemekana mtandao huo kuwa na nguvu na ushawishi mkubwa duniani katika kila kitu. Kulingana na lugha ya ishara yaani 'Symbolism' na mtiririko wa namba yaani 'numerical patterns' katika Biblia na mojawapo ya vifungu vinavyoamsha utata huu ni Ufunuo wa Yohane 13:16-18
Maana ya 666 ni siri pia. Baadhi ya uvumi kwamba kulikuwa na uhusiano na mwezi wa 6, 2006-06/06/06. Hata hivyo, katika Ufunuo sura ya 13, namba 666 hubainisha mtu, si tarehe. Ufunuo 13:18 inatuambia, "Hapa ndipo penye hekima. Yeye mnyama huyo; maan ni hesabu ya sita, sitini na sita." Kwa namna fulani, namba 666 humtambua Mpinga Kristo. Kwa karne silizopita watafsiri wa Biblia wamekuwa wakijaribu kutambua baadhi ya watu wenye 666. Hakuna kubaliano kamili. Hiyo ndio sababu Ufunuo 13:18 inasema namba hii inahitaji hekima. Wakati Mpinga Kristo atafunuliwa (2 Thes 2:3-4), itakuwa wazi yeye ni nani na jinsi ya namba 666 humbainisha yeye.
Lugha ya misemo ya kitabu cha Ufunuo (Greek,apokalypsis; English , revelation) inafanana na ie ya kitabu cha Daniel. Hivyo kuna kundi la watafiti linalodai kuwa huenda mwandishi wa vitabu hivi viwili (Daniel na Ufunuo wa Yohane) ni mmoja. Watafiti wengine wanasema kuwa Kitabu cha Ufunuo wa Yohanne kiliandikwa wakati ambao Kanisa / wakristo walipata mateso makubwa na ujumbe wa kitabu hicho ilikuwa ni kuwatia moyo wakristo waliokuwa wakiteswa kwa ajili ya imani yao wasikate tamaa na waamini kuwa Mungu yupo pamoja nao muda wote na kwamba yeye ndiye mwanzo na mwisho wa yote.
Hivyo, mateso ya hapa duniani siyo mwisho wa yote.
Ndiyo maana katika mateso yote hayo kuna ujumbe wa matumaini- Mungu atawaokoa watu wake na kuwafanya waishi naye milele katika maisha mapya na atafuta kila chozi walilo nalo. Kitabu hiki kiliandikwa mwishoni mwa utawala wa Domitian (81-97 AD).
Kulingana na lugha na ujumbe wa kitabu chenyewe, inaaminika kuwa kiliandikwa wakati wa mateso kwa hiyo, lugha na misemo iliyotumika, lazima isomwe sambamba na lugha ya zamani ya Greek. Katika Greek namba kama 1,2,3,4,6,7 na 12 au mara mbili yake zina maana fulani. Namba 6 ni namba ya uovu au mwovu na hivyo namba 6 tatu (666) ni alama ya mwovu na hasa (kusisitiza zaidi)-mwovu wa waovu-evil forces.
Kwa wakati ule, ujumbe uliwahusu-first addressees- wale waliokuwa wanatesa Kanisa kwa ajili ya imani yake hasa mfalme Nero kwani kwa Kigiriki herufi za jina hilo zinafanya 666 au mtawala yoyote ambaye alitawala kimabavu (kinyama) na kuwatesa watu na pia wakristo wenyewe ili wasikate tama. Hivyo,666 ilikuwa kama alama na jina la mtu mkatili na mpinga Kristo aliyekuwa anawatesa na kuwaua wakristo (Wafuasi wa Yesu Kristo)
Biblia inasema kwamba watu hupata ile “alama ya yule mnyama-mwitu” kwa sababu wanamfuata “kwa mshangao,” kufikia hatua ya kumwabudu. (Ufunuo 13:3, 4; 16:2) Wanafanya hivyo kwa kutukuza nchi yao kutia ndani nembo zake na uwezo wa kijeshi, kufikia hatua ya kuabudu mambo hayo. Kitabu The Encyclopedia of Religion kinasema hivi: “Utaifa umekuwa dini kuu katika ulimwengu wa leo.”
Mtu anapewaje alama hiyo ya mnyama-mwitu juu ya mkono na paji la uso wake? (Ufunuo 13:16) Mungu alipolipatia taifa la Israeli amri, alisema hivi: ‘Myafunge kama ishara juu ya mkono wenu, nayo yatakuwa kama utepe wa kipaji katikati ya macho yenu.’ (Kumbukumbu la Torati 11:18) Hilo halikumaanisha kwamba Waisraeli walipaswa kutia alama juu ya mikono na vipaji vyao kihalisi, bali kwamba maneno ya Mungu yangeongoza matendo na mawazo yao. Vivyo hivyo, ingawa kihalisi nambari 666 haipaswi kuonwa kuwa kama chanjo au chale ambayo mtu amechorwa, kwa njia ya mfano wale ambao huruhusu mifumo ya kisiasa itawale maisha yao wanatambulishwa kwa alama hiyo ya huyo mnyama-mwitu. Wale walio na alama ya mnyama-mwitu wanampinga Mungu.—Ufunuo 14:9, 10; 19:19-21.
Kwa mujibu wa ufun 13 fungu la 17, kuna sifa 3 muhimu za kumtabulisha
¨ Alama yake (Mamlaka yake)
¨ Jina lake
¨ Namba ya jina lake (666).
Angalia maana ya jina lake kwa Kigiriki = LATEINOS
¨ L = 30 lambda
¨ A = 1 alpha
¨ T = 300 tau
¨ E = 5 epsilon
¨ I = 10 iota
¨ N = 50 nu
¨ O = 70 omicron
¨ S = 200 sigma
————
666
Rejea hapa Encyclopedia Britannica under “Languages of the World”, Table 8.
Maana ya Kimaandishi:
VICARIUS – Asimamaye badala ya, au kwa
niaba ya.
FILII – Mwana/kijana wa kiume
DEI – Maana yake ni MUNGU
Ufafanuzi wa jina lenyewe
V = 5 F = no value D = 500
I = 1 I = 1 E = no value
C = 100 L = 50 I = 1
A = no value I = 1 501
R = no value I = 1
I = 1 53
U/V = 5
S = no value
112
Haya fanya mahesabu rahisi tu 112 + 53 + 501 = 666
Barikiwa sana na endelea kusoam Biblia mwenyewe na mwombe Roho Mtakatifu akufungua macho ya rohoni.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW