Sunday, November 20, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA TATU)


Ni mwaka wa 617 K.W.K. Danieli na marafiki wake watatu, Shadraki, Meshaki, na Abednego, wako katika makao ya mfalme wa Babiloni. Wakati wa miaka mitatu ya mazoezi katika makao ya mfalme, vijana hao wanadumisha utimilifu wao kwa Mungu. Miaka minane hivi baadaye, Mfalme Nebukadneza anaota ndoto ambayo inamfadhaisha. Danieli anafunua ndoto hiyo na kisha anatafsiri maana yake. Mfalme anakiri kwamba Yehova ni “Mungu wa miungu na Bwana wa wafalme na Mfunuaji wa siri.” (Danieli 2:47) Hata hivyo, punde si punde, inaonekana Nebukadneza anasahau somo hilo. Marafiki watatu wa Danieli wanapokataa kuabudu sanamu kubwa, mfalme anaamuru watupwe ndani ya tanuru ya moto. Mungu wa kweli anawaokoa wanaume hao watatu, na Nebukadneza analazimika kutambua kwamba “hakuna mungu mwingine yeyote anayeweza kuokoa kama huyu.”—Danieli 3:29.
SWALI:
Daniel 1:1, tunajua nini kuhusu Nebukadneza II zaidi ya mambo yaliyomo kwenye Biblia?
Jina lake limeandikwa kwa Kiingereza kama Nebukadneza na Nebukadreza, lakini la pili linafanana zaidi na jinsi Wababeli walivyolitamka. Linamaanisha Nabo [mungu] linda mpaka wangu.
Kwa mujibu wa Encyclopedia Britannica (1972) Nebukadneza II alikuwa mtoto wa kiume mkubwa zaidi wa Nabopolasa.
Aliwashinda Wamisri huko Carchemish mwaka 605 KK.
Nabopolasa alipokufa, Nebukadneza II alirudi Babeli na alitawala toka mwaka 605 KK hadi Agosti/Septemba 562 KK. Kumbukumbu ya matukio ya Babeli inatoa maelezo ya mapigano yake huko Misri, kuiteka Tiro, na kuishinda Yuda mwaka 597 KK. Alipigana na Elam mwaka 596 KK na alizimisha maasi mwaka 595 KK. Baada ya hapo, kumbukumbu ya Babeli haipo hapa.
New International Dictionary of the Bible, uk.696 ina picha ya amri ya Kibabeli ikiorodhesha matukio tokea mwaka wa mwisho wa Nabopolasa hadi mwaka wa 11 wa Nebukadneza II. Inataja kutekwa kwa Yerusalemu na Babeli.
Nebukadneza aliijenga bustani ya kunyongea ya Babeli, ambayo imeitwa moja ya maajabu saba ya ulimwengu wa kale. Alizijenga kwa ajili ya mke wake Amytis, na binti wa mfalme Astyages (kwa Kimidiani Ištumegu) wa Midiani.
SWALI:
Kwenye Daniel 1:1, je Nebukadneza aliivamia Yuda kwenye mwaka wa tatu wa Yehoyakimu, au mwaka wa nne kama Yer 46:2 inavyosema?
Vyote, na huu ulikuwa ni uvamizi mmoja tu, kwa sababu mfumo wa tarehe uliotumika Uyahudi kwenye karne ya tano KK ulikuwa tofauti na ule uliotumika Babeli.
Kuna maelezo ya ziada yenye kufurahisha sana hapa. Kama 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.192 inavyoonyesha, hakuna Myahudi aliyeandika karne za baadaye ambaye angetumia kalenda ya Kibabeli iliyoonyesha mwaka tofauti na jinsi Yeremia alivyoandika. Badala ya kuwa kosa kwenye Kitabu cha Danieli, jambo hili linathibitisha kuwa Danieli iliandikwa karne ya tano siyo baada ya hapo.
When Critics Ask, uk.291-293 inaeleza undani wa mifumo hii miwili ya kalenda. Kalenda ya mfumo wa "Nisani" ambayo Yeremia (na Waashuri) walitumia ilianza na mwezi wa Nisani (Aprili).
Yehoyakimu kwa sababu ya Yuda siku chache baada ya mwaka mpya, hivyo mwaka [mzima] wa kwanza ulianza siku ya kwanza ya mwaka uliokuwa unafuata. Danieli alitumia kalenda ya "Tishri" ambayo mwaka mpya ulianza mwezi wa "Tishri" karibu na Oktoba. Mwaka [mzima] wa kwanza wa kutawala kwa Yehoyakimu ulianza kwenye siku ya kwanza ya Tishri. Uvamizi wa Babeli ulitokea wakati wa majira ya joto ya mwaka 605 KK. Pia, The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1328-1329 inaongeza kuwa Wababeli hawakuhesabu sehemu ya muda wa kutawala wa mfalme mpya kabla ya kuanza kwa mwaka mpya kama mwaka wake wa kwanza, wakati Wayahudi hawakufanya hivyo.
SWALI:
Daniel 1:2, je Shinari iko wapi?
Shinari ni jina lenye maana karibu sawa na Babeli. Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.599 kinadai kuwa hili ni kosa la kikronolojia. Hata hivyo, waandishi wa riwaya mara nyingi hutumia neno lolote kati yale yenye maana karibu sawa, na Danieli anafanya hivi hapa.
SWALI:
Kwenye Dan 1:3-6, wanne hawa hawakuwa vijana pekee toka Yuda waliokuwa wakimhudumia mfalme. Kwa nini unadhani vijana wengine hawajatajwa sehemu yeyote ile kwenye Kitabu cha Danieli?
Huenda vijana wengine walifikiri kuwa hawakuwa na uhuru wa kukataa kula chakula cha walichopewa kwa hiyo walikula. Mara baada ya kukubaliana na jambo hilo, waliweza kuafiki mambo mengine zaidi. Lakini kumbuka, unao uhuru wa kuchagua mambo wakati wowote ule.
SWALI:
Kwenye Dan 1:7, jina Belteshaza linatamkwaje?
Wycliffe Bible Dictionary, uk.216 inalitamka (kwa Kiingereza) bel-te-SHAZ-er. Silabi za kwanza na tatu zina voweli fupi, "te" ina voweli ndefu "e" yenye nukta juu yake, na "er" ina "e" yenye kiwimbi juu yake.
USIKOSE SEHEMU YA NNE Daniel 1:6, je majina haya yalimaanisha nini? Belteshaza, Shadraka, Meshaki, na Abednego.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW