Tuesday, November 22, 2016
KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA TANO)
Mfalme Nebukadreza aliota ndoto ambayo ilimshtusha sana, Usingizi wake ulimwacha, Alipoamka, Akaisahau ile ndoto aliyoiota. Akawaita waganga,na wachawi,na wasirihi,na wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto yake. Waganga wote na wenye Hekima wote walishindwa kumtafsiria Mfalme Ile ndoto.Mfalme akakasirika akataka kuwaangamiza wachawi wote,na wenye Hekima wote wa Babeli.
Ndipo Danieli alimwomba mfalme ampe Muda ili Amtafsirie Mfalme Ile ndoto. Danieli na wenzake walimwomba Mungu kuhusu ile ndoto, naye Mungu akamfunulia Danieli Ndoto ya mfalme na Maana yake.Danieli akasimama mbele ya Mfalme na Kumtafsiria ile ndoto akasema,’’ Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha.Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.
Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.[DAN2:31-35].
Danieli alitoa tafsiri yake kuwa ile sanamu Huwakilisha falme kuu nne zitakazotawala Dunia [DAN2:36-45]. Alimwambia Mfalme kuwa Kichwa cha Dhahabu kilimaanisha UFALME WA BABELI, chini ya mfalme Nebukadreza. Ufalme Huu ulitawala kuanzia 605BC-539BC.
Baada ya Ufalme wa Babeli, ufalme uliofuata ulikuwa ni ufalme UMEDI NA UAJEMI unaofananishwa na mikono na kifua cha Fedha uliotawala tangu 539BC-331BC.
Baada ya Ufalme wa Umedi na Uajemi,Ufalme uliofuata ulikuwa ni Ufalme wa UYUNANI unaofananishwa na tumbo na kiuno cha shaba ambao ulitawala tangu mwaka 331BC-168BC.
Ufalme wa nne unaofananishwa na Miguu ya Chuma unawakilisha ufalme wa Rumi ambao ulitawala tangu 168BC-476AD.
Nyayo za Miguu zenye mchanganyiko wa chuma na udongo,ni Rumi iliyokuja kugawanyika katika mataifa Kumi ya Ulaya nayo ni Portuguese [suevi], Spanish [Visigoths] Germany [Alamanni], swiss [Burgundians], French[Franks], Italians [Lombards], England [Saxons], na Heruli, vandals, Othtrogoths- [Haya mataifa matatu yalikuja baadaye kung’olewa na upapa]. Haya mataifa, mengine ni Chuma ikimaanisha yana nguvu, na mengine ni Udongo, ikimaanisha kuwa Hayana nguvu.
Mataifa haya hayataweza kushikamana kama chuma kisivyoweza kushikamana na udongo.Wapo waliojaribu kuunganisha Ulaya iwe Taifa moja Kubwa kama Rumi ya zamani,wengine hata kwa kuunda undugu kwa njia ya kuoana kiukoo wa kifalme lakini walishindwa.Mfano wa Watu mashuhuri kihistoria waliojaribu kuunganisha ulaya lakini wakashindwa ni [charlemagne, charlesV, LouisXIV, Kaiser wilhelm, Hitler].
Lile jiwe lililochongwa mlimani bila kazi ya Mikono,na kuvunjavunja ile sanamu vipande vipande,na Kuwa mlima Mkubwa na Kuijaza Dunia yote,ni Ufalme wa Yesu ambao ndio Ufalme wa Mwisho utakaokuja na Kuzishinda falme zote za Dunia, na Kutawala Milele na Milele,wala watu wengine hawataachiwa Enzi yake.
SWALI:
Kwenye Danieli 2, ndoto hii ilitokea lini?
Kwenye Danieli 2, Danieli alichukuliwa mwezi wa sita hadi nane mwaka 605 KK. Tarehe 7 Septemba 605 KK, Mfalme Nebopolasa, baba yake Nebukadneza, alikufa, na Nebukadneza akawa mtawala mkuu wa Babeli. Danieli 2 ilikuwa kwenye mwaka wa pili wa utawala wa Nebukadneza.
Mwaka 604 KK kwa mujibu wa maelezo kwenye NIV Study Bible, uk.1301 na Evangelical Bible Commentary, uk.592.
Mwaka 603 KK kwa mujibu wa New International Bible Commentary, uk. 854 na Daniel: Key to Prophetic Understanding, uk.45-46 cha Walvoord.
Kati ya Aprili 603 na Machi 602 KK The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.39.
Karibu miaka minne baada ya mwaka 605 KK na matukio ya Danieli 1 kwa mujibu wa Lange’s Commentary on Daniel, uk.66 ya zamani (iliyochapishwa mwaka 1901). Aliamini kuwa Nebukadneza hakuwa mtawala pekee hadi miaka kadhaa baada ya kifo cha baba yake.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:1, kwa nini aliwasiliana moja kwa moja na Nebukadneza, mtu asiyekuwa anamcha, kwenye ndoto badala ya kuongea na Danieli?
Uovu wa mtu haumzuii Mungu kuwasiliana naye au kumtumia kwa makusudi yake.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:2-10; 4:7; 5:7,11, je Wakaldayo walikuwa ni watu gani?
Ingawa Waamori wa Babeli waliitwa Wakaldayo, hivi sivyo inavyomaanisha hapa. Katika jamii ya Kibabeli, Wakaldayo walikuwa ni tabaka la makuhani. Waamori walitokea kaskazini magharibi. Wakaldayo hawakutokea jangwa la Arabuni, licha ya jinsi Asimov’s Guide to the Bible, uk.387 inavyosema.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:2-10; 4:7; 5:7, 11, je kuwaita makuhani Wakaldayo kunaonyesha kuwa Kitabu cha Danieli kiliandikwa maiaka ya baadaye kama kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.601 kinavyodai?
Hapana. Gleason Archer anayo makala ya kina kwenye Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.285-286 inayoongelea jambo hili.
1. Danieli anatumia neno la Kiebrania, Kasdim, si tu kwa makuhani, bali pia kwa Wakaldayo (Wababeli) kwenye Dan 5:30. Kama kutumika kwa neno hili kulionyesha kuwa kitabu hiki kiliandikwa baadaye, basi Dan 5:30 ingeonyesha kuwa kitabu hiki kiliandikwa miaka ya awali.
2. Hata hivyo, kutumika kwake kwa namna mbili kunaonyesha kuwa kitabu hiki kiliandikwa wakati wa uhai wa Danieli. Lugha ya Kiakadi, ambayo Wababeli wa wakati wa Danieli waliiongea, walitumia neno hilohilo Kal-du (litokanalo na neno la Kisumeri Gal-du) kwa makuhani na taifa. Mbao yenye maandiko iliyoandikwa kwenye mwaka wa 14 wa Shamash-shumukin (mwaka 668-648 KK) unatumia neno Gal-du kwa makuhani. Archer anasema Wababeli kabla wa miaka iliyotangulia kuanguka kwa Ashuri walitumia neno Gas’du kwa Wakaldayo. Baada ya kuangukwa kwa Ashuri, walibadilisha konsonanti "s" kwenye maneno mengi kuwa konsonanti "l."
3. Wagiriki, waliokuwa wanawafahamu Wababeli muda mrefu kabla Daniele hajazaliwa, waliliita taifa hili Chaldaioi.
SWALI:
Kwenye Dan 2:3-7, je Mfalme Nebukadneza alikosa busara kuliko wafalme wengine kwa kuwaambia wanajimu na wabashiri kuwa watauawa endapo hawatato tafsiri ya ndoto?
Si lazima iwe hivyo. Kwa mujibu wa Herodotus kwenye History, kitabu cha 14, uk.134, wakati mfalme wa Sinthia alipougua, aliomba watabiri watatu wamwambie mtu aliyemfanya aumwe kwa kuapa kwa uongo kutumia meko ya mfalme. Endapo mtuhumiwa angekiri kufanya hivyo angeuawa. Endapo mtuhumiwa angekana kufanya hivyo, watabiri wengine sita wangeitwa, na endapo wasingemtaja mtu yule yule basi wabashiri watatu wa kwanza wangefungwa na kutupwa kwenye mkokoteni na kichaka kilichowashwa moto.
Hivyi ndivyo inavyoelekea kuwa wakati kazi ilipokuwa na malipo mazuri, lakini bado kukawa na sababu nzuri za kutoifanya. Nafikiri nisingekubali kufanya kazi ya utabiri wa mfalme! Baadhi ya kazi siku hizi, kama kutumikia taasisi za kihalifu, haziwezi kurekebishika na usingetaka kuzifanya. Lakini kazi nyingine zinaweza kuwa zinashinikiza sana, na unaweza kuchoka, lakini Mungu anataka uwepo hapo kumshuhudia. Kwa mfano, tuchukulie kuwa umechaguliwa kuwa kiongozi wa kisiasa ambapo unatakiwa uchague kati ya kuwiwa shukrani na moja ya makundi yenye maslahi maalumu. Unaweza kuchagua kutokuwiwa na kundi lolote lile, ingawa wakatti wa uchaguzi hautapata kiasi kizuri cha hela za kufanyia kampeni, utashindwa vibaya sana kwenye uchaguzi, na utapaswa kutafuta kazi nyingine. Danieli alikuwa anafanya kazi yenye kushinikiza sana. Lakini badala ya kuikimbia kazi hiyo, Danieli alisimama mahali ambapo Mungu alitaka awepo.
SWALI:
Je Daniel 2:4-16 inaeleza nini kuhusu tabia ya Nebukadneza?
Yafuatayo ni mambo matano.
1. Nebukadneza alikuwa na kigeugeu. Aliagiza vijana hawa wanne wa Kiyahudi wafunzwe, na baada ya kufunzwa alikuwa anaenda kuwaua pamoja na watu wengine wenye hekima kwa jambo ambalo mtu yeyote asingeweza kulifanya? Nebukadneza alifurahishwa na Danieli na rafiki zakekwenye Daniel 1:18-20, lakini walikuwa wanakwenda kuuawa pamoja na watu wengine kwenye Daniel 2:17!
2. Alikuwa mtu katili na mkali. Katika sehemu hii ya dunia, kwenye Daniel 2:5 walipokuwa wanabomoa nyumba walivuta mihimili ya mbao hadi vitu vyote vilipoanguka. Wakati wanafanya hivi, familia ilikuwa bado imo ndani ya nyumba.
3. Nebukadneza alikuwa na hasira mbaya.
4. Nebukadneza alikuwa mwenye kiburi na majivuno.
5. Nebukadneza alishangazwa kusikia wanajimu wakimjibu kuwa hakuna mtu aliyeweza kufanya jambo hili kwenye Daniel 2:10-11. Anaelekea kutokuwa na fununu yeyote jinsi maneno yake yanavyoweza kuwafanya watu wengine wajisikie au wafikiri. Au huenda hakujali jambo hili.
USIKOSE SEHEMU YA SITA Kwa nini Daniel 2:4b-7:28 iliandikwa Kiarami wakati Daniel 8:1-12:13 iliandikwa Kiebrania?
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Muhammad’s Fear Of Judgment Day
Muslims beware! The next eclipse could be the Day of Judgment . This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment