Saturday, November 26, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA SABA)


Siku Moja Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu kubwa sana ya dhahabu ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Kisha akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, ambayo aliyoisimamisha.
Akamwamuru mpiga mbiu kwamba awapigie kelee watu wa kabila zote na taifa na lugha kwamba wakati watakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, ambayo mfalme Nebukadreza ameisimamisha. Ikatolewa tangazo kwamba kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.
Hivyo Basi watu wote chini ya Mbingu walipoisikia sauti ya panda na filimbi, na kinubi na zeze na namna zote za ngoma wakaanguka kuisujudia ile sanamu ambayo Mfalme aliisimamisha. Lakini Marafiki zake Daniel ambao ni Shedrak na meshak na Abednego walikataa kuisujudia ile sanamu ya mfalme wakawa wakali wamesimama. Ndipo wakaldayo wakawashtaki hao wayahudi watatu kwamba wameikaidi amri ya Mfalme.
Mfalme aliposikia alikasirika sana. Akaamuru watu hao waitwe naye akawaambia hivi;”- Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
Wakina Shedrack na Meshak na Abednego wakamjibu mfalme kwamba hawataisujudia sanamu aliyoisimamisha mfalme na Kwamba Hata kama Mungu akiwaokoa ama la hawataisujudia ile sanamu kamwe. Mfalme alikasirika sana akaamuru Moto uchochewe mara saba na kisha akaamuru mashujaa wa jeshi lake wawafunge Wayahudi wale watatu na kisha kuwatupa katika lile tanuru la Moto. Ndipo wayahudi wale watatu wakatupwa katika lile tanuru la Moto hali wamefungwa.
Cha ajabu ni kwamba wale waliowatupa waliungua wakafa papo hapo walakini wale wayahudi watatu waliotupwa hawakuungua hata unywele tu na Moto haukuwa na Nguvu juu yao. Mungu alimtuma Mwana wake kuwaokoa akina Shedrack na Meshak na Abednego, na Mfalme alipoliangalia tanuru aliona watu wane badala ya watatu na yule wa Nne ni kama Mwana wa Miungu.
Ndipo mfalme akaamuru watu wale watolewe. Mungu aliwatukuza wale Marafiki zake Daniel mbele ya mfalme mpagani na watu wa babeli.Mfalme akaona ukuu wa Mungu na akamtukuza Mungu wa Mbinguni na kuamuru kuwa watu wote katika ufalme wake wasimtumikie Mungu mwingine isipokuwa Mungu wa Shadrak, meshak na Abednego.
Kisa hiki kinatufundisha kuwa imetupasa kuwa waaminifu kwa Mungu bila kukengeuka hata nukta ya maagizo yake hata kama kwa kufanya hivyo itaugharimu uhai wetu. Imewapasa watu wa Mungu waone kuwa ni bora kufa kuliko kuasi maagizo ya Mungu. Walakini Mungu aliyewaokoa wale wayahudi watatu atakuwa pamoja na watu wake naye atawaokoa wale wote walio waaminifu kwake.
Siku Moja Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu kubwa sana ya dhahabu ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Kisha akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, ambayo aliyoisimamisha.
Akamwamuru mpiga mbiu kwamba awapigie kelee watu wa kabila zote na taifa na lugha kwamba wakati watakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, ambayo mfalme Nebukadreza ameisimamisha. Ikatolewa tangazo kwamba kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.
Hivyo Basi watu wote chini ya Mbingu walipoisikia sauti ya panda na filimbi, na kinubi na zeze na namna zote za ngoma wakaanguka kuisujudia ile sanamu ambayo Mfalme aliisimamisha. Lakini Marafiki zake Daniel ambao ni Shedrak na meshak na Abednego walikataa kuisujudia ile sanamu ya mfalme wakawa wakali wamesimama. Ndipo wakaldayo wakawashtaki hao wayahudi watatu kwamba wameikaidi amri ya Mfalme.
Mfalme aliposikia alikasirika sana. Akaamuru watu hao waitwe naye akawaambia hivi;”- Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
Wakina Shedrack na Meshak na Abednego wakamjibu mfalme kwamba hawataisujudia sanamu aliyoisimamisha mfalme na Kwamba Hata kama Mungu akiwaokoa ama la hawataisujudia ile sanamu kamwe. Mfalme alikasirika sana akaamuru Moto uchochewe mara saba na kisha akaamuru mashujaa wa jeshi lake wawafunge Wayahudi wale watatu na kisha kuwatupa katika lile tanuru la Moto. Ndipo wayahudi wale watatu wakatupwa katika lile tanuru la Moto hali wamefungwa.
Cha ajabu ni kwamba wale waliowatupa waliungua wakafa papo hapo walakini wale wayahudi watatu waliotupwa hawakuungua hata unywele tu na Moto haukuwa na Nguvu juu yao. Mungu alimtuma Mwana wake kuwaokoa akina Shedrack na Meshak na Abednego, na Mfalme alipoliangalia tanuru aliona watu wane badala ya watatu na yule wa Nne ni kama Mwana wa Miungu. Ndipo mfalme akaamuru watu wale watolewe. Mungu aliwatukuza wale Marafiki zake Daniel mbele ya mfalme mpagani na watu wa babeli.Mfalme akaona ukuu wa Mungu na akamtukuza Mungu wa Mbinguni na kuamuru kuwa watu wote katika ufalme wake wasimtumikie Mungu mwingine isipokuwa Mungu wa Shadrak, meshak na Abednego.
Kisa hiki kinatufundisha kuwa imetupasa kuwa waaminifu kwa Mungu bila kukengeuka hata nukta ya maagizo yake hata kama kwa kufanya hivyo itaugharimu uhai wetu. Imewapasa watu wa Mungu waone kuwa ni bora kufa kuliko kuasi maagizo ya Mungu. Walakini Mungu aliyewaokoa wale wayahudi watatu atakuwa pamoja na watu wake naye atawaokoa wale wote walio waaminifu kwake.
SWALI:
Kwenye Dan 2:38, nini inaweza kuwa ni sababu ya Danieli kusema kuwa Nebukadneza alitawala wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani?

Ingawa Nebukadneza alitawala kanda wote wa mwezi mwandamo wenye rutuba [eneo linaloanzia pwani ya Mashariki ya Bahari ya Mediterania, kupita kwenye bonde la mito ya Hidekeli (Tigris) na Frati (Euphrates) na kwenda hadi Ghuba ya Uajemi], huenda palikuwa na sababu kubwa zaidi. Wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa Babeli, inawezekana walisoma mbele ya watu Shairi la Uumbaji, na mfalme alikuwa mwakilishi wa mungu Marduku, ambaye aliumba vitu vyote. Daniel: Key to Prophetic Understanding, uk.65.
Kihistoria, kila mtu anakubali kuwa Nebukadneza alikuwa ni mfalme mwenye nguvu sana Mashariki ya Kati, lakini hata kila mtu kwenye himaya ya Nebukadneza aliwafahamu wafalme wengine ambao hawakuwa chini yake. Je watu wa kwenye Biblia walijuaje jambo hili?
Neno la Kiarami kwenye Dan 2:38, 39; 4:22 ni ‘ara (Strong’s 772) linalotokana na neno la Kiebrania ‘erets (Strong’s 776). Lina maana nyingi sana. Kwa mujbu wa Strong’s Concordance neno la Kiebrania ‘erets linamaanisha "-a kawaida, nchi, dunia, shamba, ardhi, mataifa, njia, nyika, ulimwengi." Hivyo mbali ya kumaanisha dunia, neno hili linaweza likamaanisha pia nchi (yaani Mesopotamia). Msemo kama huu ulikuwa ni nahau na kichwa cha habari, kama miaka iliyotangulia Mfalme Amar-Enzu wa Utawala wa Tatu wa Kinasaba wa Uru alivyosema kuwa yeye ni lugal dubdalimmubak, au "mfalme wa Pande Nne za dunia" kwenye maandishi yake yaliyo kwenye majengo. Habari hii ni kwa mujibu wa The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.63. Inafaa ieleweke na wasikilizaji wote kuwa maneno haya hayaongelei sayari nzima, kama wakati wa Nebukadneza na wakati wa Amar-Enzu, Waelamu, Uajemi, Lydia, Misri, na Ugiriki zilikuwa nchi huru zilizofahamika sana nao. Hata hivyo, Nebukadneza, alikuwa mfalme mwenye nguvu sana Mashariki ya Kati, na kwa kadri alivyozidi kutawala ndivyo alivyozidi kuwa na nguvu zaidi.
Kwa hiyo kuna vitu viwili vinavyo wezekana: ‘ara (‘erets) ilimaanisha sayari yote ya dunia au ilimaanisha nchi ya Mesopotamia. Angalia kuwa Dan 2:38, 39 na 4:22 SI nabii;
mwishoni mwa utawala wa Nebukadneza wanamwambia jambo ambalo tayari analo. Inaelekea kuwa ni uwezekano wa pili, kwani hakuna mtu wakati ule ambaye angeelewa kuwa Wababeli walitawala Ugiriki, Umedi, Lidia, nk.
Kama wazo la nyongeza, Nebukadneza alitawala kutoka mwaka 605 hadi 562 KK, na mashambulizi ya kijeshi wakati wa utawala wake:
Mei/Juni 604 KK Wababeli walimshinda Wamisri huko Karkemishi.
11-12/605 au 604 KK Wababeli waliiangamiza Ashkeloni huko Foinike.
Mwaka 603 KK Wababeli waliiangamiza Ekroni huko Foenike.
Mwaka 601 KK Wababeli na Wamisri walipigana bila kupatikana mshindi; hasara kubwa.
Mwaka 600 KK Watu wa Lidia waliiangamiza Smyrna kwenye Asia Ndogo.
Mwaka 599-598 KK Wababeli walipgana na Waarabu.
16 Machi 597 KK Wababeli waliiteka Yerusalem, lakini hawakuiangamiza
Mwaka 596 KK Mfalme wa Babeli Nebukadneza II apigana na Waelami.
Mwaka 595-594 KK Nebukadneza II anazimisha maasi.
Mwaka 593/591 KK Mmisri Psamtik II pamoja na askari wa kukodiwa wa Kigiriki, Kifoenike na Kiyahudi waliishinda Nubia.
Mwaka 589-587 KK Wayahudi wanaiasi Babeli. Yerusalemu inazingirwa kwa miezi muda wa 30.
Mwaka 585-573 KK Wababeli wamzingira Mfalme Ethbaal II wa Tiro.
Mwaka 585 KK Vita kati ya Wamedi na Waaliate wa Lidia imeisha baada ya kupatwa kwa jua kwa tarehe 28 Mei 585 KK.
Mwaka 584-584 KK Nebukadneza II anaizingira Tiro.
Mwaka 581 KK Wababeli wanawarejesha makwao watu zaidi kutoka Yuda.
Mwaka 570 KK Wagiriki na Wakirene wanapigana kwenye jimbo la Kirene.
Mwaka 570 KK Wagiriki huko Kirene walimshinda Apries wa Misri.
Mwaka 568-567 KK Apries na Wababeli walijaribu kuivamia Misri.
Mwaka 560 KK Mfalme wa Lidia Croesus aitwaa miji ya Ionia (sehemu kuu ya pwani ya magharibi ya Asia Ndogo) kuanzia karibu karne ya 8 KK).
Mwaka 560-547/546 Waajemi walimtiisha Mfalme Croesus wa Lidia.
SWALI:
Kwenye Dan 2:44, ufalme wa Kristo utazivunjaje na kuziharibu falme nyingine?
Utazivunja falme nyingine kwa njia zisizopungua nne.
Kiroho, mapepo yana uwezo wa kuathiri falme, kama Dan 10:13 inavyoonyesha.
Kisiasa, falme zilizowahi kudai kuwa za Kikristo, au angalau ziliwahi kujifanya kuwa za Kikristo, zitatawala sehemu kubwa ya ulimwengu, kuanzia na Himaya ya Rumi wakati wa Mfalme Constantine (mwaka 324 BK).
Kitamaduni, mtazamo wa Kikristo utatawala fikra za kimagharibi kwa zaidi ya miaka elfu moja mia tano.
Hatimaye, (na jambo hili ni la muhimu zaidi) Mungu Mwana atakuja duniani, ataanzisha utawala wake, kila goti litapigwa kwa Yesu (Fil 2:9-11), na watu wote watakuwa chini ya mamlaka yake (1 Kor 15:24-25).
SWALI:
Kwenye Dan 2:48-49, je hatima ya ukatili wa Nebukadneza ilikuwa nini? Je jambo hili linaonyesha kitu gani kuhusu tabia ya Nebukadneza?
Nebukadneza alimpa Daniel cheo kikubwa na zawadi nyingi. Huenda Nebukadneza alifanya hivi si kwa ajili ya upendo wake kwa Danieli, lakini kumfanya awe mfano ili watu wengine pia wapende kumtumikia Nebukadneza kwa uaminifu.
SWALI:
Kwenye Danieli 3, ni njia zipi ambazo watu wanajaribu kuigiza hali wanayodhani ni hatima yao kwa njia zao wenyewe?
Watu wanaweza kuona kitu kuwa jaala au hatima yao, au chaguo la Mungu kwa maisha yao lenye kutokana na vipawa au karama zao, mazingira yao, mambo ambayo watu wengine wanawaambia, au fursa wanazoziona. Watu wazima hufanya hivi, lakini wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu huwa wanaambiwa kuwa wanapaswa kufanya hivi ili waweze kusaidia kufanikisha malengo yao ya kazi, au wakati mwingine mwenzi wa maisha wanayemtaka. Mara wanapofikiria kuwa kuna jambo linalowakabili, huwa wanafanya mambo haya yafuatayo.
Fahamu jinsi matokeo yenye mafanikio yatakavyo kuwa.
Huwa wanataka kupata sura ya kitu kichwani na kuiamini
Kisha watu wengine waamini mwisho walioukusudia
Chukua hatua ndogo kuufikia huku ukiepuka kuweka ahadi au "kutunza kazi yao ya siku"
Tafuta kujua hisia za watu kabla ya kuchukua hatua yeyote na tazama mambo yatakavyo kuwa hadi sasa
Wakati mwingine wanaweza "kuhesabu gharama" na fanya uamuzi kama jambo unalolikusudia kulifanya linastahili rasilimali za muda, fedha na nyinginezo ulizoandaa kuziwekeza
Wakati mwingine huthubutu kufanya vitu ambavyo matokeo yake hayatabiriki, na huweka juhudi zao zote katika malengo hayo, wakitambua kuwa wanaondoa mambo mengine ambayo wangeweza kuyafanya.
Kisha wanafanya ama jambo hilo, au jambo mbadala, au wanapatwa na msongo wa mawazo kwa sababu wameshindwa kabisa na wanafikiri hawawezi kupata nafasi nyingine ya kujaribu kitu kingine. Au, wanatambua kuwa kutakuwa na siku nyingine na fursa nyingine na wanaendelea kujaribu, kitu hicho hicho, au kitu kingine.
Mambo haya hapo juu yanaweza kuwa ni njia ya kawaida na ya busara ya kutimiza lengo lako, lakini kumbuka kuwa Mungu hahusiki na mambo hayo. Badala yake, kwa nini usianze na maombi, na uombe maongozi wa Mungu ili uweze kufanikiwa katika katika jambo ambalo anataka uwe, pia kuwa tayari kwa hali zitakazokujia ili kukuangusha.
Kisha omba maongozi ya Mungu, na kisha unaweza kuendelea na hatua hizo hapo juu, ukiomba uongozi wa Mungu na msaada wake katika kila hatua unayopitia.
SWALI:
Kwenye Dan 3:1, kwa nini Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, kwani alimkiri Mungu wa kweli kwenye Dan 2:46-47?
Ingawa Kitabu cha Danieli hakidokezei ama kipindi kirefu au kifupi cha muda kati ya maono na sanamu, mambo haya mawili yana uwezekano mkubwa wa kuhusiana. Wycliffe Bible Dictionary, uk.831-832, inaonyesha kuwa Nebukadneza huenda alikuwa anajaribu kupinga ujumbe wa Mungu uliotolewa kwenye ndoto ya mfalme, kuwa ufalme wake utaangushwa.
SWALI:
Kwenye Dan 3:1, kwa nini Nebukadneza alifanya sanamu nyembamba namna hii ya mtu mwenye urefu wa mita 27 (futi 90) na upana wa mita 3 (futi 9)?
Hivi si lazima view vipimo vya umbo bali vya sanamu. Sanamu hii huenda iliwekwa kwenye kiegemezo kirefu.
SWALI:
Kwenye Dan 3:12, kwa kuwa ni wavulana watatu tu wa Kiyahudi waliokataa kuinama mbele ya sanamu hii, je jambo hili linamaanisha kuwa Danieli nay eye pia aliinama?
Hapana, kwa sababu kwenye Dan 1:8 na Dan 6:10, Danieli anaonyesha kuwa hangefanya vitu visivyofuata maagizo ya Mungu. Danieli na Wayahudi wengine wacha Mungu hawakushikwa kwa sababu hawakuwepo pale. When Critics Ask, uk.294 pia inasema kuwa kwa kuwa Danieli alikuwa kiongozi wa serikali, anaweza kuwa alikuwa kwenye safari ya kikazi nje ya mji wakati huo.
SWALI:
Kwenye Dan 3:17-18, je Shedraka, Meshaki na Abednego waliamini kuwa Mungu atawaokoa, au hawakuwa na uhakika kiasi? Je tunapaswa kuwa na uhakika kuwa Mungu atauokoa?
Hawakuwa na uhakika wa kiasi fulani, kama ilivyoonyeshwa kwenye mstaru wa 18. Lakini hata kama Mungu asingewaokoa, walikuwa radhi kufa kwenye moto uliokuwa unawake kuliko kuafiki kuinama mbele ya sanamu.
SWALI:
Kwenye Dan 3:19, mtazamo wa Nebukadneza uliwezaje kubadilika hata hakuwa mwema tena?
Mwanzoni alifikiri alikuwa mpole kwa kuwatishia kuwatupa kwenye tanuru la moto, lakini aliwapa nafasi moja zaidi ya mwisho. Baada ya hapo hakutaka kuongea nao tena, lakini alilifanya tanuru kuwa la moto zaidi ili kutoa mfano kupitia kwao. Kwenye aya ya 22, lilikuwa moto sana hata askari waliokuwa wanawatupa ndani waliungua, lakini hakuna kielelezo chochote kuwa jambo hili lilimkera kwa namna yeyote ile. Mara nyingi wafalme na viongozi wakubwa huwa hawajali watu bali madaraka yao, na mamlaka yatokanayo na watu wa chini yao wanaowafuata. Wakati mwingine hata viongozi wanaojali watu wanaweza kuwatelekeza wanaposhambuliwa.
SWALI:
Kwenye Dan 3:19, je moto uliwezaje kuwa mkali mara saba?
Hawakuwa na uwezo wa kupima joto la moto. Lakini, hakuna shaka kuwa palikuwa na viriba vya kuchochelea moto vilivyotumika kuongezea hewa ya Oksijeni kwenye moto, na viriba saba (au mara saba) vilifunguliwa kuleta joto zaidi. Muda mrefu kabla ya wakati huu, zana za chuma hazikutumika sana kwa sababu hazikuweza kuyafanya matanuri yaliyokuwa na uwezo wa kuyeyusha kufua chuma.
SWALI:
Kwenye Dan 3:25, ni nani aliyekuwa mtu wa nne hapa?
Huyu anaaminika kuwa ni Kristo mwenyewe aliyetokea kabla ya kufanyika kwake kuwa mwili. Ingawa kuna uwezekano kuwa alikuwa malaika, maelezo ya Nebukadneza kuwa mtu huyu "ni mfano wa wana wa miungu" yanatoa uwezekano kuwa alikuwa Kristo. Waandishi wa wakati wa kanisa la awali waliosema kuwa huyu alikuwa ni Kristo ni Irenaeus, Tertullian, Hippolytus, na Cyprian wa Carthage.
Hippolytus (mwaka 225-235/6 BK) kwenye fragment 3 (Maelezo ya Kitabu cha Danieli) sura ya 2.93, uk.188 pia inasema kuwa Yesu alikuwa kwenye tanuri pamoja na Shadraka, Meshaki na Abednego, ingawa Yesu alikuwa bado kuzaliwa na bikira hapa duniani. Baada ya baraza la kanisa la awali lililofanyika Nikea, Hilary na Augustine wa Hippo walisema vivyo hivyo. Jerome alisema kuwa hakuwa Yesu bali malaika aliyejionyesha kwa sura ya Kristo.
SWALI:
Kwenye Dan 3:26, ni kitu gani cha ajabu sana kwa Nebukadneza kumwita Bwana "Mungu Aliye juu", na "Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme" kwenye Dan 2:47?
Huyu ni Nebukadneza yule yule aliyetengeneza sanamu na kuiabudu kwenye Dan 3:1. Inaonekana kuwa jambo hilo halikueleweka akilini mwake kuwa endapo kuna Mungu Mwenye Enzi yote basi tunapaswa kuzingatia mambo anayosema, na kutoiabudu miungu mingine.
SWALI:
Kwenye Dan 3:30, nini ilikuwa hatima ya watu waliowashitaki Shadraka, Meshki na Abednego kwenye Dan 3:8? Unafikiri ni sababu gani kubwa iliyomfanya Mungu afanye hivyo?
Waliona vijana wa Kiyahudi wakipandishwa vyeo. Sababu kubwa huenda HAIKUWA malipo kwa Shadraka, Meshaki, na Abednego. Inaelekea kuwa ilikuwa kwamba jina la Mungu liinuliwe, na endapo watu wengine wangesikia kuhusu kupandishwa vyeo huku wangefanywa wapende kumsikiliza Mungu Mwenye Enzi yote. Jambo hili ni la kweli zaidi kwa Wayahudi, ambao wangeweza kujaribiwa na kupotoka na kufanyika kuwa kama Wababeli, wangetiwa moyo sana.
USIKOSE SEHEMU YA NANE ...Kwenye Daniel 4:1-3, Je Nebukadneza alisema maneno haya kabla au baada ya mkasa wa Danieli?
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW