Sunday, November 20, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA PILI)


Kwenye Kitabu cha Danieli, kuna vitu gani vinavyofanana na sehemu nyingine za Biblia?
Danieli inaweza kuchukuliwa kuwa Ufunuo ya Agano la Kale. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayofanana na sehemu nyingine za Biblia.
Dhana au msemo Danieli = Sehemu nyingine za Biblia
1. Mnyama mwenye pembe kumi
Daniel 7:4-7 Ufunuo 13:1-3; 17:3
2. Magurudumu ya moto kwenye kiti cha enzi cha mbinguni
Daniel 7:9 Ezekiel 1:15-28; 10:1-22
3. Ten thousand times ten thousand and the river of fire in heaven Dananiel 7:10 Ufunuo 19:14. Angalia pia Mathayo 16:27; Jud 14
4. Yesu anakuja na mawingu; kila jicho litamwona Yesu akirudi
Dananiel 7:13 Ufunuo 1:7; Mathayo 24:30; Marko 13:26; Luka 21:27; Matendo 1:11
5. Joka akiangusha nyota
Daniel 8:10 Ufunuo 12:4
6. Gabrieli Dan 8:16; 9:21 Luka 1:19
7. Maombi ya toba ya pamoja
Daniel 9:4-19 Nehemiah 1:5-11
8. Mafuriko, au mto wenye maji
Daniel 9:26 Ufunuo 12:15; Nah 1:8
9. Miaka 3 ½
Daniel 9:26-27; 12:7,11 Ufunuo 11:1-3; 12:6; 13:5
10. Chukizo la uharibifu
Daniel 9:27; 11:31; 12:11 Mathayo 24:15
11. Mikaeli
Daniel 12:1 Ufunuo 12:7; Jud 9
12. Kitabu cha uzima 

Daniel 12:1 Ufunuo 3:5; 13:8; 17:8; 20:12,15; 21:27; Luka 10:20; Kutoka 2:32-33; Zaburi 69:28
13. Kufufuka
Daniel 12:2 Ufunuo 20:4-5
14. Tia/usiyatie mhuri maneno ya unabii
Daniel 12:4 Ufunuo 22:10
15. Sehemu ya ufunuo wa Mungu ilitiwa mhuri
Daniel 12:9 Ufunuo 10:4; Isaya 29:11-12
16. Mema na mabaya yaongezeka
Daniel 12:10 Ufunuo 22:11
SWALI:
Je muhtasari wa kitabu cha Danieli ni upi?
Wanazuoni wanatofautiana katika namna nzuri zaidi ya kuunda muhtasari wa Kitabu cha Danieli. Kuna mihtasari mikuu miwili ya Kitabu cha Danieli. Kwa upande mmoja, sura za 1-6 zinahusu maisha ya Danieli (na maono ya Nebukadneza) ziliandikwa katika nafsi ya tatu, na sura za 7-12 zina maono ya Danieli, zimeandikwa katika nafsi ya kwanza. Njia nyingine ya kuunda muhtasari wa kitabu hiki ni kuwa sura ya 1 inaelezea maisha ya awali ya Danieli iliyonadikwa kwa Kiebrania, sura za 2-7 zimeandikwa kwa Kiarami zikiwa ni maisha ya Danieli akitoa unabii juu ya hali ya baadaye ya watu wa mataifa, na sura za 8-12 zimeandikwa kwa Kiebrania zikiwani ni historia ya kinabii ya Israeli. Kama tuna michezo ya maneno, Mungu angeweza kuwa ana "michezo ya mihtasari?"
Kwa vyovyote vile, hapa ni muhtasari rahisi wa kitabu cha Danieli.
Danieli 1-6 Maisha ya Danieli
Danieli 1 Hali ya Danieli
Danieli 2 Ndoto ya Nebukadneza ya sanamu
Danieli 3 Nebukadneza anatengeneza sanamu yake mwenyewe
Danieli 4 Ndoto ya Nebukadneza ya kuwa kwake kichaa
Danieli 5 Karamu ya Belshaza na maandishi ukutani
Danieli 6 Amri ya Dario ya siku thelathini
Danieli 7-12 Maono ya Danieli
Danieli 7 Maono ya wanyama wanne
Danieli 8 Maono ya kondoo mume na mbuzi
Danieli 9 Maono ya sabini saba
Danieli 10-12 Maono ya Wagiriki
USIKOSE SEHEMU YA TATU Daniel 1:1, tunajua nini kuhusu Nebukadneza II zaidi ya mambo yaliyomo kwenye Biblia?
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW