Tuesday, November 29, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA NANE)


Mfalme Nebukadneza aliota Mti Mrefu na Mkubwa sana ulioota katikati ya nchi ambao ulikua na kuwa na nguvu, na Urefu wake ukafika Mpaka Mbinguni na kuonekana kwake mpaka Mwisho wa dunia. Majani ya Mti ule yalikuwa ni Mazuri, na matunda yake Mengi na ndani yake palikuwa na chakula cha kutosha kuwalisha watu wote. Wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.
Kisha katika Njozi Mfalme akaona Mlinzi ambaye ni Mtakatifu akishuka toka Mbinguni. Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake. Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake. Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.
Baada ya Mfalme Nebukadneza kuiota ndoto Hii, aliwaita waganga na wachawi na wanajimu na wenye Hekima ili wapate kumtafsiria ndoto ile walakini walishindwa kutafsiri ile ndoto. Ndipo Mfalme akamwita Danieli maana aliona kuwa Roho ya Miungu watakatifu inakaa ndani yake. Mfalme Alipoisikia ile ndoto alifadhaika maana alifahamu tafsiri yake. Nabii Danieli Kwa Hekima akamfafanulia Mfalme kwamba Yeye ndiye alikuwa ule Mti mrefu na Mkubwa uliofika Mpaka Mbinguni, na ambao wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake na ndege walikaa juu ya matawi yake, na ndani yake palikuwa na chakula cha kuwatosha watu wote.
Ufalme wa Babeli uliitawala dunia yote walakini Danieli alimfafanulia Mfalme kuwa sababu ya Kiburi chake na kutomtukuza Mungu ataondolewa roho ya Binadamu na kupewa moyo wa Mnyama, naye atafukuzwa mbali na wanadamu na kuishi porini kama wanyama wa mwituni na kula majani kama ng’ombe hata miaka saba ipite hata apate kujua kuwa Yeye aliye Juu ndiye anayetawala wafalme wote naye humpa Ufalme kila amtakaye.
Walakini ule ufalme wake hautang’olewa wote bali kama wale walinzi walivyoambiwa kuwa wakiache kisiki katika shina lake maana yake ni kwamba baada ya Miaka saba Ufalme wake utarudishwa. Nabii Danieli alimshauri Mfalme kutubu na kumrudia Mungu pengine Mungu anaweza kughairi na kuacha kumtenda Mfalme mambo aliyokusudia kuyafanya juu yake.
SWALI: Kwenye Daniel 4:1-3, je Nebukadneza alisema maneno haya kabla au baada ya mkasa wa Danieli?
Jambo hili lilitokea baada ya mkasa wa Danieli, kwa sababu maelezo haya ya Nebukadneza yenye kutumia nafsi ya kwanza yanatoka kwenye barua ambayo aliiandika baadaye.
*******

Yote ambayo Mungu aliyatabiri kwamba yatampata Mfalme Nebukadneza katika ile ndoto ya Mti sababu ya Kiburi chake yalitimizwa yote. Siku Moja Mfalme Nebukadneza alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akajivuna akasema kwamba;”- Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?
Neno lile lilipokuwa katika kinywa cha Mfalme sauti ilikuja kutoka Mbinguni ilisema;’- Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.
Yote yakatimia saa hiyohiyo. Mfalme Nebukadneza alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, na nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege. Baada ya Miaka saba kupita Mfalme alitubu na kumkumbuka Mungu, na kumtukuza Mungu wa Mbinguni, Fahamu zikamrudia, Enzi yake na fahari yake vikamrudia, Mawaziri wake na Madiwani wake wakaja kumtafuta.
Daniel 4 yote ni barua ya mfalme Nebukadneza kwa watu wote wanaokaa juu ya Uso wa Dunia akiandika juu ya Ukuu wa Mungu, Akimsifu, akimtukuza na akitoa Ushuhuda jinsi Mungu alivyoshusha kiburi chake na baadaye Kumrehemu. Mfalme alibadilika kabisa na kutubu na kuacha Ibada ya sanamu na Kumwabudu Mungu wa Waisraeli mpaka kufa kwake. Siku ile ya Mwisho ambayo Yesu atakuja kuwachukua watakatifu wake, Nebukadneza naye Atakuweko Miongoni mwa watakatifu watakaourithi uzima Wa milele.
Kisa hiki kinatufundisha kuwa Kiburi, Kujisikia, na Kujisifu, na kujitukuza nafsi ni machukizo kwa Mungu. Sifa na Utukufu ni Mali ya Mungu pekeena pale wanadamu wanapozitwaa sifa, na kujitukuza wenyewe na kujisifu badala ya Kumsifu na Kumtukuza Mungu, wanamkasirisha Mungu na kuiba kitu ambacho ni mali yake pekee.
Mungu anaweza kukuvika Uzuri wa kimwili, Anaweza kukufanya Mrembo, anaweza kukupa akili nyingi na Hekima kubwa. Anaweza kukuvika Heshima, Ufahari na Utajiri.
Anaweza kukufanya Msomi Mkubwa, anaweza kukufanya Mwimbaji mahiri na Mhubiri mwenye nguvu.
Anaweza kukupa Ufalme na kukupa Madaraka Makubwa. Walakini wenye Mwili wote sharti wafahamu kuwa ni Mungu ndiye aliyewapa vitu hivyo vyote na kwamba pale wanapojisifu na kujitukuza, na kujiinua, na kujiona Bora kuliko wengine na kuwa na Kiburi, Wanamtenda Mungu dhambi na Kumwibia sifa na Utukufu ambazo ni Mali yake pekee. Mungu aliyemwadhibu Mfalme Nebukadneza hata leo atawaadhibu wote ambao wana kiburi na kujisifu wenyewe kwa wema wao na vipawa vyao na kumsahau Mungu
*****
SWALI: Kwenye Daniel 4:8-9,18, kwa nini mfalme aling’ang’ana kumwita Danieli Belteshaza, na kuwa roho ya "miungu watakatifu" ndani mwake?
Danieli alisema kuwa alimtumikia Mungu Mwenye Enzi yote (umoja), lakini Nebukadneza anaelekea alisikia kuwa Danieli anaitumikia miungu (uwingi). Mara nyingi tunaposema vitu, na watu wanasema kuwa wanatuamini, bado huwa wanayachambua maneno tunayosema kwa mtazamo wao, na wanayatafsiri upya maneno yetu ili yafanane na mawazo waliyokuwa nayo kabla.
SWALI: Kwenye Daniel 4:10-17, kwa nini unafikiri Mungu alimpa Nebukadneza ndoto hii?
Ndoto hii isingeaminika na mfalme endapo ingekuwa imetolewa kwa Danieli au mtu mwingine yeyote yule. Haikutolewa kwa Nebukadneza kwa sababu alikuwa mtu wa kiroho zaidi, au bora kuliko Danieli, au kwa sababu alikuwa mcha Mungu zaidi ya watu wote. Kutoa ndoto kwa mtu aliyefaa zaidi kupewa kulikuwa ni kwa ajili ya makusudi ya Mungu, na zi kustahili kwa namna yeyote ile kwa Nebukadneza.
SWALI: Kwenye Daniel 4:13,23, je "mlinzi" ni nani?
Huyu alikuwa ni aina ya malaika. Vitabu vya Kiyahudi vya kidini vya kubuniwa (Apokrifa) pia vinaelezea malaika walinzi, lakini vinaweza kuwa viliandikwa baada ya Kitabu cha Danieli. Jambo linaloweza kusemwa kwa uhakika zaidi hapa ni kuwa Wayahudi walifahamu dhana ya malaika walinzi.
SWALI: Kwenye Daniel 4:33-37, je ni wakati gani Nebukadneza alikiacha kiti chake cha enzo kwa sababu ya kuwa na wazimu?
Danieli 4 inasema kuwa miezi kumi na mbili baada ya ndoto hii, Mungu aliyashughulikia majivuno ya Nebukadneza na kutimiza unabii huu.
Neno la Kiarami hapa linaweza kumaanisha "muda au msimu" lakini pia "mwaka." Hivyo, 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.195 inaonyesha kuwa huenda ulikuwa muda usiozidi miaka miwili badala ya miaka saba.
Believer’s Bible Commentary, uk.1080-1081, 1092 inaongezea kuwa ugonjwa huu wa akili unaitwa ‘boanthropy’ (yaani mtu-punda). Dr. R. K. Harrison anamwelezea mtu aliyekutana naye aliyekuwa na ugonjwa huu kwenye kitabu chake kiitwacho Introduction to the Old Testament, uk.1114-1117.
SWALI: Kwenye Daniel 4:33-37, je kuna ushahidi wowote mbali ya Biblia kuwa Nebukadneza alipatwa na wazimu kwa muda?
Huenda. Ingawa kitabu cha mwenye kushuku Asimov’s Guide to the Bible, uk.605 kinasema hakuna, The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.63 inataja kipande chenye kufurahisha cha Hati toka Bahari ya Chumvi cha Kiarami kilichokutwa kwenye pango la 4. Hii ni sala ya Nabonidus inayosema, "Maneno ya maombi ambayo Nabunai(d), Mfalme wa Ashuri na Babeli, mfalme mkuu, aliyosali wakati alipopigwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi kwa amri ya Mungu Mwenye Enzi yote kwenye mji wa Teima: ‘Nilipigwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi kwa muda wa miaka saba . . . kwa jina la Mungu Mwenye Enzi yote.’" (Tafsiri hii ya kukisia, inayotegemea kuongezea herufi nyingi ambazo hazikuwepo kwenye hati, ilichapishwa na J. T. Milik kwenye Revue Biblique, uk.63 (1956): 408; linganisha na Saggs, Babeli, uk.154 kwa toleo la Kiingereza hapo juu). The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.63 inasema jambo hili linaweza kuwa lilitokea baadaye, kinaweza kuwa kipande chenye masimulizi ya kimapokeo ambacho hakina uthibitisho wa wa kihistoria, kwamba huenda kina masimulizi ya kweli ama ya ugonjwa wa ngozi wa Nabonidus. Lakini inasema, ". . . uchunguzi wa kina wa kipande cha Nabonidus unaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mapokeo ya baadaye yaliyonukuriwa na kuandikwa upya kwa njia inayochangnya ya ugonjwa wa Nebukadneza mwenyewe, kama kweli haya hayaongelii ugojwa wa baadaye uliomkuta Nabonidus (ambaye miaka yake kumi ya kufungwa kwenye mji wa Arabuni ya kaskazini wa Teima [Teman] inaweza kuwa imehusisha ugonjwa huu)."
The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.246-247 inasema kuwa Maombi ya Nabonidus ni ya kubuniwa sana hata hayawez kusaidia, lakini yanaongezea mambo ambayo tunayajia kuhusu wazimu wa Nebukadneza kupitia Berossus, kuhani na mwana historia wa karne ya tatu wa Babeli, na mwandishi wa karne ya pili Abydenus, aliyesema kuwa Nebukadneza "alipagawa na mungu wa aina moja au nyingine", wakati alipotoa unabii na kutoweka Babeli.
Hivyo, ushahidi huu hauthibitishi jambo hili kikamilifu, lakini unaelezea kuwa rekodi rasmi za Babeli na hostoria ya Kigiriki havitoi maelezo yote ya tukio hili.
SWALI: Kwenye Daniel 4:33-37, je wazo la Nebukadneza kufanya vitu kama mnyama kunatokana na sanamu za Kiashuri za ng’ombe dume wenye vichwa vya binadamu na mabawa ya ndege, kama kitabu cha mwenye kushuku Asimov’s Guide to the Bible, uk.605 kinavyosema ni kubunia kunakovutia?
Haielekei kuwa hivyo. Kwanza kabisa, wanadamu wenye vichwa vya ng’ombe dume walifahamika Misri na Krete za zamani kuanzia wakati wa Musa. Pili, hizi zilikuwa sanamu za Waashuri, si za Wababeli. Danieli angekuwa na sababu kidogo za kuandika kitu kuhusu "binadamu-mnyama", kuliko Musa aliyeishi Misri.
USIKOSE SEHEMU YA TISA ...Kwenye Daniel 5:1 na 30, Belshaza alikuwa ni nani?
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW