Wednesday, November 16, 2016

JE, MUHAMMAD ALITABIRIWA KWENYE AGANO JIPYA?


Kwenye Yohana 14:16-26; 15:26; 16:5-15, je Muhammad alitabiriwa kwenye Agano Jipya kama Msaidizi au Roho Mtakatifu, kama ambavyo baadhi ya Waislam wanadai?
Jibu: Hapana. Kama jambo hili lingekuwa kweli, basi Waislam wangeamini mambo haya matano (ambayo hawayaamini)
1. Muhammad alimtukuza Yesu. (Yohana 16:14)
2. Mungu alimtuma Muhammad kwa jina la Yesu. (Yohana 14:26)
3. Muhammad alikuwa ametumwa na Yesu pia. (Yohana 16:7)
4. Muhammad alitwaa hekima ya Yesu na kuifanya ifahamike kwetu. (Yohana 16:15)
5. Muhammad alikuwa "ndani ya" mitume. (Yohana 16:17)
Kwa hiyo, hakuna Muislam mwenye ueleo wa mambo atakayeamini kuwa mistari hii inamuongelea Muhammad. Mistari hii lazima iwe inamwogelea mtu mwingine aliyetumwa na Mungu.
Kwa upande mwingine, pengine Waislam wanapaswa kumtukuza Yesu, kama wanadhani kuwa Muhammad alifanya hivyo, kulingana na mistari hii.
Kama wazo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) naye alizungumzia jinsi ambavyo Msaidizi kwenye Yohana 14-16 ni Mungu Roho Mtakatifu kwenye Disputation with Manes sura ya 34-35 uk.208-209
Tazama When Cultists Ask uk.182-183 na When Critics Ask uk.419-420 kwa maelezo zaidi.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW