Sunday, November 20, 2016

ETI BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU ALIYE ARABUNI?


Wakristo huyu aliye kuwa ARABUNI ni nani?
Waefeso 1:12-14
12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu 13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.14 Ndiye aliye ARABUNI ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake....... Ili ni swali aliloleta Kaka Fadhili Baraka na ni swali ambalo utalikuta miongoni mwa Waislamu wa Afrika mashariki tu ambao usoma Biblia ya Kiswahili ; Kwa akili za Wailamu hawa waendesha Mihadhara bila shaka Huu ni Utabiri wa Muhammad ambaye kwao ni Mtume wa Allah. Sasa naomba kulijibu kwa kuzingatia mambo kadhaa ambayo yanatajwa kwenye andiko ili;
1. Mwanzo kabisa aya haisemi UARABUNI BALI arabuni tena kwa herufi ndogo sio UARABUNI
2. Wenzetu hawa Wana matatiso kibao, yaani kwao Mtume Paulo ni kama shetani ila akitaja tu Arabuni basi ashakuwa Malaika! ! Au sijui wanapodai Kuwe hapa Andiko ili ni utabiri wa mwana wa Amina wanatufundisha kuwa Mjumbe wa shetani kama wanavyomdai Paulo, ashakuwa Mtume ili awe mtabiri wa ujio wa mtume wa Mungu! !!
3. Halafu Ukizingatia Paulo anatumia kauli ya WAKATI ULIOPO, yaani NDIYE ALIYE ARABUNI, sio NDIYE atakayekuwa ARABUNI kimsingi basi neno Arabuni hapa limetumika kwa maana ya dhamana, guarantee, deposit yaani ROHO MTAKATIFU aliyewatia muhuri Waumini ndiye dhamana yetu kuwa tu milki ya MUNGU. Tazama 2korinto 5:5
4.Lakini pia Waislamu wanatikiwa waelewe ya kwamba neno moja linawezekana kuwa na maana tofauti tofauti kutegemea na sentesi na matumisi, mathalani Neno Paka, Paka rangi, Paka Mnyama wa nyumbani, Paa, kwa maana ya kupaa juu, Paa , Mnyama wa porini, Paa la nyumba, KAA, kaa chini yaani keti, Kaa yaani Mkaaa wa kuni yaani Kaa la moto, Kaa mnyama, Kaa kwa maana ya ishi, yaani Chaka anakaa Dar, sasa sio kila ukiona neno Arabuni wewe ukimbilie tu kwa maana ya UARABUNI ama ukisikia tu Arabuni tayari umwemwona mwana wa Amina! !!

5. Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu Ndiye aliye Arabuni ya wokovu wetu....... Naomba kila Muislamu akasome tena aya hizi haswa akizingatia maneno haya halafu tuone hoja zao wanazozijenga kuhusu mwana wa Amina. .....
6. Kwanza ROHO YULE WA AHADI , Kwanza ni MTAKATIFU, swali je mwana wa Amina ni mtakatifu? !! Majibu tunayo wenyewe, Allah anamtaka aombe msamaha kwa dhambi zake na dhambi za waislamu wa kiume na wa kike. Qu 47:19, 40:55. Ilibidi Allah atume Malaika KUMFANYIA oparesheni ya kifua mara nne kuondoa fungu LA shetani moyoni mwake na kila mara huyo shetani alikuwa akirudi!
7. Alimfinyia uso kibofu aliyehitaji kusikia ujumbe ili awalinganie watu muhimu kwenye jamii, Qu 80:1-,
8. hakujua mambo ya ghaibu yaani ya siri za MUNGU na mwenyewe anakiri angelijua ghaibu angelijizidishia wema wala baya ama uovu wowote usingelimguza, Qu 7;188-189. Kwa maneno mengine, kwa kuwa hakuijua ghaibu, yaani hakuzijua siri za MUNGU Basi maovu yalimguza
9. Ama kuhusu Roho Mtakatifu kinyume na Muhammad maandiko yansema 1Cor 2:10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
10. Muhammad mwana wa Abdallah bado anasubiri adhabu kama wanadamu wengine, Qu 10;102 na baya zaidi bado anategemea sisi wanadamu tumwombee kwa MWENYEZI MUNGU, wala sio sisi tu, bali hata Allah wa Qur'an na malaika zake wanafanya Kazi nzito ya kumswalia mwana wa Amina na maombolezo haya yatazidi mpaka Qiyama ili Uenda Mwenyezi Mungu akamsamehe.
Kwa maana hiyo pasina hata kuzingatia mantiki ya aya hizi za Mtume Paulo bado mwana wa Amina hana cheti cha kupemyeshwa humu ili awe ndiye aliyekusudiwa hapa.
11. mwisho kabisa; ni vyema nikilinukuu andiko ili kwenye lugha ya kiingereza; Ephe 1:11 In the Messiah we were also chosen when we were predestined according to the purpose of the one who does everything that he wills to do, 12so that we who had already fixed our hope on the Messiah might live for his praise and glory. 13You, too, have heard the word of truth, the gospel of your salvation. When you believed in the Messiah,s you were sealed with the promised Holy Spirit, 14 who is the guarantee of our inheritance until God redeems his own possession for his praise and glory.
Utaona limetumika neno GUARANTEE , na ndio maana waislamu wasomi kama Muhoro Shaban hawaitumii hoja hii isipokuwa wale Maamuma ambao pia wamesikia hoja hizi kutoka kwa waendesha miadhara kwa miaka mingi mpaka wakadhani ni kweli kama kina Mazinge Othman Sulaiman Mazinge, Muhammad Saidi Khamisi Said Kinyogoli na wengine
Imeletwa kwenu na Mwalimu Chaka Wa Musa

2 comments:

Unknown said...

Cha kushangaza ni kwamba Waislamu wanasema Biblia ni corrupted na bado wanaiamini kwa kile wanadhani ni cha maana kwao

Unknown said...

Cha kushangaza ni kwamba Waislamu wanasema Biblia ni corrupted na bado wanaiamini kwa kile wanadhani ni cha maana kwao

WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"?

 WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"? Dr. Maxwell Shimba explains: The Word and the Divine Nature – A Comprehensive Exposit...

TRENDING NOW