Wednesday, October 12, 2016

WAISLAM WA DHEHEBU LA WASHIA WAUWAWA MJINI KABUL

Kabul

Shambulio limetokea eneo maalumu la ibada kwa Waislam ambao ni waumini wa dhehebu la Shia katika mji wa Kabul huko Afghan.

Watu 14 wamekufa na wengine 26 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Shambulio hilo lilitokea katika mkusanyiko wa washia waliokua wakiadhimisha siku muhimu ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein katika kalenda ya Shia, inayojulika kama Ashura.

Mashuhuda wanasema kuwa mlipuko ulisikika kabla ya mshambuliaji kumimina risasi. Wasuni wenye msimamo mkali kama Taliban wanaamini kuwa washia ni waasi na wanalenga misikiti na mikusanyiko ya Umma.

Mpaka hivi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lilitangaza kuhusika na shambulio hilo. BBC

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW