Saturday, October 29, 2016

NENO LA MUNGU LINASEMA NINI KUHUSU SABATO? (SEHEMU YA TISA)


Kwenye somo letu lililo pita “Sehemu ya Nane” tulijifunza sababu zilizo mfanya Bwana Yesu kuingia Sinagogi. Sasa tutajifunza kama kusali na au kuabudu siku ya Jumapili ni makosa.
Wasabato wanasema kuwa, Mungu aliweka agano lake na kamwe haliwezi kubadilika. Hivyo basi, kwenda Kanisani siku ya Jumapili ni kinyume na sharia ya Nne kati ya zile kumi, na ni makossa. Je, kusali jumapili ni makossa? Zifuatazo ni baadhi tu ya hoja hizo na majibu yake;
Neno la Mungu linasema wazi kuwa kuitunza Sabato ilikua ishara maalumu kati ya Mungu na Waisraeli: “Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli watishika sabato, kuiangalia sana hiyo sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika” (Kutoka 31: 16-16).
1. WASABATO WANASEMA KUSALI JUMAPILI NI MAKOSA: Wasabato hudai kwamba, Wakristo wanaofanya ibada zao siku ya jumapili, ni makosa mbele za Mungu, maana siyo agizo la Mungu bali ni agizo la mwanadamu.
Hoja hii ya Wasabato si ya msingi na haina ukweli ndani yake na ni dhaifu katika maantiki ya kuwa Mungu alivunja sabato kupitia Yesu ambaye ni Bwana wa Sabato.
HOJA FUPI: WAKRISTO NI WANAFUNZI WA YESU NA SIO MUSAKwanza kabisa ningependa watu waelewe kwamba, Wakristo wanaofanya ibada zao siku ya jumapili na siku nyingine, hao si wanafunzi wa Musa, bali ni wanafunzi wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ndiye mdhamini wa agano lililo bora zaidi, yaani agano jipya, kama Biblia inavyosema katika Waebrania 7:22, “Basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.”
Lakini pia, msingi wao, wa kufanya ibada siku ya Jumapili na siku nyingine, hautokani na torati ya Musa, bali ni msingi unaotoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo (nitaeleza kwa upana katika sura inayosema ‘Kwa nini Wakristo wanafanya ibada zao siku ya Jumapili’).
Hata hivyo, bado katika agano la kale Mungu aliagiza watu wakusanyike Jumapili ingawa wasabato wengi hawalioni andiko hilo.
UTHIBITISHO:Tukiangalia katika Kutoka 12:16 Biblia inasema, “SIKU YA KWANZA kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na SIKU YA SABA kutakuwa na kusanyiko takatifu, haitafanywa kazi yoyote katika SIKU HIZO, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.” Siku ya kwanza ya juma ni Jumapili, na siku ya saba ni Jumamosi kwa kalenda yetu. Kwa hiyo mtoto wa Mungu, mwanafunzi yeyote wa Musa wa nyakati za leo anapokuja na kukusumbua juu ya siku ya Jumamosi, mwambie mbona siku ya kwanza ya juma yeye hafanyi ibada na ni agizo la Mungu kama tulivyokwisha kuona katika Kutoka 12:16.
2. WASABATO WANADAI KUWA, KUABUDU JUMAPILI “SUNDAY” NI IBADA YA MUNGU JUA:
Wasabato wanadai kwamba, Wakristo wanafanya kusanyiko siku ya Jumapili, wana abudu mungu Jua, kwa sababu siku ya Jumapili kwa Kiingereza huitwa ‘Sunday’ ikimaanisha siku ya Jua.
Hoja hii si ya msingi na haina ukweli ndani yake zaidi ya kusema kinyume na maandiko. Ili tupate kuelewa ukweli wenyewe, kwanza ni vema tukaziorodhesha siku zote saba kwa kiingereza alafu tuangalie maana ya siku zote saba, hapo ndipo tutabaini ukweli. Lakini ni vema tukafahamu kuwa, siku hizi saba, zilipewa majina na wapagani wa Kirumi kulingana na mungu wa kila siku hiyo, ingawa Mungu alipoumba siku, hakuzipa majina, bali alitumia siku ya kwanza hadi siku ya saba. Hivyo kuzipa kwao majina ya miungu yao ya kipagani, haizuii Wakristo wa kweli kumuabudu Mungu wao aliyeumba siku hizo, maana Yeye ndiye Mzee wa siku. Kwa mfano, siku inapoitwa, siku ya Mwenge (Mwenge day) ikiangukia Jumamosi, je tutasema wasabato wanamwabudu mungu Mwenge, na hivyo kuwafanya wasifanye ibada siku hiyo? Kwa sababu serikali imetangaza siku hiyo ni siku ya Mwenge (Mwenge day). Au siku ya ukimwi duniani, ikiangukia Jumamosi, je itawazuia wasabato wasifanye ibada siku hiyo, kwani ni siku ya ukimwi, hivyo wakifanya ibada zao watakuwa wanamwabudu mungu ukimwi? Ebu sasa turudi kwenye kuangalia majina ya siku zote saba kwa Kiingereza na maana yake;
MAANA YA MAJINA YA SIKU KWA KIINGEREZA:>Jumatatu (Monday) - inatokana na moon day, kwa wapagani wa nyakati zile ilimaanisha siku ya kumwabudu mungu moon (mwezi).
>Jumanne (Tuesday) –inatokana na tiw’s day, kwa wapagani wa nyakati zile ilimaanisha ni siku ya mungu Tiw.
>Jumatano (Wednesday) –inatokana na wedn day au woden day, kwa wapagani ilimaanisha siku ya mungu wedn au woden.
>Alhamisi (Thursday) –inatokana na thor day, kwa wapagani ilikuwa ni siku ya kumwabudu mungu thor.
>Ijumaa (Friday) - inatokana na frig day au freia day, kwa wapagani ilikuwa ni siku ya mungu frig au freia.
>Jumamosi (Saturday) –inatokana na Saturn day (siku ya sayari zohari), kwa wapagani ilikuwa ni siku ya kumwabudu mungu wa Kirumi aitwaye Saturnyaani kwa Kiswahili sayari ya zohari.
>Jumapili (Sunday) –ilitokana na sun day (siku ya jua), kwa wapagani waKirumi ilikuwa ni siku ya kumwabudu mungu sun (jua).
Hivyo basi, Siku zote za juma, Warumi walizipa majina ya miungu yao, kwa sababu hao kwa kipindi hicho ndiyo walikuwa watawala. Swali linakuja, kwa vile zimepewa majina ya miungu ya kipagani, hivyo siku zote hazifai kufanya ibada?
Siku ya Jumamosi, Warumi walikuwa wakimwabudu mungu Saturn kwa Kiswahili zohari, swali ni kwamba, kwa kufanya ibada zao Jumamosi, wasabato wote wanamwabudu mungu zohari yaani sayari ya zohari (Saturn)?

Mtoto wa Mungu ni lazima ufahamu kwamba, kupewa jina baya la siku, halikuzuii wewe siku hiyo kumwabudu Mungu wa kweli, kwa sababu jina hilo halitoki kwa Mungu bali hutoka kwa mwanamu ambaye hajawahi kuiumba siku. Kwa hiyo kama msabato atakwambia kuwa unafanya ibada Jumapili (Sunday) hivyo unamwabudu mungu jua, basi wewe utamjibu unafanya ibada Jumamosi (Saturday), hivyo unamwabudu mungu sayari ya Saturn (zohari). Hata hivyo wanaomwabudu Mungu wa kweli siku ya Jumapili, hawafanyi ibada kwa mungu jua, bali wanafanya ibada kwa Mungu wa kweli aliyeumba Jua.
3. WASABATO WANADAI KUWA YESU ALISHIKA SABATO
Wasabato hudai kwamba, kwa vile Bwana Yesu aliingia hekaluni siku ya sabato (Marko 1:21; Luka 4:31), hivyo alishika sabato.
TAKRIBANI ASILIMIA 99 YA WASABATO HAWAELEWI MAANA YA NENO SABATO.Hoja hii pia si ya msingi na wala si ya kweli. Katika utafiti wangu nilioufanya, nimegundua kuwa waumini wa dhehebu la wasabato, asilimia 99 hawaelewi maana ya neno sabato, na hata walipoletewa dhehebu hili kutoka Marekani, walikuwa hawajatafuta kuchunguza maandiko kama watu wa Beroya (Matendo 17:11-12).
Sabato maana yake ni pumziko la kazi, na kuingia hekaluni haina mahusino na neno sabato. Kuingia hekaluni siku ya kwanza ya juma (Jumapili) na siku ya saba kwa wana wa Israeli ilikuwa ni agizo la kusanyiko la kawaida (Kutoka 12:16). Ila kama Biblia ingesema Bwana Yesu alipumzika kufanya kazi siku ya sabato, hapo tungesema kuwa alishika sabato.
Anayejua kuwa Bwana Yesu alishika sabato au la ni wasabato halisi (Mafarisayo) wa nyakati za Yesu, maana hao ndiyo waliopewa kushika sabato na Mungu mwenyewe, na siyo wanaojiita wasabato leo ambao wameagizwa kushika sabato na waanzilishi wa dhehebu hilo.
Ebu tuwasikilize wasabato halisi (Mafarisayo) zama za Yesu wanasemaje, je Bwana Yesu alishika sabato au la?
UTHIBITISHO:Katika kitabu cha Yohana 9:16 Biblia inasema, “Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, KWA SABABU HASHIKI SABATO. Wengine wakasema, awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo, kukawa matengano kati yao.”

WAYAHUDI NA MAFARISAYO WALITAKA KUMUUA YESU KWASABABU ALIIVUNJA SABATO NA KUSEMA KUWA MUNGU NI BABA YAKE
Kama ulikuwa huwajua Wasabato hali, sasa nategemea umesha pata picha kamili. Wasabato halisi wanakiri kabisa kwamba, Bwana Yesu hakushika sabato.
Bwana Yesu siku ya sabato aliendelea kufanya shughuli zake kama kawaida, Yohana 5:16-18 Biblia inasema, “Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, KWA KUWA HAKUIVUNJA SABATO TU, bali pamoja na hayo, alimwita Mungu Baba yake.”
Oh Halleluya! Tunaona jinsi Bwana wetu alivyovunja sabato na ndiyo maana, wakataka kumwua. Kama kweli, katika Agano jipya tunashika sabato, mbona Bwana wetu aliivunja sabato, na Yeye ndiyo kiongozi mkuu wa wokovu wetu (Waebrania 2:10)?
SASA, NYIE WASABATO MNAMFUATA MUSA AU MNAMFUATA YESU?
Sasa ndugu jiulize, unamfuata Musa au unamfuata Bwana Yesu aliyeivunja sabato?
Kama unamfuata Musa hutafika mbinguni, kwani yeye mwenyewe alishasema habari za kumfuata Bwana Yesu na siyo yeye, Kumbukumbu 18:15, tunasoma, “Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zake kama nilivyo mimi; msikilize yeye.”
1. Lakini kama unamfuata Bwana YESU sabato ya nini?
2. Aliivunjwa kwa kuwa alijua ni kivuli tu, ilikuwa ni ishara yake, sasa yeye aliye pumziko la kweli amekuja, sasa sabato ya nini?
Kama unasema unamfuata Bwana Yesu, na wakati bado, hautaki kuivunja sabato (kivuli), kamwe hutaweza kuona wokovu halisi uliotokana na kazi ya msalaba. Kwa kuwa Yeye ndiye kiongozi wako na Mungu wako, na aliivunja sabato na wewe uivunje, kwa kuwa sisi sote tunamfuata Kristo kwa kila neno na tendo.
Ndugu msomaji nategemea umesha elewa kuhusu Wasabato na ni wafuasi wa MUSA na sio YESU. Kama unabisha, basi nieleze kwanini katika Yohana 9:16 Biblia inasema, “Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, KWA SABABU HASHIKI SABATO. Wengine wakasema, awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo, kukawa matengano kati yao.”?
Sabato ilipeanwa kwa Waisraeli, si kanisa. Sabato bado ingali siku ya Jumamosi si Jumapili na haijawai badilishwa. Bali sabato ni sehemu ya sheria ya Agano La Kale na Wakristo wako huru kutoka kwa mkono wa sheria (Wagalatia 4:1-26; Warumi 6:14). Wakristo hawitakiwi kuitunza sabato hata kama iko siku ya Jumamosi au Jumapili. Siku ya kwanza ya juma, siku ya Bwana (Ufunuo 1:10) za sherekea kiumbe kipya Kristo aliyefufuka akiwa kiongozi wetu. Hatujaamrishwa kiufuata sheria ya Musa ya sabato ya kustarehe, bali tuko huru kumfuata Kristo aliyefufuka. Mtume Paulo alisema kwamba kila mkristo amue mweneyewe kama ataifuata sabato, “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe” (Warumi 14:5). Twastahili kumwabudu Mungu kila siku, si Jumamosi pekee or Jumapili pekee.
Warumi 14:1-12, tumewekwa huru kutokana na laana ya Sheria, hivyo basi, kusali si lazima iwe Jumamosi au Jumapili. Mungu hana utegemezi wa siku tena bali unaweza kusali siku yeyote ile na Mungu akakusikia na si lazima uwe kwenye Jengo ambalo tunaliita "Kanisa".
Biblia inaendelea kusema kuwa, tupo huru katika Kristo Warumi 6:14. Ndio maana tuanenda Kanisani katikati ya wiki na tunasali Mungu.
Warumi 14.5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Nduguzangu, kutokana na Warumi 14, tumewekwa huru kuchagua siku ya kuabudu, na nini tule au tusile, hivyo hivyo ni kuadhimisha kwa Bwana. Hivyo basi, hakuna kosa lolote lile mtu anapo sali Jumamosi au Jumapili au Jumatatu, au siku yeyote ile ya wiki. Mungu wetu yupo kila siku na siku zote alizumba yeye.
Tumefika mwisho wa Sehemu ya TISA, na sasa tutaenda SEHEMU YA KUMI.
TORATI = AMRI KUMI + SHERIA 613 + HUKUMU ZAKE
********** USIKOSE SEHEMU YA KUMI ***********
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.
www.maxshimbaministries.org

1 comment:

Dr Chesebe said...

Ndugu max,mbona ushiriki katika hukumu ya mwovu shetani kwa kutoa mafunzo ya uongo? Bwana yesu katika yohana 5:16-18,hakuivunja sabato.Ni wayahudi waliona tu hivyo kwa mtazamo wao.Marko 2:27,28 Inatueleza kuwa sabato n
Ni ya watu wore na yesu ndiye bwana was sabato.angeivunja aje? Katika mathayo 5:17,yesu anasema hakuja kulitangua tirati na manabii Bali kulitimiza.yohana14:15,yesu anasema mkinipenda mtazishika amri zangu,he,amri alizokuwa akirejelea ni zipi?

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW