Monday, October 24, 2016

NENO LA MUNGU LINASEMA NINI KUHUSU SABATO? (SEHEMU YA TANO)


Baada ya kujifunza sheria mbali mbali za Sabato na jinsi ilivyo vigumu kuzifuata hizo sharia na adhabu yake ya kifo kwa kupigwa mawe kwenye Sehemu ya Nne. Sasa tuangalie kuhusu mavazi. Je, kuna mavazi ya kitorati?
MAVAZI
Imeandikwa: ... wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja. (Mombo ya Walawi 19:19b). Usivae nguo iliyochanganyikana sufu na kitani pamoja. (Kumbukumbu ya Torati 22:11). Hii ilikuwa ni amri iliyohusu nguo halisi kabisa zinazovaliwa mwilini.
Hata leo sheria ya kutovaa mavazi yaliyochanganya rangi bado iko palepale.
Pia imeandikwa: Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki ... (Isaya 61:10).
Mavazi ni ishara ya wokovu. Wokovu ni mmoja tu. Hauwezi kupatikana kwa njia nyingine tofauti na iliyowekwa na Mungu.
Maandiko yanasema: Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. (Matendo ya Mitume 4:12), yaani ni jina la Yesu pekee. Kutafuta wokovu kwa kutumia dini, imani au jambo jingine lolote nje ya Yesu ni kujivika mavazi ya rangi nyingi. Vazi la wokovu ni la rangi moja tu; nyeupe!
Katika kipindi cha kwanza haikuruhusiwa kuvaa mavazi halisi yenye rangi tofautitofauti.
Katika kipindi cha pili, mavazi ni wokovu. Hivyo, kuwa na vazi la aina moja ni kusimama na wokovu halisi wa Yesu Kristo bila kuuchanganya na mambo ya kidunia.
Hata hivyo, katika kipindi cha utimilifu wa yote, mbinguni kuna mavazi halisi ya haki yaliyo ya milele, ambayo yatakuwa safi siku zote; milele na milele.
Imeandikwa: Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe ... (Ufunuo 7:9). Haya ni mavazi ambayo yameoshwa kwa damu ya Mwana-Kondoo wa Mungu.
Kutembelewa na Bwana
Bwana alipotaka kuwatembelea watu wake, watu walifua nguo halisi kabisa walizovaa mwilini. Imeandikwa: Bwana akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao, wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote. (Kutoka 19:10-11).
Katika kipindi cha kwanza, watu walifua mavazi yao halisi ya mwilini ndipo Bwana alikuja kusema nao. Mavazi hayo yalifuliwa kwa maji halisi.
Katika kipindi cha pili, kinachooshwa si mavazi halisi ya mwilini, bali ni dhambi katika mioyo yetu. Dhambi hizo zinaoshwa kwa njia ya damu ya Yesu Kristo.
Katika kipindi cha tatu, yaani cha utimilifu kwa yote, si tu kwamba hakutakuwa tena na haja ya kuoshwa (maana wote watakuwa watakatifu milele), lakini pia hakutakuwa na kusema kuwa kuna kutembelewa na Bwana, maana watakatifu watakuwa naye siku zote.
Imeandikwa: Nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala milele na milele. (Ufunuo 22:4-5).
Kwanini Yesu alisema hakuja kuitengua Torati?
Yesu Kristo anasema kwenye Injili kutokana na Mathayo kuwa: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Mathayo 5:17).
Sasa tujiulize maswali machache:
1. Je, Yesu alichinja Mbuzi na Mafahali kila mwaka kwa ajili ya dhambi?
2. Je, Wanafunzi wa Yesu, walichinja Mbuzi na Mafahali kwa ajili ya dhambi zao?
3. Je, Wasabato wanachinja Mbuzi na Mafahali kwa ajili ya dhambi zao kila mwaka?
Nategemea jibu lako hapo juu ni hapana, maana sijawai soma aya ambayo inasema Yesu au Wanafunzi wake walichinja Mbuzi au Mafahali. Zaidi ya hapo, sijawai waona Wasabato wakichinja Mbuzi au Mafahali kwa ajili ya dhambi zao kila mwaka. Kumbe basi, hawa Wasabato hawatunzi Torati zaidi ya kuchagua kile ambacho wanataka ili kutengeneza dini yao. Sasa, kuna faida gani ya kuchagua chagua aya ili kukidhi matakwa binafsi?

‘Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.” (Yohana 1:17).
Sheria ina mwanzo wake na mwisho wake. Nikimaanisha kuwa, yule aliye itunga sheria, anaweza kuleta sheria nyingine na kuivunja ile ya mwanzo ambayo ni dhaifu au imepitwa na wakati.
Katika Timotheo wa Kwanza Mlango wa Kwanza aya ya tano tunasoma kuwa:
“…mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki” (1 Timotheo 1:5). UMEONA NENO “MWISHO” ni UPENDO?
Mungu alipo toa sharia kwa Musa alikuwa na kusudi lake, na alipo maliza hilo kusudi, ndio alimtuma Mwanae Yesu Kristo kuja na kutuletea “NEEMA” ambayo inatufungua kutoka utumwa wa sharia.
Hivyo basi, lengo kuu la Mwanzoni la Mungu lilikuwa ni kuleta sharia itakayo waongoza wana wa Israel, lakini alikpo kuja Mwanae, Mungu alituletea UPENDO yaani, tuwe wenye haki na watakatifu katika upendo (Waefeso 1:4).
Kristo Yesu yeye ndie ‘mwisho’ wa sheria, anawakilisha utekelezo na utimilifu wa sheria ndani Yake mwenyewe. Neno la Mungu linasema kuwa YESU NDIE MWANZO NA MWISHO, ALFA NA OMEGA. Sawasawa na tabia yake Yesu ni Mwenye Haki, ni matakatifu, ni mwenye upendo. Yesu hahitaji kujaribu kufikia dhumuni na au lengo na au kusudi la kuletwa kwa Torati “Sheria”, kwasababu, Yes undie haki, kweli, upendo, utakatifu, na uzima ambayo sharia ililetwa ili tuwe hivyo.
Hebu tusome katika Warumi na tuone kama kweli Yesu ni Mwisho wa Sheria:
“Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.” (Warumi 10:4). Umeona hapo, kuwe Yes undie MWISHO WA SHERIA, SASA KAMA YESU AMEKUJA, NA KATULETEA NEEMA NA UPENDO, KWANINI TUENDELEE KUSHILIA SHERIA?,
Hebu angalia hii aya inavyo sema:
“kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.” (Warumi 5:19). Na tena, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” (2 Wakorintho 5:21).
Kimaantiki, inaleta maana kama ifuatavyo:
1. Adam katenda dhambi na akaingiza dhambi kwa wanadamu wote.
2. Yesu kaja na katuletea msamaha wa dhambi kwa wanadamu wote.
Yaani, kwa imani katika Kristo Yesu tunahesabiwa haki; pia tunazaliwa mara ya pili toka juu, yaani ‘tunapata kuwa haki ya Mungu katika Yeye.’!
Yesu ambaye ni ‘utimilifu wa sheria’ kwa tabia yake yenyewe, yeye mwenyewe ni tekelezo (mwisho) wa sheria na sisi tunaingia katika utimilifu kupitia Kristo, kwa imani, na kwa Roho Mtakatifu! “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika Kristo Yesu aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.” (Wakolosai 2:9,10).
Hivyo basi, mtu ambaye anang’angania kuwa Yesu alikuja kuitekeleza Torati kama ilivyo kuwa wakati ule wa Nabii Musa, basi mtu huyo hajui maana ya Injili “HABARI NJEMA’ na labda hata hafahamu maana ya wokovu wa Mungu katika Kristo Yesu. Mtu huyo ni kama wale ambao “wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.” (1 Timotheo 1:7).
Kuhusu kafara, kwanini sasa hatufanyia kama wakati wa Musa?
Hata leo bado tunatoa kafara ya damu ili kusamehewa dhambi zetu. Tofauti tu ni kwamba hatutoi tena wanyama halisi kama zamani za akina Nabii Musa. Wanyama waliotolewa kafara katika Agano la Kale walikuwa ni kivuli au taswira ya kafara timilifu, yaani Mwana-Kondoo wa Mungu, Yesu Kristo. Ndio maana nilisema kwenye Sehemu ya Tanu na Nne kuwa, Torati ilikuwa kama kivuli.
Yohana alipomwona Yesu alisema: Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu. (Yoh. 1:29). Kama ambavyo zamani wanyama waliuawa kwa niaba ya mtenda dhambi, yaani walibebeshwa dhambi zake, ndivyo ambavyo Mwana-Kondoo wa Mungu alivyobebeshwa dhambi ya ulimwengu wote, kisha akatolewa kafara kwa niaba ya ulimwengu wote.
Ndiyo maana maandiko yanamwongelea Bwana Yesu kuwa ni: Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake. (Ufu. 1:5).
SABABU ZILIZOPELEKEA WANA WA ISRAEL KUPEWA SHERIA YA KUSHIKA SABATO
Ziko sababu kuu mbili zilizopelekea wana wa Israeli peke yao, kuamriwa kushika sabato;
NI KUMBUKUMBU KWA WANA WA ISRAELI KUWA WALIKUWA WATUMWA KATIKA NCHI YA MISRI.
Katika kitabu cha Kumbukumbu la torati 5:15 Biblia inasema, “Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa, kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru ushike sabato.’’
Kwa hiyo, ni wana wa Israeli peke yao, ndiyo walio amriwa kushika sheria ya siku maalum ya kupumzika yaani sabato, ili kwao iwe kumbukumbu kwamba, walikuwa watumwa katika nchi ya Misri. Kwa hiyo, kwa mtu asiye Mwana wa Israeli akishika sheria ya siku ya sabato, atakuwa anakumbuka nini? Je alishawahi kuwa mtumwa huko Misri?
WANA WA ISRAELI WALIAMRIWA KUISHIKA SABATO ILI IPATE KUWA ISHARA YA AGANO KATI YAO NA MUNGU.
Katika kitabu cha Kutoka 31:13 Biblia inasema, “Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika sabato zangu, kwa kuwa ni ISHARA kati ya mimi na ninyi, katika vizazi vyenu vyote, ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.”
Kadhalika katika kitabu cha Kutoka 31:16-17 Biblia inasema, “Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika sabato, kuiangalia sana hiyo, katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Ni ISHARA kati ya mimi na wana wa Israeli milele…..” Pia katika Ezekieli 20:20 Neno la Mungu linasema, “Zitakaseni sabato zangu, nazo zitakuwa ISHARA kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.” Ezekiel 20:12 inasema, “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ISHARA kati yangu mimi na wao…..”
ANGALIZO: Neno ishara linamaanisha siyo kitu halisi, bali ni kitu kinacho ashiria kitu fulani ambacho kitakuja, ni kitu kinachoelekeza kitu fulani halisi ambacho kitakachokuja. Sabato ilikuwa ikiashiria pumziko halisi ambalo Bwana Yesu amekuja kuwapa watu duniani, na ndiyo sababu ya Yeye kujiita Bwana wa pumziko (sabato) (Luka 6:5) akimaanisha kuwa Yeye ndiye mtoa pumziko. Roho Mtakatifu kupitia Mtume Paulo, amefafanua katika kitabu cha Wakolosai kuwa, sabato ilikuwa ni kivuli cha mambo yajayo. Sabato ilikuwa siyo kitu halisi na ndiyo maana mtu akisha pata kitu halisi hawezi tena kung’ang’ania ishara au kivuli (negative). Wakolosai 2:16-17 inasema, “Basi, mtu asiwahaukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo."
Tumefika mwisho wa sehemu ya Tano, na sasa tutaenda SEHEMU YA SITA.
JE, UNAZIFAHAMU IDADI YA SABATO AMBAZO WANA WA ISRAELI WALIAMRIWA KUZISHIKA NA MALENGO YAKE?
**********USIKOSE SEHEMU YA SITA***********
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.
www.maxshimbaministries.org

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW