Sunday, October 23, 2016

NENO LA MUNGU LINASEMA NINI KUHUSU SABATO? (SEHEMU YA NNE)


Ndugu msomaji, katika Sehemu ya Tatu tulijifunza mengi kuhusu Mafarisayo na nini walisema kuhusu Siku ya Sabato.
Kumekuwa na watu ambao wanasema kuwa wanaitunza Sabato, lakini ukichunguza kwa undani, kwa kweli hawaitendei kazi Sabato kabisa bali wanaivunja kwa kiwango kikubwa sana.
Je, unafahamu kuwa, ukitembea zaidi ya Maili Moja siku ya Sabato, unakuwa umeivunja Sabato?
Kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba. (Kutoka 16:29).
Kulikuwa na kiasi kinachoruhusiwa cha mtu kutembea inapofika siku ya sabato (Matendo 1:12). Ilikuwa ni makosa kwa mtu kwenda mwendo unaozidi kiasi hicho.
Katika sheria ya Sabato ilikuwa hairuhisiwi kabisa mtu kutembea nje ya mwendo wa Sabato. Mwendo wa Sabato ulikuwa chini kidogo ya maili moja ambao urefu wake ulikuwa ni kama kutoka Bithania kwenda Yerusalemu (Luka 24:50; Matendo 1:8-12) lakini leo wako watu wanajiita Wasabato wanatoka nyumbani kwao, labda kwao ni Temeke wanakwenda kanisani Ubungo au Kimara siku ya Jumamosi, wakati kutoka Temeke mpaka Ubungo ni zaidi ya maili moja mwendo ambao unakuwa umepita mwendo wa Sabato.
Katika Torati mtu ukipata yote lakini ukikosa katika jambo moja unahesabika kukosa juu ya yote (Yakobo 2:10).
Sasa, wewe Msabato unae enda Kanisa lilipo Zaidi ya maili moja, si umesha ivunja Sabato yako? Kwanini unapoteza muda wako na kulilia au ng’ang’ania sheria ambazo ni dhaifu na hazikusaidii kitu?
Zaidi ya hapo, katika sheria ya Sabato ilikuwa mtu akivunja Sabato alitakiwa kupigwa mawe mpaka kufa, leo mbona watu wakivunja Sabato hawapigwi mawe mpaka kifo (Hesabu 15:32-36)?
Ukiwauliza Wasabato, kwanini hawapigi mawe watu mpaka kifo, watakuambia kuwa sasa hivi tuko katika kipindi cha neema, sasa kwenye eneo la kupiga watu mpaka wafe kwa kuivunja Sabato ndio tuko kwenye kipindi cha neema lakini katika mengine bado tuendelee na maagizo ya agano la kale, huu ni utoto wa kimaandiko.
Jambo jingine kama tunaendelea na maagizo ya agano la kale kwa hoja kuwa eti Yesu hakuja kuivunja Torati wala manabii bali kuitimiliza, basi kama ni hivyo tunatakiwa pia tuendelee na kuchinja wanyama kwa ajili ya msamaha wa dhambi kama ilivyokuwa katika agano la kale, (Walawi 5:5-6;7-10; Walawi 6:1-7)
Ndugu msomaji ambaye wewe ni Msabato, umesha jiuliza swali hili? Kwanini mnachagua kutunza siku tu na mengine ya Sheria za Musa hamyafuati? Watunza Sheria wakati wa mtume Paulo waliotetea sheria na waliojitahidi sana kwa ajili ya torati ya Musa, walitoa hukumu kubwa sana kwa Wakristo walio fuata mafunzo ya Yesu. Wasabato wa wakati huo/MAFARISAYO walimshitaki mtume Paulo kwa kufundisha kinyume na sheria za Musa, eti, wanadai kuwa Mtume Paulo alifundisha uongo na au alifundisha kuvunja sheria za Musa. Je, haya madai ni kweli?

Paulo anataja watu hao, “…Kwa nini tusiseme kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo, na tufanye mabaya ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.” (Warumi 3:8). Katika Kanisa lililo anza wakati wa Agano Jipya, yanapata shida sana kutoka Wasabato kwasababu ya kuhukumiwa kutenda shambi au kuvunja sharia za Musa kwa kuamua kuishi kwa Imani na neema ya Yesu na sio kuishi chini ya torati/sharia. Hii ndio sababu kumbwa ilimfanya Mtume Paulo kufundisha kwa undani Zaidi jinsi ya kuishi katika neema ya Yesu Kristo. Ukisoma nyaraka zake, utapata mafunuo makubwa sana.
Kumbe ndio maana hata hii leo Wasabato wanatulaumu watumishi wa Mungu kama “Max Shimba Ministries” eti tunapotosha watu, kumbe hii tabia ya MAFARISAYO ilikuwepo tokea wakati wa Mtume Paulo! Hata siku hizi! Wasabato ningependa mtambue kuwa, sisi hatupo tena chini ya Sheria za Musa bali tupo chini ya Neema ya Yesu Kristo. Hii ndio kazi aliyo fanya Yesu Kristo kwa kutupa Agano Jipya. Hii tabia na au hali ya kushika Sabato imewafanya watu wengi kuwa VIPOFU NA VIZIWI WA NENO LA MUNGU. “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?” (Warumi 6:1, 2). Kwa nini wale wanaojitahidi kwa ajili ya torati hawaelewi tunayoyasema? Paulo anaendelea kwa kusema, “Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!” (Warumi 6:15). Kwa nini hawayaelewi hayo? Ukweli ni kinyume cha wanavyodai! Paulo asema tena, “Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.” (Warumi 6:14). Unaona? Dhambi haitatutawala sisi! Kwa nini? Kwa sababu ‘hatuwi chini ya sheria’ – bali chini ya neema! Ina maana kama mtu akiishi chini ya sheria, dhambi inamtawala! Watu wengine hawaelewi kuwa kuishi ‘chini ya sheria’ – maana yake sheria haiwezi kutakasa, kuhuisha, wala kutuweka huru mbali na dhambi. Wanafikiri, ‘Usipokuwa chini ya sheria, unaweza kufanya dhambi’, na wanashtuka! Kama vile hawajawahi soma au kusikia Injili isemayo! Tunaokolewa kwa neema na tunaishi kwa imani, siyo kwa torati ya Musa. Je, ina maana tunao uhuru kutenda dhambi? Hasha! Je, kwa nini watu haelewi maneno ya Paulo anasemapo, “Basi, je! twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? La hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.” (Warumi 3:31)
ADHABU YA KUVUNJA SABATO
Mtu ambaye aliasi sheria ya Sabato, adhabu yake ilikuwa ni kuuawa.
Maandiko yanasema: Kila mtu atakayefanya kazi yoyote siku ya Sabato, hakika yake atauawa. (Kutoka 31:15b).
JE, WEWE UNAYE ITUNZA SABATO, UMESHA WAI FANYA HAYA MAMBO:
1. Kufanya biashara
Tena wakakaa humo watu wa Tiro, walioleta samaki, na biashara za kila namna, wakawauzia wana wa Yuda siku ya sabato, na mumo humo Yerusalemu. Ndipo nikagombana na wakuu wa Yuda, nikawaambia, Ni neno baya gani hili mnalofanya ninyi, na kuinajisi siku ya sabato? (Nehemia 13:16-17).
2. Kubeba mizigo
Bwana asema hivi, Jihadharini nafsi zenu, msichukue mzigo wowote siku ya sabato. (Yeremia 17:21).
Ndiyo maana Bwana Yesu alipomponya mtu aliyekuwa hawezi kwa muda wa miaka thelathini na nane na kumwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. (Yohana 5:8), Wayahudi walipomwona mtu huyo walimwabia, Leo ni siku ya sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro. (Yohana 5:10).
3. Kukusanya kuni
Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwapo jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya sabato ... wakamleta kwa Musa ... BWANA akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa. (Hesabu 15:32-35).
4. Kuwasha moto/kupika
Hamtawasha moto katika nyumba zenu kwa siku ya Sabato. Hii ina maana kwamba haikuruhusiwa kupika vyakula siku ya sabato. (Kutoka 35:3).
5. Kutembea mwendo mrefu
Kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba. (Kutoka 16:29).
Kulikuwa na kiasi kinachoruhusiwa cha mtu kutembea inapofika siku ya sabato (Matendo 1:12). Ilikuwa ni makosa kwa mtu kwenda mwendo unaozidi kiasi hicho.
Kama ulifanya hayo mambo matano hapo juu, siku ya Sabato basi adhabu yako ni kupigwa mawe mpaka kifo.
Mtu ambaye aliasi sheria ya sabato, adhabu yake ilikuwa ni kuuawa.
Maandiko yanasema: Kila mtu atakayefanya kazi yoyote siku ya sabato, hakika yake atauawa. (Kutoka 31:15b).
Hetu tusome ni jinsi gani Sheria ilikuwa dhaifu kwasababu ya mwili: (Warumi 8:3,4) “Maana yale yasiowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu mwenyewe, kwa kumtuma Mwanawe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili haki (kwa tafsiri nyingine ‘maagizo’) ya torati itimizwe ndani yetu sisi Wakristo. (Warumi 8:3, 4)
Je, Sabato inaweza vunjwa?
Mwenye uwezo wa kuivunja Sabato ni yule yule aliye ileta Sabato. Hivyo basi, Sabato inaweza kuvunjwa. Je, Sabato ilivunjwa?
Aliyeahidi kuivunja Sabato ni Mungu mwenyewe aliyekuwa mbinguni ambaye aliahidi kuja duniani na kukanyaga ardhini (Mika 1:2-3).
Sasa Mungu huyu aliyeifanya Sabato na kuiagiza kwa wanadamu huyu ndiye aliyekuja kuivunja Sabato. Angalia andiko hili kwa makini (Yohana 5:2-9, 18) Katika Agano la Kale sheria ya Sabato ilikuwa haitakiwi kubeba mzigo wowote, angalia andiko hili (Yeremia 17:21) kwa hiyo mtu yeyote aliyebeba mzigo alihesabika kuivunja Sabato.
Hebu tumsome Yesu kidogo: Yesu anamwambia mtu yule aliyemponya kuwa ajitwike godoro lake aende na alimwambia mtu huyo ajitwike godoro lake aende siku ya Sabato. Je, kwanini Yesu alimwambia yule mtu abebe mzigo, huku akifahamu kuwa katika siku ya Sabato kubeba mzigo ilikuwa ni kosa na kinyume cha sheria za Musa? Je aliitunza Sabato au aliivunja?
Sasa, kama Yesu aliivunja Sabato, yeye pia anatuambia kuwa, “jitieni nira yangu mjifunze kwangu kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo” (Mathayo 11:29). Je, na mimi nikifanya alicho fanya Yesu si nitakuwa nimeivunja Sabato kwa kufuata fundisho lake katika Mathayo 11 aya ya 29?
Je, inamaanisha kuwa kama Yesu aliivunja Sabato na sisi tunapaswa kuivunja kwani anatuambia tujitie nira yake na tujifunze kwake katika Mathayo 11 aya ya 29.
Kumbe ndio maana Yesu Kristo alishindana sana na Wayahudi kuhusu suala la kuishika Sabato (Mathayo 12:1-8). Sasa, kama Yesu aliitunza Sabato, kwanini Wayahudi walimhukumu?
Hapa tunaona waziwazi jinsi ambavyo Yesu anavyowatetea wanafunzi wake kuhusu kuvunja masuke siku ya Sabato. Maana kuvunja masuke pia ilihesabika kuwa ni kufanya kazi na katika Agano la Kale.
Hakuna sababu yoyote iliyokubaliwa kuvunja Sabato hata kama sababu hiyo ilikuwa ni njema bado mtu huyo alihesabika kuivunja sabato, isipokuwa kwa amri ya Mungu kama kutoa sadaka (Hesabu 28:9).
Lakini hapa Yesu anaivunja Sabato kwa kuhalalisha kuwa ni halali kufanya kazi hiyo ya kuvunja masuke, kitu ambacho katika agano la kale mtu angeuawa kwa kupigwa mawe kama tulivyoona kwa mwanamke huyu (Hesabu 15:32-36).
Tumefika mwisho wa sehemu ya Nne, na sasa tutaenda SEHEMU YA TANO.
Je, unafahamu kuwa kama wewe ni MSABATO NA UKIVAA NGUO YENYE RANGI RANGI UNAKUWA UMEVUNJA SABATO? ……….. hapo sasa……
**********USIKOSE SEHEMU YA TANO***********
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW