Ni siku gani ya Sabato, Jumamosi au Jumapili? Je, Wakristo wastahili kuitunza hii siku?
Sabato (kwa Kiebrania: שבת, shabbāt, yaani pumziko kwa Kiswahili) ni siku ya pumziko ya kila juma katika Uyahudi kwa ujumla na hasa katika nchi ya Israeli.
Kumekuwa na maswali mengi sana kutoka imani tofauti kuhusu hii siku ya Jumamosi. Wafuasi wa dini na imani zote wanao fuata Torati wanajiuliza kuhusu Sabato, je, Mwenyezi Mungu anaikubali Jumamosi tu kama siku ya ibada? Katika Agano Jipya, tunajifunza kuwa siku ya Jumapili inaitwa siku ya kwanza ya juma na walio amini walikusanyika katika siku hii ya Jumapili. Matendo 20: 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
Siku ya kwanza ya juma ni Jumapili na hii ni siku ambayo walio mwamini Yesu walikusanyika na kuabudu. Huu ni ushaidi wa kuonekana kwa macho ambao Wakristo wanaabudu Jumapili tokea Karne ya kwanza.
“Hata sabato ilipokwisha, kupambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.” (Mathayo 28:1). “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma…”. (Marko 16:9).
Bwana Yesu alifufuka kutoka wafu katika siku ya kwanza ya Juma. Zaidi ya hapo, tumesoma nyaraka za Mtume Paulo zikionyesha kuwa kuwa Wakristo wa kwanza walikuwa walikusanyika siku ya kwanza ya Juma, yaani Jumapili. “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kuumega mkate, Paulo akawahutubu…” (Matendo 20:7). “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja…” (1 Wakor.16:2).
Zaidi ya hapo, hatusomi na wala hakuna amrisho ndani ya Agano Jipya kuhusu wauminia yaani Wakristo ni lazima wakutane kwenye hii siku ya kwanza ya Juma, “Jumapili”, lakini tunao mfano wa siku ambayo Wakristo wa kwanza “Kanisa la Kwanza wakati wa Pentekoste”, na utamaduni huo wa kuabudu Jumapili unaendelea mpaka sasa. Zaidi ya hapo, ukisoma Agano Jipya kwa umakini utaona kuwa WAKRISTO WA KWANZA HAWAKUKUSANYIKA SIKU YA SABATO, nikimaanisha kuwa, hakuna aya ambayo inasema moja kwa moja kuwa Wakristo walikusanyika siku ya Sabato au kulikuwa na utamaduni au desturi au mila au sheria inayo walazimisha kukutana siku ya Sabato.
Bali wengine wanadai kuwa agizo la Constantino katika mwaka wa 321 A.D (Baada ya Yesu kuzaliwa) ilibadilisha sabato kutoka Jumamosi hadi Jumapili. Ni siku gani kanisa la kwanza lilikutana kwa ibada? Bibilia haitaji mkusanyiko wowote wa sabato (Jumamosi) kwa waumini kwa minajili ya ushirika au ibada. Ingawa, kuna kurasa wazi zinazoitaja siku ya kwanza ya juma. Kwa mfano Matendo Ya Mitume 20:7 ambayo yasema, “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokutana ili kumega mkate.” Katika 1 Wakorintho 16:2 Paulo anawasihi Wakristo wa Korintho, “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadri ya kufanikiwa kwake.” Jinsi Paulo anayataja haya matoleo kuwa “huduma” katika 2 Wakorintho 9:12, haya matoleo lazima yamehuzishwa na ibada ya siku ya Jumapili ya Wakristo. Kiistoria siku ya Jumapili, bali si Jumamosi ilikuwa siku iliyokubalika kwa Wakristo katika kanisa na matukio yao yaweza kufuatwa hadi wakati wa kanisa la kwanza.
Wapinga Ukriso na dini zingine kama Waislam wanaihusisha siku ya Jumapili na waabudu JUA, kwa kufanya tafsiri ya neno la Kiingereza ‘Sunday’ – WANALIGAWA NENO “SUNDAY” KWA KUTENGANISHA SUN AND DAY, SUN = JUA NA DAY = SIKU Na kuja na jibu kuwa wale wote wanao abudu Jumapili basi wao wanamwabudu Mungu JUA, ingawa tuna uthibitisho tosha kuwa Wakristo wa kwanza walimwabudu Yesu ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na SIO MUNGU JUA kama wanavyo dai. Ili kufahamu kwanini kuna siku hizi za wiki na maana yake, ni vyema kuangalia msingi wa hizi siku na jinsi walivyo ziweka. MFANO: Tuiangalie siku ya JUMAMOSI ambayo kwa Kiingereza ni SATURDAY, je, hili jina walilipataje? Kutokana na Warumi siku hii ya SATURDAY iliitwa kutokana na SAYARI YA ZOHALI yaani (dies Saturni) kwa sababu Warumi wa wakati huo waliheshimu sayari Zohali. SASA KAMA TUKITUMIA UTAALAMU HUO HUO WA KUHUSISHA SIKU NA IMANI AU DINI, JE, INAMAANISHA KUWA WASABATO “SDA” WAO WANAAMINI NA AU ABUDU SAYARI YA ZOHALI?
Ndugu msomaji, nimeamua kufundisha hili somo kwa kujibu maswali mengi sana yanayo ulizwa na Wasabato kwanini tunaabudu Jumapili na kutuhukumu kuwa tunavunja sheria za Musa. “Mosaic covenant/laws”
Hivyobasi, leo nakuacha hapa kwa kukukumbusha kuwa Wakristo wa kwanza waliabudu siku ya Jumapili na hakuna aya yeyote ile kutoka Biblia inayosema kiuwazi kuwa WAKRISTO WALIKUSANYIKA SIKU YA JUMAMOSI.
Sasa soma aya hizi hapa chini kwa ufasaha:
Warumi 14.5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Ndugu zanguni, kutokana na Warumi 14, tumewekwa huru kuchagua siku ya kuabudu, na nini tule au tusile, hivyo hivyo ni kuadhimisha kwa Bwana. Hivyo basi, hakuna kosa lolote lile mtu anapo sali Jumamosi au Jumapili au Jumatatu, au siku yeyote ile ya wiki. Mungu wetu yupo kila siku na siku zote alizumba yeye.
Matendo ya Mitume 2: 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Unaona hiyo aya hapo juu inavyo sema? Je, Jumatatu imekosekana kwenye hiyo aya, vipi kuhusu Jumanne? Ndio maana nilisema sisi tumewekwa huru kutokana laana ya sheria na sasa tupo huru kuabudu Mungu siku yeyote ile. Mungu si wa Jumamosi tu au Jumapili tu au Ijumaa tu. Mungu ni wa kila siku.
KWANINI UNAPENDA MAFUNZO AMBAYO NI DHAIFU?
Wagalatia 4:8 Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu. 9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? 10 Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.
Mtume Paulo anatukumbusha kuwa, mafunzo ambayo tulikuwa tunayafuata kabla ya kukombolewa na Yesu yalikuwa dhaifu. Sasa tumejazwa na Roho Mtakatifu ambaye ndie Mwalimu wetu Mkuu. Basi tushikamane naye na tujifunze kutoka kwake.
USIKOSE SEHEMU YA PILI ……………………………… “Kwanini Bwana Yesu aliingia kwenye Sinagogi siku ya Jumamosi “SABATO”? …………………….
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.
No comments:
Post a Comment