SOMO:AINA ZA UCHAWI KATIKA UISILAMU
i. Habize/Hepatoscopy(huu ni uchawi wa kutumia maini) Ezekiel21:21 Uchawi huu unakuwa hivi, mchawi anatuma kuku nyumbani kwako, huyo kuku anakuwa anasumbua sana anakula chakula nyumbani mwako anasumbua sana ukimfukuza anarudi, mwisho wake huyo mchawi anamchukua Yule kuku anamchinja na kusoma kwenye maini yake matukio yote yaliyokuwa yanaendelea nyumbani kwako kwa kutumia maini hayo. Yaweza kuwa mnyama yeyote sio lazima awe kuku, yaweza kuwa nguruwe, mbuzi au mnyama yeyote,
ii. Ngote/Hydromacy(huu ni uchawi wa maji) unarogwa kupitia maji; anaekuroga katika njia hii anaweka maji kwenye kitu chochote chaweza kuwa kikombe, dishi na kadharika, mchawi anamwita mtu anaemtaka harafu anatokea juu ya maji harafu anakuchoma kisu au ngumio au silaha yeyote mwishowake anakuuwa.
MWANZO44:5” je kikombe hicho sicho anyweacho bwana wangu? Nae hufanya uaguzi……” MWANZO44:15.
iii. Gagoo/Rhabdomancy (huu ni uchawi wa fimbo, gongo, mishale, mikuki} HOSEA 4:12 “watu wangu hutaka shauri kwa gongo lao na fimbo yao huwahubiri mambo….” Hizi ni ramri za gongo na fimbo au mishale, na kwa kutumia hivyo vitu anauwezo wa kusoma kila kitu katika mahali anapopita na kujua uzito wa watu wa eneo hilo na akishajua, atajua maneno gani achague ya kuongea na watu wake. Mwingine anapita na mkuki anachoma chini kama hatua kadhaa harafu anarudi nyumbani huku ananuizia maneno kuwa kila atakae kanyaga sehemu zile mkuki ulimopita basi mtagawana hela yeye mchawi na wewe; hii inakuwa hivi kama unahela unaenda dukani unanunua kitu kidogo ili uichenji ile hela harafu ukirudisha chenji mfukoni zinapotea, kama hauna hela basi unakufa. Uchawi wa fimbo na gongo huu unakuwa hivi mtu anatembea na fimbo akifika kwenye mtu mwenye hela ile fimbo inaongea harafu huyo mtu anadhurumiwa. EZEKIEL21:21, mfalme wa babeli ambayo leo hii inaitwa Iraq alisimama njia panda akatikisa mishale huko na huko, waganga wa kienyeji nao hutikisa mishale.kama ni hela isiyogawanyika basi kinachozidi kinazidi kwake; hii inamaana kuwa kama unamiambili hamsini basi mia hamsini itaenda kwake na mia itakuja kwako.
iv. Monka/Teraphim ( huu ni uchawi ambao hutumika kwenye vinyago ama vitu visivyo na uhai vinapewa uhai na kuweza kusogea kwa muda) yaani hii inamaanisha kuwa mchawi anaweza kuweka uchawi kwenye kitanda na kitanda kikatembea au kikakurusha na baadae kikarudi kwenye hari yake ya kuwa kitanda.
Au ukapita sehemu Fulani nguzo ya umeme inakuangukia au kinyago kinakuongelesha. ZEKARIA 10:2” kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili….” EZEKIEL21:21”maana mfalme wa Babeli alisimama kwenye njia panda……”
v. Kerumo/astrology(nyota} ISAYA 47:13”umechoka kwa wingi wa mashauri yako….” Huu ni uchawi maarufu sana kwa kuwa uchawi huu huandikwa hata kwenye magazeti. YEREMIA 10:2. Waganga huwa wanaangalia kwenya anga pindi ifikapo jioni, anaweza akakuta wingu limekaa kama mkono basi hapo kuna tafsiri yake, au anaweza akatazama kwenye nyota akaona mwezi unaonekana katika muonekano gani basi hapo napo atapata maana Fulani. EZEKIEL21:22- uchawi huu mbaya sana kwasababu kama ni biashara atauza yeye jirani yake hatauza kabisa. Yaani mchawi anaweza akaroga mtaa mzima wakamfuata yeye tu, yaani biashara yake inaonekana ni nzuri sana.
Barikiwa sana
No comments:
Post a Comment