Wednesday, October 12, 2016

BIBLIA INAKATAZA ULEVI

Je, Bibilia Ya Sema Nini Kuhusu Ulevi?
Bibilia yalinganisha ulevi na upumbavu (Mithali 26:9) na inapeyana onyo hili: Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema wakikimbilia kunywa vileo, wale wakawiao sana mpaka usiku, mpaka wamewaka kwa mvinyo. (Isaya 5:11). Ole wake yeye ambaye jirani yake kileo, akiimimina kutoka kwenye kiriba cha mvinyo mpaka wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi. (Habakkuk 2:15).Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo nao walio hodari katika kuchanganya vileo, (Isaya 5:22).
Amkeni, enyi walevi, mlie!
Pigeni yowe enyi wanywaji wote wa mvinyo, (Joel 1:5).
Mtume Paulo aliwaonya watu ya kuwa hakuna mlevi atakaeingia katika Ufalme wa Mungu (1 Wakoritho 6:10). Ulevi ni kitendo cha kawaida cha utu alisi wa dhambi hakuna awayeyeyote aishie
katika njinsi hii atakae urithi ufalme wa mungu (Wagalatia 5:19-21).
“DIVAI ni mdhihaki, kileo husababisha msukosuko, na kila mtu anayepotezwa nacho hana hekima.” Je, andiko hilo la Biblia linalopatikana katika Methali 20:1, linaonyesha kwamba ni vibaya kunywa kileo? Wengine wanafikiri hivyo. Ili kuthibitisha hilo, wao hutaja masimulizi ya Biblia ambapo watu walifanya mambo mabaya kwa sababu ya matumizi mabaya ya kileo.—Mwanzo 9:20-25.
Maandiko yana ilani nyingi juu ya kunywa kileo (Mambo ya Walawi 10:9; Hesabu6:3; Kumbukumbu la Torati 29:6; Waamuzi 13:4,7,14; Samueli wa kwanza 1:15; Methali 20:1; 31:4,6; Isaya 5:11;22; 24:9; 28:7; 29:9; 56:12; Mika 2:11; Luka 1:15).

Biblia inaonya kuhusu matokeo mabaya ya kunywa kileo kupita kiasi. Waefeso 5:18 inasema: “Pia, msiwe mkilewa divai, ambayo ina upotovu ndani yake.” Vilevile, Methali 23:20, 21 inahimiza hivi: “Usiwe kati ya watu wanaokunywa divai mno, kati ya watu wanaokula nyama kwa ulafi. Kwa maana mlevi na mlafi watakuwa maskini.” Na Isaya 5:11 inasema: “Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema ili watafute tu kileo, wanaokawia mpaka giza la jioni sana hivi kwamba divai inawawasha!”
Kile Mungu anachowaamuru Wakristo juu ya kileo ni wajizuie na ulevi (Waefeso 5:18). Biblia inakataza ulevi na athari zake (Methali 23:29-35). Wakristo wanakatazwa kuachilia miili yao itawalwe na vitu vinginevyo. (Wakorintho wa kwanza 6:12; Petro wa pili 2:19). Kunywa kileo kingi kunaathiri mtu. Maandiko yanakataza chochote kile ambacho kwa kukifanya unasababisha wengine kujikwaa (Wakorintho wa kwanza 8:9-13). Kwa mujibu wa haya ni vigumu mkristo kukiri kuwa anakunywa kileo kwa utukufu wa Mungu (Wakorintho wa kwanza 10;31).
Mungu anatuamuru kuwa tusiwe walevi (Waefeso 5:18) Kwa wakati pia Mungu atuamuru tukane kabisa vinywaji vizito. Kama ilivyo kwa wachungaji (Mambo ya Walawi 10:9) Sheria za wanazareti (Hesabu 6:3) Hekima ya waongozao (Mithali 3:4) Nabii Danieli (Daniel 1:8) Yohana mbatizaji (Luka 1:15) Waumini wote katika hali tofauti tofauti (Warumi 14:21)
Kama umekuwa mlevi fungua moyo wako kwa Mungu mfalme kisha uombe ombi hili “ Mfalme wa mbingu na nchi naja mbele yako kwa jina la Yesu kristo.
Natubu dhambi zangu. Nakiri kwamba nimekosa mbele yako na nimeharibu maisha kwa ajili ya pombe Naomba unisamehe na unisafishe. Namchukua Yesu kama mfalme na mkombozi kwa
njia ya imani kupitia kwa damu yake. Nguvu za dhambi zimevunjwa .
Nakuhitaji kwa ukombozi. Nakemea roho wa ulevi na kuzivunja nguvu za kishetani, huku nikijuwa kwamba neno la Mungu lasema “Jisalimishe kwa Mungu.
Mkatae shetani na atakutoroka (Yakobo4:7) Asante kwa kunipa
ukombozi na neno lako lihimidiwe milele na milele. Amina.”
Kwa sababu umekuwa mkristo, umezaliwa tena kupitia kwa roho
mtakatifu, yafaa ukomae katika uhusiano wako na Mungu.
Yafaa ujifunze kuisikia sauti ya Mungu na ufuate njia zake:
1). Soma Biblia
2). Omba na uongee na Mungu moyoni mwako
3). Batizwa na ujiunge na Kanisa linalompendaza Yesu kristo.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW