ALLAH ANAWACHUNGA WAHALIFU. KUMBE ALLAH NI MCHUNGAJI
Quran 19:86 Na TUKAWACHUNGA wakhalifu kuwapeleka Jehanamu.
Kumbe Allah ni MCHUNGAJI wa wakhalifu "WAISLAMU" wanaochungwa na Allah ili awapeleke Jehanamu!!
Ufafanuzi wa aya hiyo Qur'an iliyotafsiriwa na Shekhe Baruan,
Inasema: 19:86 Na tutawachunga wakosefu kuwasukumia Jehanamu nao wamebanwa na kiu, kama wanavyochungwa wanyama kwenda kwenye maji.
Inasema: 19:86 Na tutawachunga wakosefu kuwasukumia Jehanamu nao wamebanwa na kiu, kama wanavyochungwa wanyama kwenda kwenye maji.
Allah sasa anateremsha aya kuthibitsiha kuwa Waislam ndio WAHALIFU watakao ingia Jehannam.
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.
Kumbe Allah ni mchungaji wa Wahalifu. Kumbe Waislam ndio wahalifu wanao chungwa na Allah ili waingie Jehannam. Je, Jehovah anayo sifa hii ya Allah au hana.
Ebu tusome Biblia.
YESU NI MCHUNGAJI MWEMA
Waislam msikilizeni Mchungaji huyu hapa. Yohana 10:11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Yesu Kristo, Mchungaji Mwema, alifundisha:
“Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kwenda nyikani, aende kumtafuta yule aliyepotea hata amwone? …
“Nawaambia, vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye” (Luka 15:4, 7).
Tunapokuja kuelewa kwamba Yesu Kristo ndiye Mchungaji Mwema, hamu yetu huongezeka kufuata mfano Wake na kuhudumia walio na mahitaji. Yesu alisema: “Mimi ndimi mchungaji mwema, nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo” (Yohana 10:14–15). Kwa sababu ya Upatanisho wa Kristo, hakuna yeyote miongoni mwetu atakayewahi kuwa amepotea sana kwamba hatuwezi kupata njia yetu kwenda nyumbani. (ona Luka 15).
Yesu Kristo, hapa anajitambulisha kwetu kama Mchungaji mwema anayeutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Daudi, kama mchungaji wa kondoo, aliwalinda sana kondoo wake. Alipokuwa akija simba, au dubu na kumkamaa kondoo, Daudi alimfuata na kumpiga na kumpokonya kinywani mwake, kwa ujasiri mkubwa (1 Samweli 17:34-35). Yesu Kristo, alikuja kwetu kama Mwana wa Daudi (Marko 10:46-52). Daudi, alikuwa mfano tu wa Yesu Kristo. Yesu Kristo, ni Mchungaji mwema kuliko Daudi. Shetani kama simba aungurumaye, anapotujia na kutukamata na kutaka kutumeza, hatuna haja ya kubabaika, bali tuliitie Jina la Yesu Mchungaji Mwema na Yeye atatuokoa mara moja. Kama kondoo wa Mchungaji mwema Yesu Kristo, hatupaswi kuogopa mabaya. Tukiwa na Yeye, na kumtumaini katika maisha yetu, hatutapungukiwa na kitu (Zaburi 23:1-6). Mchungaji Mwema Yesu Kristo, aliyekuwa tayari hata kuutoa uhai kwa ajili yetu pale msalabani, anatujali sana kututakia mema, kuliko wengi wetu tunavyowaza. Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuifahamu kweli hii (1 Petro 5:7).
Leo tumeona tofauti ya Mchungaji Allah anaye peleka watu Jehannam na Yesu Mchungaji mwema.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment