Wednesday, October 5, 2016

ALLAH SIO YEHOVA "YAHUH" ( يهوه ) MWENYEZI MUNGU (SEHEMU YA TISA)



JE, MJI ALIOUCHAGUA ALLAH NI KAMA NA ALIOUCHAGUA MUNGU WETU WAKRISTO?
Je, Mji wa Allah unaitwaje?
Quran 27 au surat An-Naml 91 (sisimizi/mchwa/wadudu chungu)
Bila shaka nimeamrishwa nimuabudu mola wa mji huu (wa Makka) ambaye ameutukuza na ni vyake tu (Mwenyezi Mungu) vitu vyote…
Quran 3 au Surat Aal-Imran 96 (watu wa Imram)
Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyo Makka yenye baraka na uwongozi kwa ajili ya walimwengu wote.
Quran 106 au Surat Quraysh 3-4 (Makureshi-kabila)
Basi nawamuabudu Bwana wa nyumba hii (Al-ka'ba) Ambaye anawalisha (wakati Waarabu wenzi wao wamo) katika njaa na anawapa amani wakati wenzi wao wamo katika khofu. Hivyo tunaona kuwa Allah ndiye bwana wa Al-ka'ba kadiri ya aya hii na Al-ka'ba iko katika Makka. Kupitia aya hizi tunaona Allah mungu anayeabudiwa na Waislamu amechagua mji wa Makka kuwa ndio mji wake mtakatifu na tena Muhammad (s.a.w) aliamrishwa amuabudu mola wa mji huo wa Makka ambaye ndiye Allah.
Je, Mungu wetu aitwae Yehova alichagua mji gani? Endelea..
Mji aliouchagua Mungu wetu Yehova ni huu..
2 Nyakati 6:4-6,
Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza kwa mikono yake, akasema, Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wowote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu yeyote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo, na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli.
Maandiko hayaelezi mji mwingine wowote aliouchagua Mungu wetu hapa duniani bali ni mji wa Yerusalemu tu.
2 Nyakati 12:13, Ezra 6:12; 7:15,27; Zaburi 26:8; Zakaria 2:12
Kupitia aya hizi tunaona Mungu wetu Yehova, mji wake aliouchagua niYerusalemu. Neno Yerusalemu ni la lugha ya Kiebrania na maana yake ni "chimbuko la amani". Hata Waisraeli walipokuwa mbali na mji wa Yerusalemu bado walipiga magoti na kuelekeza nyuso zao Yerusalemu. (Tazama Danieli 6:10). Mji aliouchagua Yehova ni Yerusalemu, na mji aliouchagua Allah ni Makka. Na hii ndio tofauti ya mji wa Allah na Yehova.
Kumbe Yehova Mwenyezi Mungu sio Allah wa Waislamu.
Max Shimba Ministries Org.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW