Sunday, October 9, 2016

AJILIPUA NDANI YA MSIKITI SAUDIA


Mlipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua ndani ya msikiti wa madhehebu ya Shia katika mkoa wa mashariki wa taifa la Saudi Arabia na kusababisha madhara makubwa.
Kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Mtu mmoja aliyeshuhudia alikiambia chombo cha habari cha Reuters kwamba kulikuwa na mlipuko mkubwa katika msikiti wa Imam Ali katika kijiji cha al-Qadeeh.
Amekadiria kwamba kuna majeruhi 30 katika shambulizi hilo ambapo zaidi ya watu 150 walidaiwa kusali ndani ya msikiti huo.
Picha za runinga ya kundi la Hezbolla al-Manar zilionyesha vioo vilivyovunjika pamoja na vifusi ndani ya msikiti.
Miili iliozibwa na nguo ilionekana imetapakaa katika sakafu ya msikiti huo.
Watu wa dhehebu la Shia walio wachache wanaishi mkoa wa mashariki na kumekuwa na malalamishi ya washia wanaotaka kupewa haki zaidi.
Hili ni shambulizi la kwanza lililotekelezwa katika msikiti wa Shia.
Tukio hilo linajiri huku muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ukiendeleza kampeni yake dhidi ya waasi wa kishia katika taifa jirani la Yemen.
Taifa la Saudi Arabia pia limetishwa na Islamic state ambalo linalengwa na muungano wa kimataifa iwemo ufalme huo wa kisunni.
Source: Al Arabiya

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW