Wednesday, September 28, 2016

ROHO MTAKATIFU NI MUNGU


Ndugu msomaji; 
Je, unamfahamu Roho Mtakatifu?Je, Roho Mtakatifu ni nani kwako? Katika kijarida hiki kifupi, ningependa tumzungumzie Roho Mtakatifu kama alivyo semwa na kutajwa katika Biblia Takatifu. Kuna utatanishi mkubwa sana na maelezo mengi sana kuhusu Roho Mtakatifu. Kuna imani zingine kama Mashahidi wa Yehova, wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Nguvu Fulani na au ni uwezo wa Mungu katika kufanya mambo. Wengine kama Waislamu, wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Malaika Gabriel. Wengine husema kuwa Roho Mtakatifu ni sehemu ya Nafsi ya Mungu. Lakini, Biblia inasema nini kuhusu Roho Mtakatifu. Ni vyema tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu kwa kutumia aya za Biblia na sio theologia na akili zetu.
ROHO MTAKATIFU NI MUNGU
Tuanze kwa ushaidi wa aya: Matendo ya Mitume 5:3-4. Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata? 4 Kabla hujauza hilo shamba lilikuwa mali yako. Na hata baada ya kuliuza, fedha ulizopata zilikuwa zako. Kwa nini basi umeamua moyoni mwako kufanya jambo kama hili?
Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.” Katika aya hizo hapo juu, Petro anapambana na anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na anasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali Mungu. Kwa maana nyingine, Petro alikuwa anamwambia Anania kuwa, kumdanganya Roho Mtakayifu ni sawa na kumdanganya Mungu.
Huu ni uthibitisho wa kwanza kuwa, kumbe Roho Mtakatifu ni Mungu.
ROHO MTAKATIFU YUPO KILA MAHALI
Hebu tuangalie kama Roho Mtakatifu ana adhama za Mungu aliye hai. Sifa, moja ya Mungu ni kuwa, yeye yupo kila Mahali. Je, Roho Mtakatifu anayo hii sifa ya kuwa kila mahali? Fungua Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” Daudi anatuambia kwa kupitia Zaburi kuwa, huwezi kumkimbia Mungu.
Daudi anamtaja Mungu na au anamwita Mungu kuwa ni Roho. Hii sifa ya kuwa kila mahali ni ya Mungu pekee, na katika Zaburi 139: 7-8, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu yupo kila mahali. Tuendele na ushahidi zaidi wa kuwa kila mahali; katika Wakorintho wa Kwanza, hapa Mtume Paulo anasema yafuatayo 1 Wakorintho 2 aya ya 10 Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu.
Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake?
Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.” Kama Roho Mtakatifu anafahamu kila kitu kilicho ndani ya Binadamu, ambao wametapakaa Duniani kote, basi kitendo cha kuwa kila mahali kwa wakati mmoja ni Mungu pekee ndie aliye na huo uwezo. Tuendelee kwa Ushihidi mwingine katika aya hiyo hiyo ya 10 ya Wakorintho wa kwanza Sura ya 2. Roho Mtakatifu ni Mungu kwasababu ana akili, hisia, na mapenzi yake. Katika Wakorintho wa kwanza 2:10 tumesoma kuwa Roho Mtakatifu hufikiria na hujua siri iliyo ndani yako. Hii sifa ya kufikiria na kujua, inavunja hoja ya Mashahidi wa Yehova kuwa Roho Mtakatifu ni “Nguvu”. Nguvu haina uwezo wa kufikiria wala kufanya maamuzi.
ROHO MTAKATIFU UHUZUNIKA
Katika Waefeso 4:30 inasema “Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi” Unaweza jiuliza, ni kivipi unaweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu? Kama Roho Mtakatifu angekuwa ni “Nguvu –Energy” kama anaitwa na Mashahidi wa Yehova, je, ni kivipi Nguvu ipate huzuni?
Unapo tenda dhambi huku Roho Mtakatifu akiwa ndani yako kama alivyo fanya “Anania – Matendo ya Mitume 5:3-4” Unamhuzunisha Roho Mtakatifu maana yeye hujua yote na akuna siri ambayo haifahamu. Hii sifa ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu ina pinga madai ya Mashahidi wa Yehova na inapinga madai ya Waislam yanayo kama Uungu wa Roho Mtakatifu.
ROHO MTAKATIFU HUTUOMBEA
Warumi 8:26-27 Bibilia Takatifu (SNT)=12pt26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno. 27 Na Mungu ambaye ana chunguza mioyo yetu anafahamu mawazo ya Roho kwa maana Roho huwaombea watakatifu kufuatana na mapenzi ya Mungu.
Katika aya hapo juu, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu anatuombea na kutusaidia katika udhaifu wetu. Hii sifa ya upendo usio na kipimo ni ya Mungu peke yake. Zaidi ya hapo, tunasoma kuwa, Mungu anachunguza mioyo yetu kwa kupitia Roho Mtakatifu. Kumbe basi, Roho Mtakatifu anafahamu mapenzi ya Mungu kwako.
Hii sifa ya Roho Mtakatifu kuwa na uwezo wa kufahamu nini Mungu anawaza inamfanya Roho Mtakatifu na yeye awe Mungu. Hakuna mwenye uwezo wa kufahamu mawazo ya Mungu, isipokuwa Mungu.
ROHO MTAKATIFU HUFANYA MAAMUZI YAKE
Roho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11). =12pt1 Wakorintho 12:7-11=12ptNeno: Bibilia Takatifu (SNT)=12pt7 Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote. 8 Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha. 11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.
Katika Wakorintho wa kwanza hapo juu, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu ndie anaye toa zawadi/karama ya hekima, ufahamu, imani, kuponya, miujiza, unabii, nk. Hii sifa ya kutoa hizi Karama ni ya Mungu, lakini hapa kwenye Wakorintho tumesoma na kugundua kuwa, Kumbe Roho Mtakatifu ndie anaye toa hizi karama za Mungu. Hivyo basi, kwa kuwa Roho Mtakatifu ndie anaye toa hizi karama za Mungu, hufanya hivyo kwa kuwa yeye ni Mungu na hizo karama ni zake.
ROHO MTAKATIFU ANAFAHAMU MAMBO YOTE
Kama ambavyo Mungu anafahamu mambo yote na anaweza yote, vivyohivyo Roho mtakatifu ni Mungu na anauwezo wa huohuo wa kufahamu yote. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26). Yohana 14:26 Neno: Bibilia Takatifu (SNT) 26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Katika Yohana hapo juu, tunajifunza kuwa, Roho Mtakatifu yupo nasi kila siku na anaishi ndani yetu. Huu uwezo wa kuishi ndani yetu na kuwa kila mahali, na kufahamu yote ambayo Yesu aliyo tuambia na kutukumbusha, huu uwezo ni wa Mungu na unamfanya Roho Mtakatifu kuwa Mungu.
HITIMISHO
Roho Mtakatifuni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye pia anayo nafsi na kwa hiari yake ameamua kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu kwa kuzingatia mgawanyo wa majukumu waliyokubaliana yaani nafsi ya Mungu Baba, Mungu Mwana(Yesu) na Mungu Roho Mtakatifu.
Kazi/lengo kubwa la ujio wake ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu kwenye ulimwengu huu wa mwili, ili kumsaidia kuishi katika mapenzi ya Mungu.
Katika huduma yake Max Shimba Ministries
@February 10, 2015
New York, NY 10019

1 comment:

Unknown said...

What does science (scientists) say about the Holy Spirit?

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW