Friday, September 2, 2016

NINI MAANA YA KUUMBWA KWA MFANO WA MUNGU?

Mungu ni Roho. Je wewe ni nani?
Katika somo hili la uumbaji wa binadamu, nitajibu hoja na maswali mbali mbali ambayo yanaulizwa zaidi na waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidini, kupitia wahadhiri wao wa Dini, Waislamu wamekuwa wakipinga kuwa Mungu hana Mfano kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Mwanzo Sura ya Kwanza na aya ya 26.
Ndugu msomaji, nakusihi ufuatilie somo hili kwa makini ili ujue ukweli kuhusu kuumbwa kwa Binadamu kwa Mfano wa Mungu na nini maana yake:
Katika siku ya mwisho ya uumbaji, Mungu alisema, "Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu" (Mwanzo 1:26). Mungu alimuumba Mtu kutoka vumbi na akampa uhai kwa kumpulizia pumzi yake mwenyewe (Mwanzo 2:07). Binadamu ni kiumbe cha kipekee ambacho Mungu alikiumba na baada ya kukiumba, akatumia pumzi yake kukipa uhai, zaidi ya hapo, binadamu ni kiumbe pekee chenye Mwili, Roho na Nafsi.
Kuwa "mfano" wa Mungu maana yake, katika suala rahisi ni kwamba sisi hatufanani na Mungu katika maana ya mwili na sura na/au mwonekano wetu, bali sisi tunafanana na Mungu katika Roho. Maandiko yanasema kwamba "Mungu ni roho" (Yohana 4:24). Binadamu tuna Mwili, Roho, na Nafsi. Unaweza kuniuliza, ni kivipi ninaweza kuthibitisha hayo? Ngoja nikupe mfano mdogo. Mtu anapo kufa, huwa tunasema hivi: Huu ni Mwili wa Marehemu “Fulani”. Kwanini tunauita “MWILI WA MAREHEMU”…Fulani? Kwa kifupi ni kwamba, Yule ambaye alikuwa anaishi katika huo MWILI amesha ondoka na/au toka katika huo MWILI na kwenda sehemu nyingine. Kumbe basi Binadamu si Mwili, bali kuna zaidi ya MWILI.
Biblia inasema kuwa, Mungu alipo pulizia pumzi ya uhai ule udongo ambao aliuumba, huo udongo ukafanyika na ukawa kiumbe chenye uhai. Kumbe basi, kilicho fanya huo udongo kuwa kiumbe chenye uhai ni ile pumzi ambayo Mungu alipulizia ule udongo alio ufanya katika umbo la mtu. Hiyo pumzi ndio Roho ya Binadamu. Hiyo Roho ndio mfano halisi wa Mungu.

Sasa tuagalie zaidi maana ya Sura ya Mungu na inahusiana kivipi na sisi Wanadamu. Mtu ni tofauti na hafanani na Wanyama amboa hawana mamlaka juu ya vilivyo umbwa, nikimaanisha kuwa Binadamu alipewa Mamlaka katika kila kitu ambacho kipo hapa duniani (Mwanzo 1:28), na zaidi ya hapo, binadamu alikuwa na uwezo wa kuzungumza na Muumba wake, kitu ambacho Wanyama wote hawana.
Hebu, tumtazame Binadamu kiakili, kimaadili, na kijamii.
Kiakili, mtu ameumbwa kama wakala wa busara. Kwa maneno mengine, mtu anaweza kuchagua nini anataka kufanya kwa kutumia fikra yakinifu na/au pevu. Kwa kufanya hivyo, mtu ameonyesha uhuru wa akili ambayo Mungu anao. Mfano, mtu anapo tengeneza mashine, anapoandika kitabu, fanya mambo mbalimbali, huko ndiko kuna ashiria neno la kufanana na Mungu, maana Mungu aliumba vitu vyote na sasa binadamu anaonyesha ustadi wa akili pevu kwa kufanya mambo ya uvumbuzi katika sura ya Mungu.
Kimaadili, mtu aliumbwa kwa uadilifu na kutokuwa na hatia ya dhambi, huo ni mwaonekano wa utakatifu wa Mungu. Mungu akaona kila alichokifanya ( pamoja na uumbaji wa Mwanadamu) alikiita kuwa ni "kazi nzuri sana" (Mwanzo 1:31). Dhamiri zetu au "dira ya maadili yetu" ni alama ya awali ya hali tuliyo kuwa nayo. Binadamu tumetunga na kuandika sheria za kutuongoza na uovu, sifa na tabia nzuri , nk, hayo yote ni kuthibitisha ukweli kwamba sisi tulifanywa na/au umbwa katika mfano wa Mungu mwenyewe.
Kijamii, mtu aliumbwa kwa ajili ya ushirika na/au kushirikiana. Huu ni uthibitisho kuwa Mungu ni Utatu ambao ni asili ya upendo wake. Katika Bustani ya Edeni, Mtu alikuwa na uhusiano na Mungu (Mwanzo 3:08 ina maana ushirika na Mungu ), na Mungu alifanya mwanamke wa kwanza kwa sababu "si vema huyo mtu awe peke yake " (Mwanzo 2:18). Kila wakati mtu anapo oa, hufanya urafiki na huyo aliye muoa, huzaa watoto na kuwa na familia hayo yote ni kutuonyesha ukweli kwamba sisi ni tulifanywa katika mfano wa Mungu.
Sehemu ya kuumbwa kwa mfano wa Mungu ni kwamba Adam alikuwa na uwezo wa kufanya uchaguzi kwa huru. Adam alipewa haki ya kuchangua mema au mabaya, uhuru huo ni sehemu ya mfano wa Mungu.
Ndugu msomaji, nategemea leo umefahamu kidogo maana ya kuumbwa kwa mfano wa Mungu ni katika Roho na si Mwili au mwonekano wetu. Mungu ni Roho. Je wewe ni nani?
Katika Huduma yake
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW