Tuesday, September 6, 2016

KUMBE MAJINI HAYANA DINI ISIPOKUWA NI UISLAMU TU

Maneno haya tunayapata katika kitabu cha “ULIMWENGU WA MAJINI NA VITUKO VYAO” kilichoandikwa na sheikh Said Hamis Mkama. Phone namba +255754913480 DSM.
E.mail:mkamasaid@yahooo.com
Katika uk. wa 6 Sheikh anasema.
Ayah hii ni uthibitisho jinsi majini yanavyoshirikiana na wanadamu katika baadhi ya mambo kama Mwenyezi Mungu anavyosema.
”Na sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu mimi” (Quran 61:56 Surat Adh-dhaariyaat”)
Hiyo ndiyo hali halisi ya ushirikiano baina ya majini na Binadamu, kwa kweli majini tunajumuika nao katika mambo mengi kama vile Ibada, au kusikiliza Darasa bila ya sisi kuwaona, majini kitabu chao kwa sasa ni Quran iliyoteremshwa kwa mtume Muhammad (s.a.w)
KWA MUJIBU WA KAULI HIYO NI DHAHIRI KUWA MAJINI YANA USHIRIKIANO MKUBWA SANA NA WAISLAMU WENZAO WA KIBINADAMU kwa kuwa Sheikh anatuambia kuwa huwa wanajumuika nao katika Ibada na kusikiliza Darasa, pia Sheikh anaendelea kutuambia kuhusu Majini hayo ni namna gani ambavyo hayana imani yo yote zaidi ya Uislamu, katika Uk. wa 30 Sheikh Mkama anasema.
”Miongoni mwa mwa vituko vya majini ni pamoja na kujipa majina matukufu, kama vile Sharifu, Sheikh, Walii, Ruhani na mengine mfano wa hayo, vile vile majini hudai wanatoka miji mitakatifu kama vile Madina, Jiddah, Makkah, Hadharamaunt, na miji mingine mfano wa hiyo. Vile vile majini hudai vyakula vinavyotumiwa na miji hiyo kama vile Tende, Halwa, na mara nyingi hupenda adhana, Dhikri, Quran, na Swala”
Sheikh anaendelea kutupa habari katika uk. wa 31 anasema.
” Ibada iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, jambo hilo limesababisha wasiokuwa Waislamu kuikashifu Dini ya kiislamu kwa kudai ni dini ya majini. Hatupingi, kwani majini wapo waislamu, na wala hawana kitabu ila Quran na hawana mtume ila Muhammad (S.a.w)”
KWA HIVYO TUNAFAHAMISHWA KUWA MAJINI HAYANA KITABU ISIPOKUWA NI QURAN, AKIMAANISHA KUWA IMANI YAO NI YA KIISLAMU TU KWA KUWA QURAN NDIYO MUONGOZO WA WAISLAMU WOTE DUNIANI, NA PIA SHEIKH ANAENDELEA KUTUPA HABARI YA KUWA JINI HAWEZI KUMPANDA MUISLAMU NA AJITAMBULISHE KUWA YEYE NI KIONGOZI WA IMANI YA KIKRISTO AU KUDAI MIJI YA WAKRISTO KATIKA UK. WA 32 ANASEMA:
”Kwa hivyo siyo rahisi Jini amuingie muislamu na aseme yeye ni Papa, au Askofu, Mchungaji, Padri, Kadinal, wa kanisa aidha Pentecoste, Sabato, Romani Catholic, Lutheran, Anglican, au Moravian,au kutaja miji kama vile Paris, Washington, London, Roma, nk. Au kuomba asomewe kitabu cha Biblia, au aseme asomewe 1 Wakorinthio au Waefeso au Mathayo, nk. Au kudai misa kama vile pasaka, krismas, na mengineyo, au kuanza na haleluya, badala yake husema Assalaam alaykum”
HATA MIMI NAKUBALI NI KWELI KABISA JINI HAWEZI KUYATAKA HAYO AMBAYO YAPO KATIKA IMANI YA KIKRISTO KWA KUWA MAJINI HAYANA KITABU ILA QURAN NA HAYANA MTUME ILA MUHAMMAD, MAANA MUHAMMAD NI MTUME WA MAJINI, NA PIA MAJINI HAYO HUWA YANATOA KHUTBA YA MWISHO KABLA YA KUINGIA MWEZI WA RAMADHANI KAMA AMBAVYO SHEIKH ANATUPA HABARI HIYO KATIKA UK. 32 MWISHONI MWA UK. HUO
Hotuba ya mashetani mwezi wa shaabani karibu ya ramadhani huwa kama ifuatavyo, “Assalaam alaykum, umeshuka kutoa taarifa, karibu itakuwa hatushuki kwa vile mwezi wa toba umekaribia na sisi mwezi wa toba hatufanyi kazi tunamuomba Mwenyezi Mungu akujalieni mfunge salama tutakutana mfungo mosi. Kwa hiyo kilinge kifungwe na kisifunguliwe ila kwa Tawassul na Maulid”
HAYO NDIYO MAMBO YA MAJINI A.K.A MASHETANI NAYO HUWA YANAFUNGA MWEZI WA TOBA NA KUSITISHA KUFANYA KAZI NA NDIYO MAANA MWEZI WA RAMADHANI MAOVU HUWA HAKUNA MAKAHABA, MAJAMBAZI NK/ HUWA WAKO RIKIZO KWA KUWA WACHOCHEZI WA MAOVU HUWA WAPO KATIKA MFUNGO WA RAMADHANI.

Published by Abel Suleiman Shiliwa

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW