Muhammad kuna wakati alirogwa: "Ilielezwa na ‘Aisha: nguvu za kimazingaombwe zilifanywa dhidi ya Nabii kwa hiyo akaanza kufikiri kwamba alikuwa akifanya kitu ambacho kwa hakika hakuwa akikifanya. Siku moja alimwomba akimsihi (Allah) kwa kipindi kirefu na kisha akasema, ‘Najihisi kuwa Allah amenivuvia jinsi ya kujitibu mwenyewe.’…" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sehemu ya 10 na.490 uk.317. Pia soma juzuu ya 4 sehemu 34 na.400 uk.267, juzuu ya 8 sehemu ya 56 na.89 uk.56-57, juzuu ya 8 sehemu ya 59 na.400 uk.266-267. juzuu ya 7 sehemu ya 47-49; na.658-660 uk. 441-443.
Kuna habari zaidi katika maelezo haya. Ilielezwa na ‘Aisha: Nabii aliendelea kwa kipindi hiki na kile alidhani kuwa alikuwa ameshajamiiana na mkewe, lakini kwa hakika alikuwa hajafanya hivyo. Siku moja aliniambia, "O ‘Aisha! Allah amenielekeza kuhusu jambo hili nililomwuuliza. Ndipo waliponijia wanaume wawili, mmoja wao alikaa karibu na miguu yangu, aliyekuwa kichwani pangu akauliza (huku akinisonda kwa kidole) ‘Kuna tatizo gani na mtu huyu?’ Yule mwingine alijibu, ‘Lubaid bi A’sam." Wa kwanza akauliza, ‘Ni malighafi gani ilitumika.’ Mwingine akajibu, ‘ngozi ya sehemu ya kiume ya mti wa tende na suke lake pamoja na nywele zilizoshikamanishwa pale, na Kutunzwa chini ya jiwe katika kisima cha Dharwan.’" Kisha Nabii alikwenda kwenye kisima na akasema, "Hiki ni kisima sawa na kile nilichooneshwa kwenye ndoto. Vilele vya tende za mtende ule zilionekana kama vichwa vya mashetani, na maji yake yalionekana kama mvuke wa Henna."…’Aisha aliongeza, "(Mwanamazingaombwe) Lubaid bin A’sam alikuwa mtu kutoka Bani Zuraiq, na mshirika wa Wayahudi." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sehemu ya 56 na.89 uk.57 Pia soma Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sehemu ya 59 na.400 uk.266.
Labid bin el-Asam Myahudi alimweka Muhammad chini ya kupiga ramli. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3435 uk.60-61.
Muhammad alirogwa Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5428-5429 uk.1192-1193; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 4 na.1888 uk.411.
Pia ikiwa mtu alisema uongo kwa kukusudia kwa Muhammad, hatima ya watu hao ilikuwa Jehanam (akhera). Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3754 uk.161-162, pia Abu Dawud juzuu ya 3 sehemu ya1372 na.3643 uk.1036. Kwa hiyo, kwa kuzingatia hili, Muislam anapaswa kuwa mwangalifu ikiwa atasema kitu anapaswa kuamini na kufuata yote ya Bukhari, Sahih Muslim, Ibn-i-Majah, ambayo hujenga mengi yaliyo msingi wa Sharia ya Muislam.
Muhammad aliwapa Waansar mazingaombwe [kama vile albadiri] kwa ajili ya kuondoa sumu ya inge. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5442-5444, 5448 uk.1192, 1196.
Baadhi ya mazingara ni sawa, kwa sababu Sa’id bin Jubair alitumia hirizi alipoumwa na inge. Alijifunza kwa Muhammad. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.625 uk.141.
Muhammad alitumia ndumba [nguvu za kimazingaombwe] dhidi ya jicho ovu na wanyama jamii ya mjusi wenye sumu Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3525 uk.48.
Muhammad alimpa ‘Aisha ndumba ili kutibu jicho ovu. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na. 5445,5447-5450 uk.1196.
Muhammad aliamini katika jicho ovu, na kulikuwa na hirizi dhidi yake al-Tabari juzuu ya 39 uk.134.
No comments:
Post a Comment