Sunday, August 14, 2016

MSICHANA INITIATIVE: YAFICHUA MATUMIZI YA SHARIA ZA KIISLAMU KATIKA SHERIA ZA TANZANIA

Msichana iniative, ni Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuwatetea watoto wa kike katika masuala mbali mbali. Hivi karibuni Taasisi hiyo ilifungua kesi ya Kikatiba yenye lengo la kupinga sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto wa kike aolewe akiwa na miaka 15. Katika kesi hiyo Msichana Iniative iliomba Mahakama Kuu itamke kwamba msichana kuolewa chini ya mika 18 ihesabike ni kosa.

Mahakama Kuu ilikubaliana na ombi la watetezi hao na kutamka kuwa ni kosa binti kuolewa akiwa na miaka 15, huku makahakama hiyo ikiipa Serikali mwaka mmoja kurekebisha mapungufu hayo yaliyomo katika sheria hiyo kwa kutamka kwamba umri sahihi wa kufunga ndoa ni miaka 18 kwa wote wavulana na wasichana. 

Imeripotiwa kwamba Serikali ya Tanzania inakusudia kwenda Mahakamani kukata rufaa ya hukumu hiyo. Yaani ni kama Serikali inasema umri huo wa miaka 15 ni sahihi. Lakini swali linaloumiza kichwa ni kwamba ikiwa umri huo ni halali ni kwanini mtoto mwenye umri huo huo asiruhusiwe kupiga kura hadi afikishe miaka 18 wakati tendo la kura ni la muda tu na ndoa ni ya kudumu?
Sheria za Tanzania, zinatambua kwamba mtu mwenye umri wa miaka 15 ni mtoto asiyeruhusiwa hata kupiga kura. Lakini pia anahesabika kuwa yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake.

Waislamu Tanzania wanasema sheria hiyo inayotamka kwamba msichana aolewe hata akiwa na miaka 15 ilitungwa kutokana na ushauri wa wazee wa Kiislamu wakiongozwa na Sheikh Marehemu Muhammad Ali al Bukhri wakati wa kutunga sheria hizo. 

Kwa muda mrefu sheria hiyo imepigiwa sana kelele na asasi mbali mbali zikiipinga sheria hiyo kwa kuiona inakiuka haki za binadamu ikiwemo kumnyima elimu binti anayetamani kusoma kwa kuruhusu wazazi wake kumuoza hata akiwa na miaka 15 tu.

Swali kubwa linalojitokeza ni kwamba ni kwa nini baada ya hukumu hiyo kutolewa vyombo vya habari vya Kiislamu vya hapa Tanzania vinailalamikia sheria hiyo kwa kuiita hujuma dhidi ya Uislamu?

Wanasema, “ si haki kuigusa sheria nyeti kama  hiyo bila kushirikisha wadau wote, jambo walilolitafsiri kuwa ni sawa na kuihujumu sheria ya ndoa ya Kiislamu.”

Katika Uislamu mmoja wa wake za Mohammad aitwaye Bi Aysha aliolewa na Mtume wa Waislamu Mohammad akiwa na miakla 6 huku yeye Mohammad akiwa na miaka 53 na akaanza kushiriki naye tendo la kujamiiana naye akiwa ana miaka 10 huku Mohammad akiwa na miaka 57.

Kwa hiyo sharia za Kiislamu zilizotolewa kupitia ushauri wa wazee wa Kiislamu kuhusiana na suala nyeti la ndoa ndilo limekuwa kikwazo cha mabadiliko ya haraka ya sheria hiyo kandamizi dhidi ya wasichana.

Serikali kila wakati imekuwa ikishauriwa kuibadilisha siku ya Jumapili kutoifanya siku ya kupiga kura kwa sababu ni siku ya ibad kwa baadhi ya Wakristo, mpaka leo imegoma, lakini inaonekana iko tayari kwenda makahama kuu kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kwa lengo la kutetea maslahi ya Uislamu badala ya maslahi mapana ya taifa.

Daniel Mwankemwa
Dar es Salaam
04 Agosti, 2016                                          

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW