Somo: Mapepo ni nini?
Lengo Kuu: Uhusiano Baina ya Mtu na mapepo
Lengo Mahsusi: Kujua namna ya kuzishinda roho za kipepo na kazi zake.
Uhusiano Baina ya Mtu na mapepo.
Bwana Yesu asifiwe sana,
Ndugu zangu wapendwa, karibu katika mwendelezo wa somo letu. Katika sehemu iliyotangulia, tulijifunza dhana ya pepo, asili na mkuu wa mapepo. Pia, tuligusia kwa ufupi juu ya utiifu wao juu ya Mungu na hatua ya kuchukua ili kukabiliana na uhalifu unaoendelezwa na mapepo kupitia maombi, toba na kulishika neno la Bwana.
Ndugu mpendwa, katika sehemu hii, tutachunguza Uhusiano uliopo baina ya mtu/binadamu na mapepo.
Tunaposema uhusiano katika muktadha huu, tunamaanaisha, vitu vinavyoweza kumkutanisha mwanadamu na pepo/ roho wabaya.
Yafuatayo ni baadhi ya maeneo yanayoweza kuwakutanisha binadamu na mapepo:-
(a) Sadaka- mwanadamu katika kukamilisha ibada zake, huweza kujikuta anatoa sadaka kwa mapepo. Tukio hili huweza kudumisha uhusiano baina yake na pepo. Zoezi hili, linafahamika sana kama tambiko, amabapo zawadi za wanyama, pombe, mazao mbali mbali na pesa pia hutolewa kwaajili ya masuala ya kiibada.
Sambamba na hili, wakuu wa ibada hizi, hujihusisha na shughuli za uaguzi, uganga, utabili na kubashiri,ramuli n.k.
Sambamba na hili, wakuu wa ibada hizi, hujihusisha na shughuli za uaguzi, uganga, utabili na kubashiri,ramuli n.k.
Kwakufanya ibada hizi,mwanadamu hujifungamanisha na mapepo/ roho wachafu na kuongozwa nao.
Mara nyingine, watu hufanya ibada hizi wakidhani wanamwabudu Mungu na sadaka hizi wanamtolea Mungu, kumbe siyo kweli (Kumbukumbu la Torati 32:17).
Ndugu zangu, ibada hizi ni machukizo kwa Mungu na hapendezwi nazo. Mungu huchukia ibada hizi, yeye hafurahii ibada za namna hii kwakuwa ni ibada za mashetani.(1Wakorintho 10:20-30)
(b) Dhambi na Upagani- huu ni mlango mkuu wakuwanganisha watu na mapepo. Watu wengine hudhania kuwa wapagani hawatahukumiwa, ndugu yangu hukumu ipo tuu, ili mradi tu wewe ni binadamu, lazima hukumu ipo. Kujitenga na Mungu kwa kutenda dhambi adhabu yake ni hukumu, na hata mpagani atahukumiwa kwa dhamili yake. (1Timotheo4:1&2). Ndugu mpendwa, kubali leo umpokee Yesu, awe Bwana mwokozi wako, uwe huru.
(c) Kutii mafundisho ya uongo- mafundisho ya uongo ni yote yanayoenda kinyume na mwongozo wa Mungu. Kwa kuyatii, basi ni dhambi, na hukumu ya dhambi ni mauti. Kutolifata neno la Mungu kama lilivyo ni kufuata mafundisho ya uongo. Ndugu, tambua ya kuwa neno liko wazi na limefunuliwa kwa wote, hakuna atakayesema hakujua. Kila kona leo, kuna dini nyingi amabazo nyingine, hazifundishi kweli ya Mungu kama ilivyo, jiepushe na kujitenga na roho hizo, (1Timotheo 4:3-5).
(d) Kuyafuga- hii ni hali ya kukaa nayo. Njia hii, hutumiwa aidha kwa woga au kwa kuyapenda. Ndugu, hakuna urafiki kati ya pepo na mwanadamu. Daima lengo la pepo ni kuharibu na kuua. Kuna watu wanafuga mapepo, wengine wanayatumia kiganga, wanapagawa mapepo n.k. hili hufanaya roho hizi zifanye masikani ndani ya mtu, ndani ya uzao wake, mali, shamba na ahata mifugo (Mathayo 8:30-32).
Ndugu mpendwa, Kwa kuyapa nafasi mapepo kuwepo katika familia yako, hutoa mwanya wa kuitesa familia kizazi hata kizazi. La msingi hapa ni kuziamuru hizi roho ziondoke katika familia yako. Omba kwa vita na kukemea, ujitenge, uitenge familia yako, uzao wako, mali zako, shamba, biashara, mifugo na kila kitu, kiwe huru. Kikabidhi mikononi mwa Mungu awe Bwana na Mlinzi wako na kila kitu chako.
Je, mtu/ binadamu hupataje mapepo? Chanzo/asili yake ni nini? Endelea kufuatana nami toleo lijilo......Somo: MAPEPO NI NINI? FUATILIA [SEHEMU YA TATU]
No comments:
Post a Comment