Lengo Kuu: Kujua Mapepo na kazi zake.
Lengo Mahsusi: Kujua namna ya kuzishinda roho za kipepo na kazi zake.
MAPEPO
Ni roho chafu, roho za mashetani, ziwaingiazo watu ili kuwatesa kwa magonjwa na mateso anuwai.
Ni roho chafu, roho za mashetani, ziwaingiazo watu ili kuwatesa kwa magonjwa na mateso anuwai.
“Naye Yesu akisha kuona kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi,mimi nakuamuru mtoke huyu, wala usimwingie tena”(Marko 9:25) pia (Mt 4:24 &7:22).
Sifa kuu ya Mapepo ni kuwa, hayana umbo, nyama wala mifupa. Ni roho, na roho haiwezi kuwa na mwili wala mifupa (Luka 24:39)”....ni shikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili wala mifupa...” Isipokuwa, Huweza kuingia ndani ya mwili wa kiumbe hai na kuvaa umbo na sura yake.
Kumbuka: Hii ziyo mizimu au Roho za wafu. Mtu akishakufa, roho yake haina uwezo wa kurudi duniani. Usidanganyike. Fuatilia kisa cha tajiri na masikini, roho ya tajiri haikuweza kurudi duniani. (Luka 16:27-31)
Wala, roho hizi (mapepo) siyo malaika walioasi, kwa kuwa wao wametekwa na tayali wako kwenye kamaba zao wakingoja siku ya hukumu (Yuda 1:16,2Petro 2:4)
Swali: Je, mkuu wa mapepo ni nani? Ili kupata jibu fuatana nami.....
Biblia katika kitabu cha Marko 3:22, imeeleza wazi, aliye mkuu wa mapepo. Naye ni Beelzebuli. Hili ni dhahili, kuwa huyu ndiye mkuu wa mapepo na ndiye pepo mkuu.
Je, mapepo yanamfahamu Mungu, yanamchukuliaje?Mepepo yanafahamu fika kuwa Mungu yupo. Tena yanajua kuwa Mungu anauwezo na nguvu zaidi yao, ndiyo maana humwogopa. (Yakobo 2:19).”Wewe waamuni ya kuwa Mungu ni mmoja; watenad vema.mashetani nao wanaamini na kutetemeka”
Kama vile mapepo yanavyomogopa Mungu na hata kutetemeka, kadharika mtu asiye na roho wa Mungu, huyaogopa mapepo. Je, hujaona mtu anaogopa kulala peke yake ndani, pengine hata mchana huogopa kubaki nyumbani peke yake wengine wanapokuwa hawapo? Hata wanafunzi wa Yesu, kabla ya kumpokea Roho Mtakatifu, walikuwa waoga juu ya pepo. (Mathayo 14:26,Luka 24:37). Hivyo, watu wote, wanapaswa kuokoka na kupokea nguvu ya Roho mtakatifu ili kuwashinda mapepo na kazi zao zote.
Zingatia hili, mapepo yananao uwezo wa kutenda miujiza kupitia watu, vitu na hata wanayama ili kuwadanganya watu na miujiza yao ya uongo (Ufunuo 16:14).
Hakika, kazi za mapepo zikidhibitiwa vilivyo, kazi zote za adui/ shetani zitakuwa zimeshindwa na maangamizi yote ya kipepo hayatapata nafasi tena. Amen.
Je, kuna uhusiano gani kati ya watu/ binadamu na mapepo? Chanzo/asili yake ni nini? Endelea kufuatana nami toleo lijilo....... Somo: Mapepo ni nini?
FUATILIA SEHEMU YA PILI
No comments:
Post a Comment