Sunday, August 14, 2016

KWANINI WAISLAM WANATUMIA BIBLIA KUTHIBITISHA UTUME WA MUHAMMAD?




TUNAZIDI KUCHAMBUA HOJA ZA MIHADHARA YA KIISLAMU;
LEO TUANGALIE JUHUDI ZA WAHADHIRI KUTAFUTA UTABIRI WA MUHAMMAD MWANA WA ABDALAH KWENYE BIBLIA:
Nabii Isaya ameandika kwamba: Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi (Isaya 29:12).
Waislamu walipoona andiko hili wakadhani kuwa tayari wameshapata ushahidi kuwa Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia kwa kuwa Muhammad alikuwa ni mtu ambaye hakuwa amesoma.
Ukifuatilia sura nzima ya 29 na mantiki iliyozaa mstari huu wa 12, unaweza kuishia kucheka tu, ingawaje hili si jambo la kucheka.
Wanachofanya Waislamu ni upotovu mkubwa ambao unaangamiza mamilioni ya watu wa Mungu milele katika jehanamu ya moto. Watu wanaaminishwa uongo na wao wanaukumbatia kana kwamba ni ukweli.
Kwa ujumla, ukisoma sura ya 29 ni sura ambayo inatamka hukumu juu ya Ariel (Yerusalemu) kutokana na uasi wao juu ya sheria na maagizo ya Mungu, Yehova. Hebu tusome sura hiyo kwa Taratibu:
1 Ole wa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi alifanya kituo chake ndani yake; ongezeni mwaka baada ya mwaka; sikukuu na zirudi wakati wake,
2 ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli.
3 Nami nitapiga kimo juu yako pande zote, nitakuhusuru kwa ngome, nami nitajenga maboma yakuzunguke.
4 Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong'ona toka mavumbini.
5 Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula.
6 Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.
7 Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, nao wamwudhio, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.

8 Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
9 Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo.
10 Kwa maana Bwana amewamwagieni roho ya usingizi, amefumba macho yenu, yaani, manabii; amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji.
Mbali na hukumu hizo hapo juu, Mungu bado akaendelea kusema kuwa, kutokana na uasi wao, hata neno lake hawatalielewa. Yaani hawataweza kusikia au kujua Mungu anasema nini hata kama watasoma au kusikia neno lake. Hii ni pamoja na wale ambao ndio wanatarajiwa kuwa wenye kuelewa neno hili – yaani manabii na waonaji – ukiachilia mbali wale wasio na maarifa juu ya neno la Mungu, yaani watu wa kawaida. Kwa hiyo, anaendelea kusema:
11 Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri;
12 kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.
Sasa basi, kama kweli Muhammad ndiye anayetajwa kwenye Isaya 29:12, kimantiki ina maana kuwa yeye ni kati ya wasioelewa lolote kwa kuwa wako chini ya hukumu ya Mungu; maana kama tulivyoona, sura hii ni tamko la hukumu ya Mungu kutokana na uasi. Si vibaya hata hivyo! Ndiyo maana nikasema kwamba unaposoma hoja hii ya Waislamu unaweza kuishia kucheka tu.
Lakini ebu tazama CHUO hiki ni WATU humpa mtu asiye na maarifa? Sasa kama chuo hiki kinakusudiwa ni Qurani? Je, watu hawa waliompa Muhammad chuo hiki ni kina nani? hivi kumbe Quran imetoka kwa WATU wakumpa Muhammad?
Hata hivyo, kwa kuwa sasa Muhammad ni nabii asiyeelewa chochote kutokana na kuwa chini ya hukumu ya Mungu kulingana na mantiki ya andiko hili, maana yake ni kuwa ujumbe alioleta kwa wanadamu hautoki kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi. Ndiyo! Labda kama, kwa makusudi tu, hutaki mantiki iliyopo. Kwa nini basi umfuate mtu wa namna hiyo?
Fanya maamuzi; nafsi yako ni ya gharama Mpendwa

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW