Mwalimu Chaka
Leo napenda tuangalie baadhi ya mafundisho na upindaji wa maandiko ya Mungu kama tunaona katika Injili hii ya Barnaba.
Utabiri wa Ujio wa Muhammad katika Injili ya Barnaba.
Utabiri wa Ujio wa Muhammad katika Injili ya Barnaba.
Katika Biblia tunasoma jinsi Yohana Mbatizaji alitangaza ujio wa Bwana Yesu:
"Sasa huu ulikuwa ni ushahidi wa Yohana, Wayahudi wa Yerusalemu walipowatuma makuhani Walawi, na kumwuliza yeye ni nani. naye alikiri, wala hakukana, alikiri kwamba "Mimi siye Kristo." Nao wakamwuliza, " Ni nani basi? U Eliya wewe?" Akasema, "Mimi siye." "Je, wewe u Nabii yule? "Yeye akawajibu, "La" Basi wakamwambia, "Wewe u nani? ili tuwapelekee jibu wale waliotutuma?, Wanenaje juu ya nafsi yako?" Yohana alijibu kwa maneno ya nabii Isaya, "Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Nyoosheni njia ya Bwana.’”
"... siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, "Tazama Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:19-29)
Katika Injili ya Barnaba tunaona kisa hiki kimebadilishwa na kumfanya Yesu kutabiri kuja kwa Muhammad, kama Qur'an inasema Isa alifanya (Qur'an 7:157, 61:6).
"Waliona wengi ambao walikuwa wanafuata Yesu, kwa ajili hiyo wakuu wa makuhani wakafanya shauri wao kwa wao ili wamtege Yesu kwa maneno yake. Kwa hiyo wao waliwatuwama Walawi, na baadhi ya walimu wa Sheria kumwuliza, wakisema: "Wewe ni nani" Yesu alikiri, alisema ukweli: ". Mimi sio Masihi" Wakasema: "Je, wewe ni Eliya au Yeremia, au mmojawapo wa manabii wa kale?" Yesu akajibu: "Hapana" Nao wakamwambia, "Wewe ni nani Sema, ili tupate kutoa ushuhuda kwa wale waliotutuma?." Kisha Yesu akasema: "Mimi ni sauti ya mtu apitaye kwa njia yote za Yudea, kwa kilio akisema: “Tayarisheni njia ya Mjumbe wa Bwana, kama ilivyoandikwa katika Isaya." (Sura. 42)
"Ndipo kuhani: akamuuliza "Ataitwaje Masihi atakapokuja ... " Yesu akamjibu, "jina la Masihi ni la kupendeza ... Muhammad, ndilo jina lake lenye kheri" (Surah. 97).
Hapa mwandishi wa Injili ya Barnaba anadai Masihi atakeyekuja ni la kupendeza, yaani Muhammad jina lenye kheri" !!! eti Muhammad ndiye Masihi!!!! ili tutalichambua mbeleni
JE YESU NI MWANA WA MUNGU ?
Katika Biblia jina ‘Mwana wa Mungu’ ni jina lililopewa kwa taifa la Israeli (Kutoka 4:21-23) na pia kwa wafalme wake wote (2 Samweli 7:11-14, Zaburi 2).Kwa mujibu wa Biblia Yesu ni mwana pekee atokaye kwa Baba aliyejaa Neema na kweli. Maandiko yapo mengi kuhusiana na hili. Wanafunzi walikiri ili pia.
"Basi Yesu akaenda pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi wake akasema, "Watu unena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? " Wakasema, "Wengine wanasema kuwa u Yohana mbatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya,. Na wengine, Yeremia au mmojawapo wa Manabii." Akawauliza. "Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?" Simoni Petro akajibu, "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai." Yesu akamwaambia, "Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana mwili na damu, havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni." (Mathayo 16:13-17)
Kinyume na Biblia, Qur'an inafundisha kuwa Yesu sio Mwana wa Mungu (Qur'an 9:30). Katika Injili ya Barnaba tunaona kwamba Mwandishi wake Anabadilisha kukiri kwa Petro ili kuendanishe na kile Qur'an inasema:
"(Yesu) aliwauliza wanafunzi wake, akisema:"Watu wanasema mimi ni nani" Wakasema: "Baadhi yao wanasema kuwa u Eliya, wengine Yeremia, na wengine mmojawapo wa manabii wa kale." Yesu akajibu, "Ninyi; nanyi mnasema mimi ni nani?" Petro akajibu, "Wewe ndiwe Masihi, Mwana wa Mungu." Kisha Yesu kwa hasira, akamkemea akisema: "Ondoka na utoke mbele yangu" (Injili ya Barnaba Sura. 70)
Katika Sura ya 222, ambayo ndiyo sura ya mwisho ya Injili ya Barnaba tunasoma:
"Baada ya Yesu kuondoka (baada ya kutoka mafichoni kwa njia ya dirisha la nyumba kwenye bustani ya Gethsemane) wanafunzi walitawanyika kwa njia na sehemu mbalimbali za Israeli na kote duniani, na kwa kweli walichukiwa na Shetani, walipata adha na matezo, kwa mazingizio ya uwongo. Ikawa baadhi ya watu waovu., waliondoka na kujifanya kuwa wanafunzi, wakahubiri kwamba Yesu alikufa lakini hakufufuka Wengine wakahubiri kwamba kweli alikufa, lakini akafufuka. Wengine walihubiri na bado wanahubiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, miongoni mwao ni Paulo kudanganywa. ".
Mwandishi wa Injili ya Barnaba anafanya juhudi kusahihisha Injili ya kweli iliyotangulia na Paulo. NIngependa kuuliza Ni lini na ni kwa jinsi gani Mwandishi alipata ufahamu kwamba wanafunzi hao walikuwa wametawanyika katika sehemu mbalimbali duniani? Swali hili Naliacha wazi, lakini kwa urahisi tunaweza tuIkalijibu, kwa maana sisi kama Wakristo tunatambua kwamba ni ubunifu mwingine wa bandia .
Mwandishi wa Injili ya Barnaba anafanya juhudi kusahihisha Injili ya kweli iliyotangulia na Paulo. NIngependa kuuliza Ni lini na ni kwa jinsi gani Mwandishi alipata ufahamu kwamba wanafunzi hao walikuwa wametawanyika katika sehemu mbalimbali duniani? Swali hili Naliacha wazi, lakini kwa urahisi tunaweza tuIkalijibu, kwa maana sisi kama Wakristo tunatambua kwamba ni ubunifu mwingine wa bandia .
Fuatilia sehemu ya Nne
No comments:
Post a Comment