Friday, August 26, 2016

KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS? (SEHEMU YA NNE)



Mwalimu Chaka
Tunazidi Kuichambua Injili Hii ambayo inajaribu kuhusishwa na Mtume Barnaba.
Leo tuangazie Mwandishi.
MWANDISHI: Muislamu ambaye alikuwa na uelewa kiasi wa Biblia Kuna uhakika kabisa na wa kutosha kutibitisha kwamba mwandishi wa Injili hii bandia ni Muislamu. Mtu yeyote akisoma kwa makini kitabu hiki kinachojulikana kama Injili ya Barnaba atapata kina mguso wa Kiislamu ndani yake.
i) Kwanza, kitabu hiki kina maelezo ya kufanana na Kristo. Katika sura ya 112 inasema: "Jua, ewe Barnaba, ya kwamba mimi ninahofia. Mmoja wa wanafunzi wangu atanisaliti kwa vipande thelathini vya fedha. Zaidi ya hayo, nina uhakika kwamba yule atakayenisaliti atauawa kwa jina langu, kwa sababu Mungu ataniinua juu ya nchi na kubadilisha sura ya huyo atakayenisaliti ili kila mmoja
aweze kufikiri yeye kuwa ni mimi. Na wakati akifa kifo kibaya na cha kutisha, nitabaki na aibu hiyo kwa muda mrefu duniani. Lakini wakati Muhammad, mtume mtakatifu wa Mungu, akija, aibu hii itaondolewa kwangu” "(Surah 112:13-17).
Habari hizi ni sanjari na mafundisho ya Kiislamu ya Zama za miaka ya kati
ii) Kifo cha Yesu. Biblia inafundisha kuwa Yesu alisulubiwa na kufa. "Kisha (Pilato) akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Lakini alikuwa kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa ili asulubiwe. ... Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye Simoni, wakamshurutisha auchukue msalaba. ... Walipikwisha kumsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kura ... ‘Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akaitoa roho yake". (Mathayo 27:26-50.)
Kinyume na Biblia, Qur'an inafundisha kuwa Isa ambaye anadaiwa kuwa ndiye Yesu hakusulubiwa na wala hakufa msalabani (Qur'an 4:156-157). Tunaona tena jaribio, katika Injili ya Barnaba la Mwandishi akijaribu kubadilisha tukio la kusulubiwa kwa Yesu ili kuendana sambamba na kile Qur'an inasema:
"Mungu alitenda ajabu hata, Yuda akabadilishwa kisura kuwa kama Yesu na hata katika usemi wake pia na askari walichukua Yuda wakamfunga ... Hivyo wale watu wakamwongoza mpaka mlima wa Kalvari, ambapo walitumia kutundika wahalifu,na ndipo wakamsulubisha Yuda "(Sura. 216-217).
Sasa hapa bila shaka ameowanisha usemi ya Qurani kuwa " Bali walibabaishiwa mtu mwingine wakamdhani kuwa Nabii Isa!!!

Mifano hii inaonyesha jinsi Mwandishi wa Injili ya Barnaba kwa utaratibu anavyojaribu kuandikwa upya Injili ya Biblia kwa kuifanya ikukubaliane na Qur'an.
Ni katika matukio adimu ambapo anafanya makosa. Tukiangalia mabadiliko haya tunaweza kuelewa malengo ambayo Mwandishi alikuwa anajaribu kufikia. Alikuwa anarudia kuandika Injili ili sasa iwe imemekubaliana na Qur'an; alikuwa anajaribu kuwashawishi watu kuwa Yesu alifundisha kile ambacho Qur'an inafundisha.
iii) Tatu, kuna madai kwamba Maandiko matakatifu yemeharibiwa. Katika sura ya 12 ananukuu Kristo kama akisema: "Kweli nawaambieni, kwamba kama kweli isingelitokomezwa kutoka Kitabu cha Musa, Mungu asingelimpa Daudi, baba yetu, Kitabu cha Pili yaani Zaburi. Na kama kitabu cha Daudi kisingeli potoshwa Mungu haziniamini kwa injili aliyoikabidhi kwangu, kwa sababu Bwana Mungu wetu habadiliki na Yeye alitamka ujumbe mmoja kwa wanadamu wote ... Wakati mjumbe wa Mungu akakapokuja atasafisha sehemu ya kitabu changu ambayo itakuwa imepotoshwa kwa na waovu” (Sura 124:8-10).
Kauli hii ni kashfa dhidi ya uhalisi wa maandiko yote Matakatifu na haiwezekani kuwa imetoka kwa Kristo, ambaye alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” (Mathayo 24:35).
Baadhi ya Waislamu wameniambia kwamba kwa kuwa Injili ya Barnaba ina baadhi ya mafundisho machache kinyume na Qur'an. Basi hii inathibitisha haikuwa imeandikwa na Muislamu kwa kuwa Muislamu asingelifanya aina hii ya makosa.
Hata hivyo, kwa sababu tu mwandishi amefanya makosa madogo na machache kuhusu Uislamu haina maana yeye sio Muislamu. Waandishi wa Kiislamu leo bado ufanya makosa madogo madogo katika maandishi yao. Hii haina maana wao sio Waislamu, ila tu ina maana wao wanajifunza, kama sisi sote pia.
Ni sawa na Mwandishi wa Injili ya Barnaba. Hivyo bado pana uwezekano mkubwa zaidi kwamba Mwandishi wa Injili ya Barnaba alikuwa Muislamu.
Fuatiilia sehemu ya tano ambapo nitajaribu kulinganisha baadhi ya mafundisho ya Injili hii dhiti ya Qurani

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW