Friday, August 26, 2016

KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS? (SEHEMU YA PILI)



Mwalimu Chaka
KUHITILAFIANA NA INJILI TAKATIFU
Kuna ushahidi mwingi kwamba Mwandishi wa Injili ya Barnaba alikuwa hana uhusiano wowote na Mitume wa Kristo, au wanafunzi wake ambao waliandika vitabu vyao wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
1.Ushahidi wa kwanza ni kutokufahamu kwa mwandishi JIOGRAFIA ya Palestina ambayo ndiyo nchi na kitovu cha masimulizi ya kidini. Anasema, “Yesu akaenda kando ya ziwa Galilaya na akapanda mashua kusafiri hadi Nazareti, mji wake mwenyewe. Kukawa na dhoruba kubwa na mashua ilikuwa karibu kuzama” (Sura ya 20:1-2). Ni vizuri kujua kwamba Nazareti iko juu ya mlima wa Galilaya, wala sio mji wa pwani, kama mwandishi anavyosema.
2. Mahali pengine anasema, “Kumbuka kwamba Mungu aliamua kuharibu Ninawi kwa sababu hapakuwa na mmoja katika mji huo ambaye alikuwa mcha Mungu. Yeye (Yona) alijaribu kutoroka Tarso, kwa kuwa na hofu ya watu, lakini Mungu akamtupa baharini na samaki akammeza na kumtupa nje karibu Ninawi” (BARNABA Sura 63:4-7). Ni jambo lanalojulikana kwamba mji wa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa Dola ya Waashuri na alikuwa umejengwa kando ya ufuo wa mashariki wa Mto Hidekeli, kwenye kijito kinachojulikana kwa jina la al-Khisr. Kwa hiyo, haupo katika eneo la bahari ya Mediterranean kama ilivyoelezwa na mwandishi huyu.
3. Mwandishi alikuwa hana ufahamu juu ya historia ya maisha ya Yesu Kristo. Katika sura ya tatu ya Injili hii ya kughushi, imeandikwa, “Yesu alipozaliwa, Pilato alikuwa Gavana wakati wa uongozi wa Rabi Anania na Kayafa .” ( Sura 3:2).
Hii si kweli kwa sababu Pilato alikuwa liwali kutoka mwaka wa AD 26-36. Anania alikuwa Rabbi mkuu kutoka AD 6, na Kayafa kutoka AD. 8-36.

4. Katika sura ya 142 imeandikwa kwamba “Masihi hatakuja kutoka ukoo wa Daudi lakini kutokana na kizazi cha Ishmaeli, na kwamba ahadi ilitolewa kwa Ishmaili, na sio kwa Isaka” (Sura 124:14). Hii ni kosa kubwa kwa sababu mtu yeyote mwenye kusoma ukoo wa Kristo katika Injili ya kweli ataona kwamba, kulingana na mwili, Yeye alishuka kutoka kwa ukoo au nyumba ya Daudi, na kabila la Yuda.
5. Mwandishi amejumlisha hadithi ambazo hazikuwa na msingi katika dini ya Kikristo. Zifuatazo ni mifano ya hadithi hizo.
a) “Wakati Mungu alisema na wafuasi wa Shetani, “Tubuni na kukiri kwamba mimi ni Muumba wenu, ‘wakamwambia, ‘Sisi tumegeuka na kuacha kukuabudu wewe kwa sababu Wewe ni mdhalimu, lakini Shetani ni mwenye haki kwa wasiokuwa na hatia na yeye ni Bwana wetu.” Basi, Shetani, alipokuwa anaondoka, akatema mate kwenye lundo dogo la udongo na Gabriel akaondoa mate yale na baadhi ya vumbi, matokeo yake akaja mtu kuwa na kitovu katika tumbo lake.” (Sura ya 35:25-27).
b). Yesu akajibu, akisema, 'Hakika mimi nalimuhurumia Shetani wakati nilipojua kuhusu kuanguka kwake na ninawahurumia watu ambao anawajaribu ili wafanye dhambi. Kwa hivyo Mimi nalifunga na kuomba kwa Mungu wetu ambaye alisema na mimi kwa kupitia Malaika wake Gabriel akisema, ‘Unataka nini, ewe Yesu, na nini haja yako?’ Mimi nikajibu, `Bwana, Wewe unajua ubaya gani Shetani imesababisha na kwamba yeye, ambaye ni uumbaji wako, anawaharibu wengi kwa njia ya majaribu yake. Kuwa na huruma, Ee Bwana.' Mungu alimjibu, Yesu. ‘tazama, mimi nitamsamehe ila aseme tu, ‘Bwana, Mungu wangu, nimekosa, nihurumie’ Na mimi nitamsamehe na kumrejesha katika hali yake ya awali.” Yesu akasema, "Niliposikia hii Nilifurahi nikiamini kwamba mimi nimefanikiwa kuleta maridhiano. kwa hiyo nilimwita Shetani, naye alipokuja Shetani aliniuliza, ‘Je nikufanyie nini yenu ewe Yesu?' Mimi nikamjibu, `Wewe utafanya hivyo kwa ajili yako mwenyewe, kwa sababu mimi sihitaji huduma yako, lakini nimekuita na ni kwa faida yako.' Shetani akajibu, `Kama hutaki huduma yangu, Sitaki yako pia, kwa maana mimi ni mbora kuliko wewe. Wewe hustahili kunihudumia mimi. Wewe umetotokama na na udongo lakini mimi ni nimetokamana na Roho.” ( Surah 51:4-20).
Hakuna mtu anayeweza kuamini kwamba hadithi hii ya kishirikina ni kutoka katika Injili ya uongozi wa Mungu. Awali ya yote, Mungu hakufurahishwa na Shetani alipoanguka na akamuondoa kutoka kwa uwepo wake. Sio sambamba na utakatifu wa Mungu kufanya mazungumzo ya maridhiano na Shetani. Pili, tangu mwanzo, Kristo aliingia katika vita visivyokoma na shetani. Biblia inasema, ‘mtu atendaye dhambi ni wa Ibilisi, maana Ibilisi ametenda dhambi tangu mwanzo. Mwana wa Mungu alidhihirishwa kwa sababu hii, ili azivunje kazi za Ibilisi (1 Yohana 3:8). Tatu, katika mapambano yake pamoja na Kristo, Shetani hakuwahi na hajawai jitokeza kusema kwamba alikuwa bora kuliko Kristo. Kinyume chake, katika mkutano huko Kapernaumu alipoamrishwa kumwaja mtu, aliyekuwa amepagawa alilia kwa sauti kubwa akasema, Acha! Tuna nini nawe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najua wewe u nani Mtakatifu wa Mungu! (Luka 4:34).
Ni vyema kukumbuka kwamba hoja hii ya Shetani kwa mujibu wa Injili ya Barnaba ni kinyume pia na Qur’ani ambayo anasema Shetani kaubwa kwa Moto (Qu 7:12) na Isa ambaye Waislamu wanadai ndiye Yesu ni Neno atakaye kwa Mungu na pia ni Roho wa Mungu. (Tazama Qur’ani 66:12, 4:171)
FUATILIA SEHEMU YA TATU

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW