Sunday, August 14, 2016

KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS? (SEHEMU YA KWANZA)

Mwalimu Chaka
SWALI: Kwa nini Wakristo Hamuitambui Injili ya Barnaba?
lililoulishwa na: Abdullah Mbwana, Mombasa.
Imetibitishwa kwamba kitabu kinachojulikana kama Injili ya Barnaba hakina uhusiano wowote na Ukristo. Ni ushahidi bandia kuhusu Injili takatifu na jaribio la kuwakilisha kwa ubaya dini ya Kikristo.
Kitabu hiki kinachohusishwa na Barnaba kilitafsiriwa katika lugha ya Kiarabu na Dr Khalil Sa'adah, kutoka nakala ya Kiingereza katika mwaka 1907.
Injili hii ilikataliwa kabisa na Wakristo kwa sababu ilikuwa ya kubuni na ya uongo.
Wale ambao waliikubali walikuwa baadhi ya madhehebu ya Waislamu. Walifanya hivyo kwa sababu rahisi sana; kwamba sehemu kubwa ya Injili hii inaunga mkono madai kwamba Kristo hakusulubiwa, lakini sura yake aliwekewa Yuda Iskarioti ambaye alisulubiwa badala yake Yesu. Lakini pia ndani ya Injili inaonekana Yesu eti akitabiri Ujio wa Nabii Muhammad huku akimtaja kwa jina
Maoni ya Wanachuoni
Wasomi ambao wamesoma kwa makini suala hili na kuchambua kitabu hiki, kwa kauli moja wamekubaliana kwamba hiki kitabu, ambacho kwa uongo kimehusishwa na Barnaba, hakikuwahi kuwepo kabla ya karne ya 15. Hii ni karibu miaka 1500 baada ya kifo cha Barnaba halisi. Kama kingeli kuwa kinapatikana kabla ya kipindi hicho, basi Wasomi wa Kiislamu kama Al-Tabari, Al-Baindhawi, na Ibn Kathir wasingelikuwa wamehitilafiana katika maoni yao juu ya mwisho wa Kristo, wala kuhusu utambulisho wa mtu ambaye ndiye aliyesulubiwa badala ya Yesu.
Kama tukirejea nakala za zamani ya Biblia Takatifu za nyuma kipindi cha kabla ya Uislamu na ambayo Qur'an inashuhudia juu ya ukweli wake, hatuoni Injili inayojulikana wala kuhusishwa na Barnaba. Wala haikutajwa katika meza ya yaliyomo, iliyoandaliwa na mababa wa Kanisa, ya vitabu ambavyo vinajumlisha Biblia Takatifu.

Utafiti wa Historia unaonyesha kwamba muswada wa awali wa Injili hii bandia alionekana kwa mara ya kwanza katika mwaka wa1709, katika milki ya Craemer, mshauri wa Mfalme wa Prussia. Kisha kikachukuliwa kutoka kwake na kuwekwa katika Maktaba Vienna katika mwaka wa 1738. Wasomi wote ambao walichunguza muswada huu wamebainisha kuwa kava yake ilikuwa katika mtindo wa mashariki ya kati na kwamba yalikuwemo maelezo mafupi katika Kiarabu. Kutokana na uchunguzi wa karatasi na wino uliotumika, inaonekana kwamba Injili hii imeandikwa katika karne ya 15 au 16.
Msomi wa Kiingereza, Dk Sale, anasema alipata nakala ya kitabu hiki katika lugha ya Kihispania iliyoandikwa na Mustafa al-'Arandi wa Aragon (Hispania), ambaye alidai yeye alikuwa ameitafsiri kutoka kwa nakala ya Kiitaliano.
Utangulizi wa nakala hii anasema kuwa mtawa mmoja aitwaye Marino, ambaye alikuwa karibu na Papa Sixtus V, alitembelea maktaba ya Papa siku moja katika 1585, na kukuta barua ya Mtakatifu Irenaeus akimkosoa Mtume Paulo kwa kutumia hoja zake kutoka kwa Injili ya Barnaba. Baada ya hapo Marino huku akiwa na hamu ya kupata hii Injili. Siku moja alikutana na Papa Sixtus V katika maktaba ya kipapa, na walipokuwa wakizungumza, Papa akalala usingizi. Mtawa huyu akaitumia nafasi hiyo, akakitafuta kitabu, akakipata na kukificha katika mavazi yake. Akisubiri mpaka Papa alipoamka na kisha kuondoka, huku kachukua kitabu hicho pamoja naye.
Hata hivyo, mtu yeyote asomayee maandiko ya St Irenaeus utapata hakuna kumbukumbu ya Injili ya Barnaba na hakuna upinzani wa aina yoyote kutoka kwake dhidi ya Mtume Paulo.
Kuna, hata hivyo, ukweli ambao kila mtu anaweza kujua. Imeandikwa katika Matendo ya Mitume kwamba Barnaba alikuwa Rafiki wa Paulo wa karibu wakati akihubiri Habari Njema katika Yerusalemu, Antiokia, Ikonio, Listra na Derbe. Barnaba pia walihubiri Habari Njema katika kundi moja na mpwa wake Yohana Marko katika kisiwa cha Kipro. Hii inaonyesha kwamba Barnaba alikuwa Muumini katika Injili ya Msalaba ambayo Paulo, Marko na Mitume wengine walikuwa wanahubiri, na ambayo inaweza kwa muhtasari kuwa sentensi moja fupi: Kristo alikufa msalabani kama upatanisho kwa ajili ya dhambi za ulimwengu na kufufuka tena siku ya tatu kwa ajili ya haki ya kila mtu aliye amwaminiye.
Kwa kuwa Injili ya Barnaba inakanusha ukweli huu wa msingi, ni wazi kuwa kitabu hiki ni uzushi tu wa kupotosha kwa hila za ujanja.
Baadhi ya Wasomi wamedhai kuwa mwandishi wa Injili ya Barnaba ni Marino aliyekuwa mtawa, baada ya kusilimu na kubadilisha jina kuwa Mustafa Al-'Arandi. Wengine wana maoni tofauti na wemeamini kwamba nakala ya Kiitaliano sio toleo asili ya kitabu hiki lakini ilikuwa imetafsiriwa kutoka asili ya Kiarabu. Mtu yeyote mwenye kusoma Injili hii ya uzushi ya Barnaba anaweza kuona kwamba Mwandishi ana maarifa mbalimbali ya Qur'an na kwamba mengi ya maandiko ni karibu sana na tafsiri halisi ya aya za Qur'an. . Fuatilia sehemu ya pili ninapoanza kuchambua Injili hii .
USIKOSE SEHEMU YA PILI

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW